Anaitwa Anjela Anthony, anamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyomtendea, mwaka 2016 Anjela alipata neema ya kununua kiwanja na kujenga nyumba yenye vyumba vinne(4) na baada ya hapo alipokuwa kanisani mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii alimpa zawadi ya dollar 100 na kumwambia akajenge nyumba nyingine.
Pia Anjela anamshukuru Mungu tena, alivyoenda kusanyiko mtumishi wa Mungu Stefan alikuwa akihubiri na kusisitiza kuwa kama kuna kitu unasikia ndani unataka ukifanye, nenda kakifanye na kitakuwa, na Anjela alikuwa anasikia ndani msisitizo wa kununua kiwanja kingine na ndipo akapokea lile neno na kulitendea kazi. Kusanyiko lilipoisha ndugu yake alimpigia simu na kumwambia amepata kiwanja mahali, Anjela alimwambia Bosi wake kuwa amepata kiwanja mahali na anataka akinunue, na ndipo bosi wake alimwambia kuwa alitamani kumnunulia kiwanja. Anamshukuru Mungu sana wiki mbili(2) hazikuisha Bosi wake alimpa hela yote ya kile kiwanja na akaenda kununua hicho kiwanja, sifa na heshima zimrudie Mungu wa Efatha.