Ibada ya Jumapili 14/09/2025

UJUMBE: NJOONI KWA KRISTO MPATE PUMZIKO

Mchungaji Aimana Dominick, Kanisa la Efatha Mwenge Dar es Salaam

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”

Pumziko la kiungu si sawa na pumziko la kidunia. Pumziko la Mungu lipo kila siku, kila wakati, na kila mahali. Ni tofauti na pumziko la kidunia ambalo hudumu kwa muda mfupi tu. Pumziko la kiungu hubeba furaha na amani ya Mungu.

Kwa hiyo, lolote linalokusumbua au kukulemea leo, hakikisha unaliweka mikononi mwa Yesu Kristo, kwa maana anakualika kulingana na Neno lake. Hukumu na kukata tamaa havitokani na Mungu. Leo hii, baada ya kuweka chini mizigo yako au mambo yanayokusumbua, utapokea faraja na tumaini jipya. Baada ya ibada ya leo, hakikisha unabaki katika kweli yake kweli itakayokuwezesha kuishi katika furaha yake katika majira haya mapya.

MAOMBI

Ee Baba wa Mbinguni, nakushukuru kwa uongozi Wako katika maisha yangu.

Ninaweka imani yangu yote katika mipango Yako iliyo kamili juu ya maisha yangu.