IBADA YA JUMAPILI – 29.06.2025
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA 1. Nguvu ya Msalaba 1 Wakorintho 1:18“Kwa maana neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.” Kwa wale wanaopotea, ujumbe wa msalaba ni upuzi, lakini kwa wale wanaookolewa ni nguvu ya Mungu. Lazima uelewe ni nani anayetafakari kuhusu wokovu mara kwa mara wale wanaotafakari kuhusu wokovu mara zote wanakua kiroho, kiakili, na hata kiuchumi. Lakini wale wanaopuuzia wokovu, hata kama wanadai wameokoka, maisha yao yanazidi kudidimia siku baada ya siku, na wanakumbwa na matatizo kwa sababu hawatafakari kuhusu wokovu. Nguvu ya msalaba inakukumbusha jinsi ya kuishi. Lakini
TABIA ZA WANA WA MUNGU
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Kutafuta Ufalme wa Mungu: Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Watu wa Mungu wana tabia ya kumtafuta Mungu kila wakati. Yesu alituonyesha katika sala ya “Baba Yetu” kwamba tunapaswa kutamani Ufalme wake uje na mapenzi yake yatimizwe hapa duniani. Waefeso 2:19 “Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” Tunapomwabudu Mungu na kuishi kwa kuzingatia mambo ya Ufalme wake, tunakuwa sehemu ya familia ya Mungu hata tukiwa hapa duniani. Kutafuta Ufalme wa Mungu maana
Somo: Mbaraka
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira A. Umiliki wa mwanadamu; Hatuwezi kuzungumzia Baraka pasipo kuelewa nafasi ya mwanadamu; Nafasi ya mtu itamuhakikishia mtu huyo nini anachoweza kumiliki. Mwanzo 1:26-27 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Nafasi ya mtu ni lazima iungamane na muumbaji, pasipo hilo kumiliki ni kitu kigumu kwa huyo mtu. B. Baraka ni nini? Ni neno lililotamkwa kwa uumbaji; Mungu alitamka neno kwa kiumbe kilichoumbwa na kwa kupitia hilo neno hicho
Mungu anataka tuweje?
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA MWENGE. Tunapozungumzia mwaka wa kumiliki, tunapaswa kugundua nani ndiye mmiliki. Biblia inasema, “Mbingu na nchi na vyote viijazavyo ni vya Bwana.” Ikiwa mmiliki ni Mungu, unapaswa kumjua YEYE na kuwa pamoja naye ili uweze kumiliki. Mwingine pia anayeweza kukupa umiliki ni ibilisi, lakini yeye si mmiliki wa kweli; badala yake, yeye ni mwizi. Ibilisi huiba na kumiliki vitu vya wizi. Ikiwa wewe ni wa ibilisi, unaweza kumiliki, lakini utakuwa mwizi. Msingi wa Jinsi Unavyopaswa Kuwa Watu wa Mungu Wanamiliki Kile Kilicho cha Mungu Ili kumiliki kile Mungu alichonacho, yapaswa uwe
Mwaka wa kumiliki
Hatuendi kuabudu kwa sababu sisi tunataka, la! Bali ni amri na ni agizo la Mungu, kwa maana hiyo ili wewe uabudu unapaswa kuwa mtii katika hiyo amri, ukiabudu unaonyesha kuwa unamuheshimu Mungu na kumtii na hiyo inakuwa ni namna yako ya kuwasiliana na YEYE aliyekuumba. Ibada ni namna ya kuwasiliana na yule ambaye ndiye chanzo chako, hivyo unapokwenda mbele za Mungu au kuabudu kuna vitu vingi unatakiwa kutafakari kabla haujaenda hapo, usiende kanisani kwa namna ulivyokuwa ukifanya, kwa sababu hauwezi kuabudu pasipo kuona muujiza wowote, Kwa namna unavyotii, namna yako ya kuabudu kwa Mungu ndivyo Mungu analeta watu kukuletea mahitaji
Kujitambua
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA Tunaenda ibadani na kufanya kila kinachohusu kanisa, hayo yote ni maandalizi ya kwenda kule tunakotamani kwenda. Yesu aliweka mfano na kusema; Ufalme wa Mungu unafananishwa na wanawali kumi, watano wenye busara na watano wapumbavu. Kanisa ni bibi harusi wa mwana kondoo, lengo la kuwa bibi harusi ni ili kuandaa watu waweze kujua kuwa kuna siku watatakiwa na Bwana wao. Katika mambo yote lazima ujue wewe uliyeokoka ni bibi harusi lakini katika ma bibi harusi wale kumi waliokuwa wanamsubiria Bwana Yesu, watano walikuwa ni wapumbavu na watano ni wenye busara. Je! Wewe uko wapi hapo?
Umiliki wa wana wa Mungu
KATIBU MKUU WA KANISA LA EFATHA PROFESSOR EMMANUEL CHAO Biblia inatukumbusha ya kwamba milki na urithi wote wa wana wa Mungu umefungwa ndani ya ufalme wa Mungu na hakuna chochote kinachoweza kupatikana nje ya huo ufalme. Unapozidi kuuelewa ufalme wa Mungu ndipo unakuja na mema yake yaliyofungwa nayo. Wakolosai 1:12 “Mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.” Urithi wetu umehifadhiwa ndani ya nuru na hauwezi kuchangamana na kitu chochote kilicho nje ya nuru. Waefeso 1:13-14” Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri
Somo: Mwaka wa kumiliki
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA – KANISA LA EFATHA SOMO: MWAKA WA KUMILIKI Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Hii ina maana kuwa chochote ufanyacho kwanza tafuta ufalme wa Mungu. Chochote unachotaka kutafuta au kugundua katika maisha yako tafuta kwanza ufalme wa Mungu, kama unataka kuanzisha jambo au unataka kufunga ndoa tafuta kwanza ufalme wa Mungu; kama unataka uwe na watoto, ujenge nyumba au kuishi Maisha mazuri tafuta kwanza ufalme wa Mungu ili hivyo utakavyovipata viweze kudumu katika maisha yako. Kwa maana chochote unachokitaka chanzo chake kipo katika kutafuta kwanza ufalme
Ziara ya Kitume katika kanisa la Efatha Bunju-Kinondoni
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Yohana 14 “Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Katika nyumba ya Baba yangu mna nafasi nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia makao. Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami; ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufikia ninakokwenda.” Tomaso akamuuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia? Yesu akawaambia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.” Huwezi kuiona mbingu pasipo kupita kwa
Linda sana moyo wako
NENO LA SIKU. Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha. Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Mafanikio hayatokani na fedha unazozalisha, wala vitu ulivyonavyo bali yanatokana na wewe ulivyo ndani yako, kama wewe ni mtu wa kushindwa ndani basi utashindwa na nje, lakini kama wewe ni mshindi ndani basi utashinda na nje. Mara zote ibilisi anapenda kukudhoofisha ndani ili uwe mpotezaji nje. Kama kuna kitu unapaswa kukilinda sana ni moyo wako, linda moyo wako maana humo ndimo zilipo Nguvu za mafanikio, Nguvu za ushindi wako zipo hapo. Ndani ya