KWELI ILIYO MOYONI MWAKO.
SOMO: Zaburi 51:6 “Tazama wapendezwa na kweli iliyo moyoni nawe utanijulisha hekima kwa siri”. Hakuna kitu kibaya kama Moyoni mwako ukawa unahukumiwa na dhambi au tabia fulani ambayo Moyo wako unajua kabisa kuwa unayo, lakini wewe unakaza Moyo na kusema hapana mbona nipo sawa. Fika mahali na uamue kukubaliana na hiyo hali unayoisikia ndani ya moyo wako kuwa tabia uliyonayo si sawa ili uweze kutoka hapo. Ukifika mahali ukaweza kusimama katika kweli inayosema ndani ya Moyo wako haijalishi umefanya nini ndipo utaweza kubadilika. MTUME BENSON KIKOTI – KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM, TANZANIA.
SHUHUDA
Anaitwa Anjela Anthony, anamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea, mwaka 2016 Anjela alipata neema ya kununua kiwanja na kujenga nyumba yenye vyumba vinne(4) na baada ya hapo alipokuwa kanisani mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii alimpa zawadi ya dollar 100 na kumwambia akajenge nyumba nyingine. Pia Anjela anamshukuru Mungu tena, alivyoenda kusanyiko mtumishi wa Mungu Stefan alikuwa akihubiri na kusisitiza kuwa kama kuna kitu unasikia ndani unataka ukifanye, nenda kakifanye na kitakuwa, na Anjela alikuwa anasikia ndani msisitizo wa kununua kiwanja kingine na ndipo akapokea lile neno na kulitendea kazi. Kusanyiko lilipoisha ndugu yake alimpigia simu na kumwambia amepata kiwanja
KUPOKEA ROHO MTAKATIFU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha Matendo ya Mitume 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Kipawa hutafsiriwa kama kitu kinachotolewa na kukubaliwa bila sharti ikimaanisha tendo la kupokea. Kipawa hakijakamilika mpaka pale mtu apokee kile kilichotolewa bure kwake. Swala la kipawa ni ile hali yako ya kupokea. Tutajua umepokea kipawa kwa kuona udhihirisho; kuna hali fulani, tabia na jambo litachipuka ndani yako. Watu wataanza kuona unapenda kuomba, kusoma Biblia, kwenda Kanisani na kwa njia hiyo unaruhusu Roho Mtakatifu azidi
MWAKA WA KUMILIKI
Mwaka wa kumiliki ni wa msingi sana katika maisha yako, kwa sababu ukiwa na kitu cha kumiliki utambulisho wako pia unakuwa mkuu. Kama hauna chochote cha kumiliki hata utambulisho wako unakuwa mdogo sana, hivyo namna unavyomiliki ndivyo unavyokuwa mkuu. Kwa namna unavyo miliki ndivyo utambulisho wako unavyokuwa, hivyo umiliki ni kitu cha kurutubisha utambulisho wako, pasipo kuwa na kitu cha kumiliki ni rahisi kwako wewe kuwa mtu asiye na jina. Umiliki unakusababisha uwe na hadhi; Mungu kamwe hajawahi kutembea na watu wasiojulikana, kuanzia mwanzo wa Biblia mpaka mwisho, Mungu alitembea na watu wanao tambulika, hivyo utambulisho pia ni muhimu sana