Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
Ndani ya kusanyiko hili, alama itawekwa juu ya maisha yako, alama itakayobainisha kile ambacho utaanza kushuhudia kila siku kuanzia sasa.
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.”
Kuna jambo linaenda kutokea kwako, nguvu ya Mungu itaanza kufanya kazi ndani yako kushughulika na kila kitu kinachokusumbua. Mambo makubwa yako karibu kutokea katika maisha yako, mambo ambayo hata hujayaomba.
Nguvu ya Mungu ipo karibu kudhihirika katika maisha yako, kazini kwako, katika biashara yako, na katika kila eneo la maisha yako ikileta mabadiliko. Baada ya kusanyiko hili, miujiza itaanza kutokea kwako ambayo hata hujaiomba.
Kwa wale ambao biashara zao zimekwama, zitafufuka na kustawi kama uyoga. Kwa wale ambao furaha yao ilipotea, furaha ya Bwana inarudi kwako. Kwa wale ambao wamepoteza uwezo wa kuisikia sauti ya Mungu au kuona maono yake, mtarejeshewa. Mungu ataanza kuzungumza nawe kwa namna utakayoielewa wazi. Kuanzia leo, mabadiliko yataanza kutokea katika maisha yako hata ukiwa umelala. Kuna jambo la kiungu linaenda kukutokea usiku wa leo. Wengine wataona maajabu kabla hawajafumbua macho yao.
Baada ya kusanyiko hili, hakuna atakayeondoka bila kupokea jibu la maombi yake.