Kisha akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, yaani, Funguka.
Marko 7:34
Uponyaji na Ukombozi kwa Damu ya Yesu
Kanisa la Efatha, lililojulikana awali kama Huduma ya Efatha, lenye msingi wa kitume na kinabii, lilianzishwa mwaka 1996 na kupewa usajili rasmi nchini Tanzania mwaka 1997. Mwaka 2021, lilipata usajili wa kanisa.
Kanisa hili lilianzishwa na Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ambaye ndiye Mtume Mkuu wa kanisa hili.
Mafundisho yanayotolewa wakati wa ibada za Efatha ni ya kitume na kinabii, zikiambatana na udhihirisho wa nguvu za Mungu katika kuokoa, kuwaponya na kuwaweka huru wale waliokuwa wamefungwa na nguvu za giza. Kwa sasa kanisa lina makanisa Tanzania bara na visiwani na nje ya nchi.
MTUME NANABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Dhamira
Kuhubiri Injili ili kuwaleta watu wote kwa Yesu Kristo kwa kutoa huduma bora na yenye usawa katika mafundisho, uponyaji, na utwisho wa uumbaji; pamoja na kuboresha uwekezaji wa kiuchumi wa Kanisa ili kuwezesha dhamira kanisa.
Maono
Kuhubiri Injili ya Yesu Kristo kwa ulimwengu ili watu wapate wokovu, uponyaji, na utwisho kupitia Jina na Damu ya Yesu Kristo.