Bonde la Mifupa Mikavu
Mhubiri: Askofu Charles Kariuki – Kutoka Kenya MAANDIKO: Ezekieli 37:1-13 “Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.” UTANGULIZI Wapendwa katika Bwana. Leo tunajifunza kuhusu Bonde la Mifupa Mikavu, ujumbe wa kinabii unaotufundisha juu ya hali ya kanisa na nafasi ya waamini mbele za Mungu. Katika maono haya, Nabii Ezekieli anawekwa katikati ya bonde
Weka Nafsi Yako Mahali Sahihi
Mhubiri: Askofu Charles Kariuki – Kutoka Kenya Utangulizi: Tulio okoka ni kanisa la Yesu Kristo; kanisa ni wakala pekee aliyepewa mamlaka ya kuonyesha nguvu za Mungu duniani. Hivyo, hali ya kanisa inafikirwa sana na Mungu. Ikiwa Kanisa limetekwa, nguvu za Mungu haziwezi kudhihirishwa ulimwenguni. Mathayo 16:18: “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” Kanisa la Yesu Kristo lina nguvu kubwa na ni kiungo pekee cha kushinda nguvu za ulimwengu huu. Kujua nguvu za kanisa ni jambo moja, lakini kuwa na nguvu hizo ni jambo jingine. Ondoka Mahali Pasipo Sahihi
Kusimama Katika Nafasi Zetu
Mhubiri: Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira UTANGULIZI Wapendwa katika Bwana, leo tunajifunza kuhusu kusimama katika nafasi zetu tulizopewa na Mungu. Kila mwanadamu ameumbwa akiwa na nafasi yake maalum mbele za Mungu, lakini nafasi hizo zimegawanyika katika hatua tatu kuu: Nafasi kabla ya dhambi Nafasi baada ya dhambi Nafasi baada ya wokovu 1: NAFASI KABLA YA DHAMBI Kabala ya kuanguka kwa Adamu, mwanadamu aliishi katika bustani ya Edeni, akiwa katika utimilifu wa amri ya Mungu. Mungu aliwabariki Adamu na Hawa, na akawapa maagizo matatu makuu: Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa
Muhtasari Mahubiri Siku ya Pili
MUHTASARI WA SIKU YA 2 Mada: Kusimama katika Nafasi ya Mungu na Kutembea katika Baraka za Kimungu Siku ya 2 ilijumuisha mafundisho yenye nguvu kutoka kwa Mchungaji James Commey na Mchungaji Jens Garnfeldt kutoka Denmark, ikisisitiza nafasi yetu ya kiroho, mamlaka, na baraka tunazopokea katika Kristo. Lengo kuu lilikuwa kuelewa ni nani sisi katika Mungu, kutembea katika kusudi lake, na kusimama imara katika nafasi ya kiroho aliyotupa. 1. MUNGU ANA NAFASI NA KUSUDI KWAKO (Mchungaji James Commey) Akirejelea Waefeso 2:6-7, Joshua 1:6, na Esta 4:14, Mchungaji Commey aliwafundisha waumini kuwa Mungu amepanga nafasi ya kipekee kwa kila mtu katika maisha
Mungu Anabadilisha Hatima Yako
Mhubiri: Mchungaji James Commey (Kutoka Denmark) MAANDIKO: 2 Timotheo 3:16 Mwanzo 1:26 1 Mambo ya Nyakati 4:9 UTANGULIZI: Ahadi za Mungu ni Amina na Kweli. Mungu ametupa mtazamo wa kutatua matatizo yetu. Nguvu ya kubadilisha mazingira yako inategemea ufahamu wako juu ya Neno la Mungu. Kusudi la Neno la Mungu ni kuona, kurekebisha, na kutoa maagizo ili tufanye yaliyo sahihi. Biblia inasema katika 2 Timotheo 3:16: “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.” Kwa hiyo, Neno la Mungu si hadithi tu bali ni mwongozo
Nguvu ya Mbaraka wa Mungu
MHUBIRI: Mchungaji Jens Garnfeldt (Kutoka Denmark) MAANDIKO YA MSINGI: Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.” UTANGULIZI: Biblia inatufundisha kwamba Mungu ametubariki ndani ya Kristo Yesu kwa baraka zote za kiroho katika ulimwengu wa roho. Lakini mara nyingi, tumepunguza maana ya baraka tukidhani ni vitu vya kawaida kama kazi, gari, nyumba, au mke/mume. Hata hivyo, mbaraka wa Mungu ni kitu kikubwa zaidi ya mali au vitu tunavyomiliki. Mbaraka wa Mungu si kitu cha nje ni uwepo na uhalisia wa Mungu mwenyewe unaotiririka ndani ya
Somo: Utawala wa Mungu na Mamlaka ya Mtu
Mhubiri: Pastor Jens Garnfeldt (Kutoka Denmark) Maandiko: Mwanzo 1:26, Zaburi 8:4 6, Zaburi 115:16 UTANGULIZI: Biblia inasema katika Mwanzo 1:26, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Hapo tunaona kusudi kuu la Mungu kwa mwanadamu utawala. Mungu alimuumba mwanadamu si kwa bahati mbaya, bali kwa kusudi maalum la kutawala, kumiliki, na kuwakilisha mamlaka ya Mungu hapa duniani. MUNGU ALIMPA MWANADAMU UTAWALA Baada ya Mungu kuumba mbingu na nchi, alimuumba mwanadamu ili awe wakili wake
Simama Katika Nafasi Yako
Mchungaji James Commey (Kutoka Denmark) MAANDIKO YA MSINGI: Waefeso 2:6-7 Yoshua 1:6 Esta 4:14 UTANGULIZI: Mungu anatembea katika mataifa, na kila anapotembea, huwa anainua watu wake wale wanaoelewa wito wao, nafasi yao, na jukumu walilopewa na Mungu.Mungu anatafuta watu wanaomruhusu aishi ndani yao, wanaoelewa kusudi na hatima yao. Ndani ya moyo wa mtumishi wake, Mungu ameweka tamanio la kuwasaidia watu waelewe kile walichopewa na Mungu.Ni mapenzi ya Mungu kwamba mimi na wewe tusimame katika nafasi zetu ili tuweze kumiliki yale aliyotuandalia. 1. MUNGU ANA NAFASI KWA AJILI YAKO Mungu ana nafasi maalum kwa ajili yako katika: Maisha yako binafsi Huduma
Ujumbe wa Ufunguzi wa Kusanyiko Kuu 2025
Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira Ndani ya kusanyiko hili, alama itawekwa juu ya maisha yako, alama itakayobainisha kile ambacho utaanza kushuhudia kila siku kuanzia sasa. Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.” Kuna jambo linaenda kutokea kwako, nguvu ya Mungu itaanza kufanya kazi ndani yako kushughulika na kila kitu kinachokusumbua. Mambo makubwa yako karibu kutokea katika maisha yako, mambo ambayo hata hujayaomba. Nguvu ya Mungu ipo karibu kudhihirika katika maisha yako, kazini kwako, katika biashara yako, na katika kila eneo la maisha