Kutafuta Shilingi Iliyopotea.

Mhubiri: Askofu Thabo Masenya Kutoka Afrika Ya Kusini

Luka 15:8-10 “Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”

Baada ya huyu mwanamke kuipoteza shilingi yake alifanya mambo matatu; aliwasha taa, akafagia na kutafuta; na baada ya kuipata ile shilingi aliwaita marafiki zake na kusheherekea.

Kutafuta kondoo waliopotea ni muhimu, lakini pia kumtafuta shilingi pia ni muhimu sana, Biblia inaasema kuwa sisi ni wana wa Mungu na utajiri ni haki yetu lakini ikiwa kama sisi ni wana wa Mungu na utajiri hauonekani kwetu inamaana kuwa umeibiwa; je shilingi ya kanisa iko wapi? Maana yake ni kuwa kanisa limepoteza shilingi, ni wajibu wa kanisa Kwenda kutafuta shilingi iliyopotea, kuna mambo mengine hatuwezi kufanikisha sisi kama kanisa mpaka tumepata hiyo shilingi; kwa maana uchumi una umuhimu mkubwa sana katika kuipeleka injili.

Biblia inasema fedha ni jawabu la kila kitu, ni kweli kabisa kuwa nguvu ni nzuri lakini kuna mabo mengine hauwezi kufanya kama hauna fedha. Biblia inasema “masikini akitoa mashauri hata hasikilizwi, lakini mjinga ambaye ana fedha akitoa ushauri utamsikiliza tu” huku duniani kuna watu wengi ni wajinga lakini wanafedha wanasikilizwa na kuna watu wengine wana hekima sana lakini ni masikini hata wakisema hawawezi kusikilizwa.

Kuna wengine wamebeba majibu ya familia zao lakini familia zao haziwasikilizi kwa sababu ya kiwango chako cha uchumi walichonacho. Mwana wa Mungu hakikisha unaitafuta shilingi yako iliyopotea kwa maana hapo ndipo ilipo thamani yako.

Ukiwa na mafundisho mazuri kuhusu uchumi na maarifa ya namna ya kutunza fedha ndipo unakuwa katika safari ya kutafuta shilingi yako.

Kuna mvua kubwa ya kifedha inayokuja kwako; Kanisa siyo jengo bali ni watu hivyo kuna mvua kubwa ya kiuchumi inakuja kwako.

Kile kilichokuwa kigumu kwako ndicho kitakuwa chepesi sana. Ninaachilia utajiri kwa watu wa kwako katika jina la Yesu. Kile ambacho ibilisi anawazuilia watu Mungu ataleta mpenyo wa ukuu katika Maisha yako.

Kuna watu wanashindwa kuingia katika utajiri wao kwa sababu ya vifungo vya kifamilia, leo vifungo vyovyote vya kifamilia ambavyo vimekushikilia vinaenda kukuachilia. Kuna roho zinachukua fedha yako na kukukataza wewe ushindwe kufikia utajiri wako; utajuaje hilo? Kwa ishara ya ndoto, ikiwa unaota kuwa upo shule ya msingi au sekondari ilihali ulisha maliza muda mrefu sana, hii ni ishara kuwa ibilisi amekurejesha nyuma wewe hausongi mbele, Wengine wanaota kuwa wapo kijijini ingawa hawajawahi hata kuishi kijijni, hii ni kwa sababu kuna roho inakurejesha nyuma, ukiwa na ndoto za aina hizi, inamaana kuwa ibilisi anataka kukurejesha nyuma.

OMBI:

1. Mwambie Mungu akuweke huru kutoka katika roho ya kurudishwa nyuma, Maisha yako lazima yasonge mbele na siyo kukurudisha nyuma kwa jina la Yesu.

Kuna aina ya watu wanapotafuta utajiri wakiw akatika mchakato huo watu wanapambana kupata mpenyo wa utajiri kwa sababu ya aina fulakini ya Maisha, ibilisi anapambana na huo mpenyo wako lakini Mungu NAKUWEKA huru leo haijalishi umefungwa kwa namna gani leo Mungua kakuweke huru kw ajina la Yesu.

OMBI:

1. Inaweza kuwa kuna nzi anakufuatilia mara zote, ukiona nzi maana yake kuna kitu kimeoza kwako wewe unatakiwa uwe huri katika maisa yako. Viunja roho ya uharibifu katika maish ayako ,chochote unachokifanya hakitaharibiwa tena wala hakita oza kwa jina la Yesu, Maisha yako ya kifedha hayataharibiwa wala hayataoza.

2. Mara zote unapambana hata kama unanunua nguo mpya lakini ikawa namatobo, hii ni ishara kuwa kuna kitu kinaiba fedha yako.