Ni wakati wako wa kumiliki
NENO LA SIKU. Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha. Yohana 15:5 “ Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” Ukikaa katika mzabibu mwema ambaye ni Baba wa mbinguni Yeye atakupa kumiliki lakini ukikaa nje yake yaani katika mzabibu mwitu utazaa matunda ya dunia hii ambayo ni ya uharibibifu na kamwe hautaweza kumiliki milki zako alizokukusudia Baba yako wa Mbinguni. Biblia inasema “maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”, ukiona kuwa hauwezi kufanya chochote jua kuwa huenda umeokoka
Wazo la Mungu kwako
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA Wazo la Mungu kwetu lilikuwa ni hili; Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Hili ndilo wazo la Mungu kwa mwanadamu aliyemuumba. Ili tuweze kufikia makusudi ya kuishi kwetu hapa chini ya jua ni lazima tuelewe ilikuwaje mpaka sisi tukawa huku duniani. Katika mstari huu wa Biblia tunamuona Mungu akisema kwa habari zako na sio habari za mtu mwingine, siku ukielewa na kuliweka hili katika akili
Mshukuru Mungu kwa aliyokutendea
MTUME: ELIAKUNDA MWINGIRA Zaburi 34:1-4 “Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. Katika Bwana nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi. Mtukuzeni Bwana pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja. Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.” Mungu ni mwema kwetu siku zote, tumekuja mbele zake kumshukuru kwa sababu ya yale aliyotutendea, yale yaliyokuwa yametukandamiza yameondolewa, aibu yetu imefutwa na ndiyo maana tunakila sababu ya kumshukuru.
Tenda kwa ushujaa na uhodari ili upate kumiliki
NENO LA SIKU Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha Tarehe 17/10/2024 Yoshua 1:7 “Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.” Mafanikio hutokana na Juhudi katika Kazi. Mtu anapofuata maelekezo ya kufanya mambo ili yapate kutokea huingia katika hatua ya Ustawi, asipotenda kwa Ushujaa na Uhodari hawezi kustawi. Mungu alimwagiza Yoshua awe Hodari na Moyo wa Ushujaa ndipo ataweza kuwarithisha Wana wa Israeli Nchi yao ya Ahadi, hii inamaana kuwa kama asingekuwa hodari na mwenye
Ili ufikie ndoto yako kuna gharama unapaswa kulipa
NENO LA SIKU. Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha. Tarehe 16/10/2024. Mathayo 24:13 “Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.” Wabeba ndoto wana vizuizi vingi sana kutoka kwa wapinzani wao. Kabla ya kuona ndoto yako ikitimia kuna maumivu mengi utapitia ili hiyo ndoto ipate kutimia, kwa sababu NDOTO ni kama mtoto akitoka katika tumbo la mama yake. Usiwe na mashaka unapopitia maumivu ili kuifikia ndoto yako kwa sababu upo katika Njia sahihi. Kabla ya Yusufu kuifikia ndoto yake, alipita kunako maumivu mengi; alitaka kuuawa na ndugu zake, aliuzwa utumwani, alifungwa gerezani lakini aliishia kuwa mtu mkuu
Haki ya Mungu kwako
NENO LA SIKU. Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha. Tarehe 15/10/2024. Kila mtu huku duniani ana ratiba yake ambayo Mungu amempangia na ili uweze kuvipata vile Mungu alivyokuandalia ni lazima utembee katika kweli ya Mungu ili uweze kuipata haki yako. Mara zote usipende kumuomba Mungu akupe kufanana na mtu fulani? La, kwa sababu unapoomba Mungu akupe kuwa kama mtu fulani ina maana kuwa utapata ambacho sio chako. Mfano; haki ya Daudi ilikuwa afikie kuwa mfalme katika njia aliyopitia yeye; lakini haki ya Yusufu ilikuwa lazima akawe mtumwa katika nyumba ya Potifa, aende jela ndipo akawe mkuu
Urithi wako umeandaliwa mbele ya adui zako
NENO LA SIKU. Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha. Tarehe 14/10/2024. Zaburi 23:5 “Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika.” Mungu amekukusudia kumiliki ndani ya Mwaka huu wa Kumiliki, lakini meza yako imeandaliwa mbele ya adui zako, pale ambapo watesi wako wapo, sasa usipowashughulikia hao adui zako kamwe hautaweza kumiliki yale yaliyo ya kwako. Mungu akawaambia wana wa Israel amewapa nchi ya maziwa na asali, wapi? Hapo ambapo kuna majitu, walipofika mahali wakakata tamaa na kujiona wao ni kama panzi mbele ya hayo majitu hawakuweza kuirithi ile
Baraka kutoka kwa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Sasa ninaachilia baraka ambazo Mungu amenipa ili niweze kutembea nazo, zije juu yako kwa jina la Yesu Kristo. Neema ambayo Baba yangu wa Mbinguni amenipa, sasa nakuachia. Nakubariki ili asiwepo yeyote atakayesimama dhidi yako kwa jina la Yesu. Yeyote au chochote kitakachoinuka dhidi yako, Mungu atainuka dhidi yao. Kila kitu kitakachoinuka kukushambulia, Mungu atainuka kukishambulia. Mlango wowote uliokuwa umefungwa, sasa naufungua kwa jina la Yesu. Kila ukuta uliokuwa umejengwa mbele yako, nauangusha kwa jina la Yesu. Mamlaka yoyote inayokukandamiza na kukutendea vibaya, naiinamisha mbele yako kwa jina la Yesu. Ikiwa ni ugonjwa au laana zilizowekwa na mwanadamu au shetani, sasa
Baraka kutoka kwa Askofu Charles Kariuki.
Isaya 55:12 “Kwa maana mtatoka kwa furaha, na kuongozwa kwa amani; milima na vilima vitashangilia mbele yenu, na miti yote ya shamba itapiga makofi.” Haya ndiyo yatakayokutokea baada ya mkutano huu; ulikuja na huzuni lakini utaondoka na furaha, ulikuja mgonjwa lakini utaondoka ukiwa na afya. Milima na vilima vilivyokuwa vikwazo katika njia yako ya maendeleo vitakuongoza, vikikupeleka kuelekea urithi wako. Maadui na wapinzani wako ambao kwa miaka walikupinga na kukuzuia watajiunga na mchakato kukusaidia kufikia urithi wako. Wale waliokuchukia zamani wataanza kupiga makofi na kutangaza kuwa umebarikiwa na Mungu. Huu ni wakati wako wa kumiliki, na lazima umiliki urithi wako.
Maswali ya muhimu
Biblia ina maswali madogo na maswali makubwa. 2 Wafalme 7:3: “Sasa kulikuwa na wanaume wanne wenye ukoma mlangoni pa jiji; walijulizana, ‘Kwa nini tukakaa hapa mpaka tufe?’” Huu ulikuwa ni swali kubwa lililoulizwa na wale waliosumbuliwa, waliotengwa, na kukabiliana na hali ngumu. Wanaume hawa wanne waliuliza swali hili kwa pamoja. Swali hili lilitokea wapi? Na kwa nini walikuwa wanne, kila mmoja akiwa na swali lile lile? Swali hili lilitokea hapa: 2 Wafalme 7:1: “Elisha akasema, ‘Sikilizeni neno la Bwana; hivi ndivyo Bwana anavyosema: Wakati huu kesho, pishi moja ya unga wa ngano itauzwa kwa shekeli, na pishi mbili za shayiri