Mhubiri: Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira
Hapa duniani kuna Team mbili; team ya Bwana Yesu na ya ibilisi na kila team ina wachezaji 11; katika team ya MUNGU kuna wachezaji 11 nao ni:-
- Upendo; 1 Yohana 4:12 “Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.” Ukiwa na pendo la MUNGU ni rahisi kushinda katika kambi ya adui, adui anapokuja na ujangja wake pendo la Mungu litakukamilisha na kukupa namna ya kutoa hapo ili uwe salama.
- Kama unataka kucheza katika team ya Mungu hakikisha una upendo katika team yako.
- Kusamehe; Marko 11:25 “Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.” Mahali popote penye Pendo Mungu huwepo mahali hapo, hivyo kwa kupitia toba unamualika Mungu na Mungu anapokuja analeta Pendo ambalo litakufanya ufanye mambo makubwa.
- Ukiwa na msamaha ni rahisi kuwa chini ya Mungu na kuwa juu ya ibilisi. Kwa sababu ni kwa njia ya msamaha tu ndipo unaweza Kwenda mbele za Mungu kwa ujasiri.
- Haki: huyu ni mchezaji namba tano katika ufalme wa Mungu; yeye anazuia adui yeyote mbaye anakuja kukaribia kwenye kufunga goli. Haki ni ya muhimu sana kama unataka kuwa mtumishi mwaminifu mbele za Mungu na kama unataka kutembea na kufanya kazi za Mungu.
- Ibilisi anaiogopa sana hii nafasi kwa maana haki ni utakatifu na yeye hawezi, ibilisi hawezi kucheza na wenye haki wa Mungu.
Mathayo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” Unaweza kulibeba pendo lakini je! Utalitunzaje hilo pendo? Hakikisha wewe ni mwenye haki wa Mungu.
- Imani; Imani kwa Mungu wako; Waebrania 11:6-7 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.”
Hapa duniani kuna Team mbili; team ya Bwana Yesu na ya ibilisi na kila team ina wachezaji 11; katika team ya MUNGU kuna wachezaji 11 nao ni:-
- Ujasiri; kwa nini unahitaji ujasiri? Ni kwa sababu ukiwa katika eneo la ulizi ni lazima uwe na ujasiri kwa maana ibilisi haogopi hivyo hakikisha anapokuja kwako ili kukushinda anakuta wewe ukiwa na ujasiri, akija kukutishia uwe na ujasiri katika Imani yako kwa maana kama hauna ujasiri utakimbia.
- Matendo 4:13 “Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.” Kama haubebi ujasiri basi kufanya miujiza si kitu rahisi, ibilisi atakuja na kukutishia nawe kamwe hautaweza kufanikisha kile unachokitaka.
- Unahitaji ujasiri kwa Mungu wako, unachohitaji sema kile unachokiamini na kile neno linachosema bila kujiangalia ulivyo sasa, hiki ndicho tunakiita ujasiri, ukisema hivyo unaifanya Mbingu ifanya kile unachokisema, sema bila kuogopa, bila mashaka zungumza ukijua kuwa kuna kitu kitatokea kwa sababu Imani huona kitu kinachokuja kabla hakijaja katika damu na nyama na hutoa kitu katika ulimwengu wa roho na kukileta katika ulimwengu wa damu na nyama, ndio hauna fedha wala haua nyumba, lakini sema Imani yako, tamka kile unachokitaka kwa ujasiri nacho kitakuwa chako.
- Matendo 4:13 “Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.”
- Bidii katika Bwana; hii ni namba nane katika team, bila bidii kamwe hauwezi kustawi, ukimuona mtu aliyestawi jua kuwa halali anatumia bidii, anafanya kazi usiku na mchana.
- Bidii siyo jambo la kiroho bali ni jambola kutumia akili, acha akili yako ijue ni kitu gani cha kufanya na namna ya kufanya. Kama akili yako ni dhaifu kamwe hautakaa uamrishe chochote kwa ajili ya ufalme wa Mungu, kwa maana mwili mara zote ni mdhaifu.
- Waebrania 4:11 “Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.” bidii inakufanya usianguke.
- Mithali 22:29 “Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo.” mtu yeyote mwenye bidii anasimama mbele za wakuu.
- Mtu mwenye bidii mara zote anastawi, Mungu akafungue akili yako ili ujue namna ya kutafuta fedha. Ukiwa masikini ujasiri unatoweka.
- Bidii ni ufunguo wa wewe kustawi, ukifundishwa na ukafanyia kazi kile ulichokifundishwa basi utafanikiwa, lakini ukikaa kamwe havitakuja kama muujiza, ili uweze kukaa katika nafasi yako unahitaji bidii.
- Kumbu kumbu 28:1 “Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;”
Hapa duniani kuna Team mbili; team ya Bwana Yesu na ya ibilisi na kila team ina wachezaji 11; katika team ya MUNGU kuna wachezaji 11 nao ni:-
- Sadaka zako kwa Mungu: Warumu 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Unahitaji ustawi ndio ili hilo jambo litokee kwako unahitaji sadaka.
- Huruma: Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.” Hauwezi kumwabudu Mungu ikiwa hauwezi kujitoa, tunamwabudu Mungu na kukamilisha sadaka ya dhabifu bila sadaka hiyo ibada yako inakuwa haina mana, Waebrahia 5:7 “yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;”
Huruma za Mungu; katika team ya Mungu hii huwa ni namba mbili katika ufalme wa Mungu, hakikisha haumuumizi mtu yeyote na kama ikitokea umemuumiza muombe msamaha.
- Maombi: kama ni katika team ya mpira huyu ni mchezaji namba 10 awapo uwanjani, ishi maisha ya maombi ukitembea omba kwa maana maombo ni ufunguo wa kile unachokihitaji, maombi ni ya muhimu sana. Waebrania 5:7 “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;”
Kupitia maombi unaenda kumiliki, familia yako, ndoa yako, unarejesha uchumi wako, unarejesha umiliki wako.
- Utii; huyu ni mchezaji namba 3 katika ufalme wa Mungu, Matendo ya Mitume 6:7 “Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.”
- Uvumilivu; huyu ni golikipa, awapo uwanjani anavumilia kila aina ya shuti linalopigwa kwake. Uvumilivu ni wa muhimu sana kwa mtu kama unataka kuushinda ulimwengu; Yesu asingeweza kuushinda ulimwengu kama asingekuwa mvumilivu.
Kama Mungu amekuridhia kuiona siku ya leo hayo unayopitia yanapita, vumilia mabaya, ili uweze kuwa mtu mkuu, Ibrahim alivumilia akawababa wa mataifa.
- Uvumilivu. Bila uvumikivunkatika jambo lolote hauwezi kufanikisha katika eneo lolote. Uvumilivu katika kazi, ndoa, utumishi nk ni muhimu sana kwa kila mmoja. Musa alivumilia akavusha watu, ibrahimu alivumilia ndo maana akawa bana wa mataifa mengi. Mtu mkubwa ana changamoto nyingi ila anapaswa kuvulilia kwa kuwa anae Yesu ndani yake na yatapita kwa kuwa wewe ni mtu wa imani na unatii neno lake.
MAOMBI:
- Baba leo nimeelewa mwamba pasipo pendo siwezi Kwenda mbali wala kushinda na mimi nataka kushinda naomba pendo likae ndani yangu.
- Bwana Yesu nipe kujitoa kwa ajili yako nisijionee huruma.
- Bwana Yesu Imani yangu unapotaka kuyumba naomba uirejeshe katika mstari, naomba Imani yangu isiyumbishwe kwa maneno wala mazingira. Eeh! Bwana umba kiu na njaa ya kusoma Neno lako ili Imani yangu iwe thabiti.
- Eeh! Mungu nipe nguvu ili bidii ikajengeke ndani yangu.
- Haki; baba leo najua na ninatambua kuwa wewe ni mwenyehaki, mimi nimwanao kuanzia sasa naomba unipe kuishi katika viwango vya Imani.
- Eeh! Mungu nipe ujasiri katika maish ayangu, nisiishi kwa mashaka bali unipe ujasiri.
- Bwana nipe kuwa mtii.
Miezi yako mitatu utashangaa watu ambao hawajawahi kukuletea hata chumvi wanakuletea sukari.
Kanisa kaa haliombni hilo kanisa limekufa, huhitaji watu million waweze kubadilisha mji bali wewe unaweza kubadilisha.
Umasikini unasababishwa na kutokuomba kwa bidi, ukiomba kwa bidi Maisha yako yanabadilika n ahata … kama kuna vitra kati yako na mume wako hali inabadilika,
Maombi ni ufunguo.