Category: Mahubiri

Mahubiri Ka Kuvuka Mwaka Mpya – 31/12/2025

KANISA LA EFATHAMTUME NA NABII: JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA Jiangalie mwenyewe: je, kweli unastahili kuwa hapa leo? Je, wewe ni bora kuliko wale waliokufa? Inaniletea machozi kuona tunavuka mwaka mmoja kwenda mwingine tukiwa bado hai. Ninajiuliza kwa nini watoto wanazaliwa na kufa, ilhali wazazi walidhani wao ndiyo muda wao ulikuwa umefika.. wengine walikufa kwa risasi, wengine kwa kupewa sumu, wengine kwa ajali. Lakini mimi na wewe tuko hai. Mwambie Mungu asante kwa kuwa hai. Ni mambo mangapi umepitia, lakini leo bado upo hai mwambie Mungu asante.Mpendwa, yule aliyekuponya amekuponya, nawe hujui siku ya kuondoka kwako; acha kujivuna, ishi maisha ya shukrani

Read More

Timu Ya Mungu Dhidi Ya Timu Ya Ibilisi

Mhubiri: Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira Hapa duniani kuna Team mbili; team ya Bwana Yesu na ya ibilisi na kila team ina wachezaji 11; katika team ya MUNGU kuna wachezaji 11 nao ni:- Upendo; 1 Yohana 4:12 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.” Ukiwa na pendo la MUNGU ni rahisi kushinda katika kambi ya adui, adui anapokuja na ujangja wake pendo la Mungu litakukamilisha na kukupa namna ya kutoa hapo ili uwe salama. Kama unataka kucheza katika team ya Mungu hakikisha una upendo katika team yako. Kusamehe;

Read More

Kutafuta Shilingi Iliyopotea.

Mhubiri: Askofu Thabo Masenya Kutoka Afrika Ya Kusini Luka 15:8-10 “Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.” Baada ya huyu mwanamke kuipoteza shilingi yake alifanya mambo matatu; aliwasha taa, akafagia na kutafuta; na baada ya kuipata ile shilingi aliwaita marafiki zake na kusheherekea. Kutafuta kondoo waliopotea ni muhimu, lakini

Read More

Dawa Tatu Za Mungu: Imani, Tumaini Na Upendo

Mhubiri: Askofu Charles Kariuki – Kenya) Siri kuu ya ushindi wa kila Mkristo. Mungu ana dawa tatu za kiroho ambazo anatupatia kila mmoja wetu kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku. Dawa hizi si za hospitali, bali ni za uzima wa roho, nafsi na mwili. Mungu anataka uzibebe, uzihifadhi moyoni na uzitumia mara tatu kwa siku bila kuruka hata moja. Swali ni: Dawa hizo ni zipi? 1 Wakorintho 13:13 – “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.” UFAFANUZI WA DAWA TATU ZA MUNGU IMANI Imani ni uwezo wa kuamini kile ambacho

Read More

Yesu Chanzo Cha Amani Na Uponyaji Wetu

Mhubiri: Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira 1.    UTANGULIZI Waefeso 2:13-18 “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani…” Leo utaenda kuona amani ya moyo wako. Yote yaliyokukatisha tamaa lazima yawe na kikomo. Mungu ni Baba yetu, naye ametupa nafasi ya kumkaribia. Yeye ni kimbilio

Read More

Umoja Katika Kanisa

MHUBIRI: Askofu Thabo Masema, Afrika Kusini Lazima uelewe kwamba ili huduma iwe na ufanisi, ni lazima kuwe na umoja kufanya kazi pamoja katika huduma. Ili kanisa liweze kukua na kuwa na nguvu, ni lazima liwe na umoja, kwa maana huko ndiko nguvu yake ilipo. Kuna watu ambao wameitwa kuhudumu kwa ubora mkubwa ndani ya kanisa, lakini hawatafuti kujulikana. Lakini wapo wengine, wakifanya jambo lolote kanisani, wanataka kila mtu ajue. Kwa mfano, mtu akiombea ibada siku ya Jumamosi na Jumapili kukawa na upako mkubwa, anaweza kujisifu akisema, “Ni kwa sababu nililala nikiomba jana usiku.” Hata hivyo, Ufalme wa Mungu unajengwa pale

Read More

Mtazamo Wako Ndio Utakaoamua Hatma Yako

Mhubiri: Askofu Charles Kariuki Kenya UTANGULIZI Inawezekana kuna mambo yaliyotokea kwa ajili yako ambayo si mazuri katika siku hii, lakini mimi kama balozi wa mbinguni ninakutangazia kwamba ijumaa hii utaifurahia. Ijumaa yako imebarikiwa utaifurahia na utamshukuru Mungu kwa ajili ya siku hii. UKIRI “Baba katika jina la Yesu, ninakubaliana na Neno lako kwamba ijumaa yangu imejawa na furaha, imejawa na wema, na si vinginevyo. Kwa jina la Yesu, naibariki ijumaa yangu na ninaianza kwa tumaini kubwa, nami najua tumaini langu halitazimishwa.” MTAZAMO Ikiwa umeshawekwa katika nafasi yako katika Ufalme wa Mungu na umeitambua nafasi hiyo, kinachofuata ni kudumu katika hiyo

Read More

Utambulisho Wa Mwana Wa Mungu

Mhubiri: Askofu Thabo Masenya Kutoka Afrika Ya Kusini Neno: Kumbukumbu la Torati 28:1-14 UTANGULIZI Baraka si neno tu tunalotamka ni hali ya kiroho. Unaposema “umebarikiwa,” unamaanisha umebeba roho katika maisha yako inayoletea mambo mazuri. Unaposema “umelaaniwa,” unamaanisha umewezeshwa kushindwa na chochote uchokifanya. Leo, Mungu anatutaka tujue nafasi yetu halisi kama wana wake walobarikiwa. MAANA YA KUWA MBARAKA Baraka Ni Nini Baraka ni roho inayokuja kuishi ndani yako Baraka ni uwezo wa kufanikiwa katika kila kitu Baraka ni uhakika wa mafanikio yaliyoandaliwa na Mungu Ulinzi wa Baraka “Yule aliyembariki hakuna anayeweza kumlaani” (Numeri 23:20) Ibilisi hawezi kukuchezea ukijua nafasi yako Wewe

Read More

Umuhimu wa Ushirikiano Katika Kanisa la Kristo

Mhubiri: Askofu Charles Kariuki (Kenya) Neno: 1 Wakorintho 12:5-7 UTANGULIZI Kila mmoja wetu anahitaji kuelewa nafasi yake na kazi yake ndani ya kanisa. Ukilijua hili, litabadilisha maisha yako. Ukihaulielewa kanisa, ni rahisi kupoteza wajibu wako na kujikuta hatarini. Hakuna yeyote ndani ya kanisa ambaye hana kazi – na hakuna anayeweza kufanikiwa akiwa peke yake. HATARI YA KUFANYA KAZI PEKE YAKO Mfano wa Eliya – Nabii Mwenye Nguvu Lakini Peke Yake Eliya alikuwa nabii mwenye nguvu sana: Aliizuia mvua isinyeshe kwa miaka mitatu Alilishwa na kunguru kwa mwaka mzima Aliishi kwa mjane Aliwaua manabii 450 wa Baal Lakini kosa lake kubwa:

Read More

Balozi wa Mbinguni: Kuelewa Utambulisho Wako na Mamlaka Yako katika Kristo

Mhubiri: Mchungaji Thabo Masenya (Afrika Kusini) Neno: 2 Wakorintho 5:19-20 UTANGULIZI Kila mmoja wetu amesikia watu wakisema “unahitaji kujua wewe ni nani.” Lakini katika ulimwengu wa Kikristo, hii siyo kauli tu; ni ukweli wa kiimani. Ukijua wewe ni nani katika Kristo, utaweza kupata vitu vingi sana. Lakini usipojua wewe ni nani, usipoijua nafasi yako, upepo unaweza kukusukuma mbali na baraka zako. UPATANISHO NA UTAMBULISHO MPYA Mungu Ameupatanisha Ulimwengu Fungu letu la msingi linatuambia: “Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao” (2 Wakorintho 5:19). Yesu alikuja ili aondoe dhambi na atupatanishe na Mungu. Wewe ni

Read More