Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha
Matendo ya Mitume 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”
Kipawa hutafsiriwa kama kitu kinachotolewa na kukubaliwa bila sharti ikimaanisha tendo la kupokea. Kipawa hakijakamilika mpaka pale mtu apokee kile kilichotolewa bure kwake.
Swala la kipawa ni ile hali yako ya kupokea. Tutajua umepokea kipawa kwa kuona udhihirisho; kuna hali fulani, tabia na jambo litachipuka ndani yako. Watu wataanza kuona unapenda kuomba, kusoma Biblia, kwenda Kanisani na kwa njia hiyo unaruhusu Roho Mtakatifu azidi kuchipuka ndani yako.
Mwana wa Mungu kama una amini, fanya bidi ili umpokee Roho Mtakatifu.