NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha
Tarehe 23/6/2025
SOMO: NENO LA MAARIFA
Kutoka 31:3-4 "nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba"
Neno la Maarifa litakupa nini katika maisha yako?
● Hukuwezesha kufahamu kinachoendelea Duniani na jinsi ya kufanya kazi ili upate Mali.
● Hukusaidia kuwa Mvumbuzi na Mbunifu ili ufanye mambo yenye ubora na yatakayokuwezesha kufanikiwa.
● Utapanda daraja na kuwa Mtu Mkuu kwa sababu ni Mtendaji mzuri.
● Litakupa kujitegemea kwa kuwa kile unachokifanya kitakupa fedha na hautakuwa maskini wala omba omba. Hali hii itakufanya usiwe mkia bali utakuwa Kichwa wakati wote. Ukiwa mvivu hauwezi kumiliki kitu kwa sababu uvivu hukaa akilini na haikuwezeshi kuwaza mambo makubwa.
Kila wakati omba Roho wa Maarifa afungue macho yako ili ujue chakufanya na kuwa kama Mungu alivyokukusudia. Ukijifunza na kutafakari Biblia na mafundisho unayofundishwa itakufanya uendelee mbele lakini usipofanya hivyo utarudi nyuma.
TANGAZO
Nakuamuru uwe na Maarifa ili uweze kupata Mali; kwa Jina la Yesu.
... See MoreSee Less