Umuhimu wa Ushirikiano Katika Kanisa la Kristo

Mhubiri: Askofu Charles Kariuki (Kenya)

Neno: 1 Wakorintho 12:5-7

UTANGULIZI

Kila mmoja wetu anahitaji kuelewa nafasi yake na kazi yake ndani ya kanisa. Ukilijua hili, litabadilisha maisha yako. Ukihaulielewa kanisa, ni rahisi kupoteza wajibu wako na kujikuta hatarini. Hakuna yeyote ndani ya kanisa ambaye hana kazi – na hakuna anayeweza kufanikiwa akiwa peke yake.

  1. HATARI YA KUFANYA KAZI PEKE YAKO

Mfano wa Eliya – Nabii Mwenye Nguvu Lakini Peke Yake

Eliya alikuwa nabii mwenye nguvu sana:

  • Aliizuia mvua isinyeshe kwa miaka mitatu
  • Alilishwa na kunguru kwa mwaka mzima
  • Aliishi kwa mjane
  • Aliwaua manabii 450 wa Baal

Lakini kosa lake kubwa: Alipenda kufanya kazi peke yake!

  • Hakuwatafuta wengine 7,000 waliosalia ambao hawakukubali kumwabudu Baal
  • Alikimbia kwa Yezebeli peke yake
  • Alimuomba Mungu amuue badala ya kumkabili kwa nguvu za pamoja
  • Hakumaliza kazi yake – akachukuliwa na Mungu mapema

Somo Kwetu Leo

Tungekuwa sisi (wengi) tungemkabili Yezebeli kwa nguvu ya umoja. Lakini Eliya alikimbia kwa sababu hakuwa na mtu wa kumtia moyo. Siku zako za usoni zinategemea ushirika wako na wengine kanisani.

  1. KANISA NI MWILI WA KRISTO

Tofauti za Huduma, Mmoja Bwana

1 Wakorintho 12:5-7 inatukumbusha:

  • “Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule”
  • “Kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana”

Kila Kiungo Kina Thamani

  • Mwili si kiungo kimoja – ni viungo vingi
  • Viungo vingine vimefichwa na havipati heshima
  • Lakini kila kiungo kina kazi yake muhimu
  • Usitake kuwa kama kiungo kinachoonekana – tosheka na mahali ulipowekwa

Umuhimu wa Kila Mshirika

  • Mwili haiitwi mwili ikiwa huna viungo vingi
  • Kanisa haliitwi kanisa ikiwa huna washirika wengi
  • Kila mshirika amepewa mchango wa kufanya
  • Hakuna kanisa la mshirika mmoja au wawili
  1. FANYA KAZI YAKO KWA BIDII

Mwili Unakua Kwa Kila Kiungo

Waefeso 4:15-16 inasema:

  • “Mwili wote ukiungamanishwa… kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja”
  • Mwili unakua pale kila kiungo kinapofanya kazi
  • Kiungo kisichofanya kazi kinakuwa kidhaifu

Fanya Kazi Yako Bila Kuangalia Wengine

  • Kama wewe ni wa kufagia, fagia kwa bidii
  • Kama wewe ni wa kupanga viti panga kwa bidii
  • Kama wewe ni mtoaji, toa kwa bidii
  • Usimtazame mwenzako akifanya kazi yako

 Kanisa ni Kama Timu ya Mpira

  • Kila mchezaji anajua nafasi yake uwanjani
  • Lengo ni kuhakikisha timu haifungwi
  • Yesu kama kichwa anafurahi pale viungo vyote vinapofanya kazi

HITIMISHO

Kuna miujiza mingine haipatikani kwa kuombewa tu, inahitaji kufanya kazi! Kila mmoja wetu ajiunge katika kazi ya Bwana. Fanya kazi yako kwa bidii, iwe unaonekana au hauonekani. Jua kuwa wewe ni muhimu sana kwa ukuaji wa kanisa.

WITO

Leo nakuamuru: Tosheka na mahali ulipowekwa na Mungu! Acha kuangalia wengine. Anza kufanya kazi yako kwa bidii kwa faida ya mwili mzima.

MAOMBI

“Baba, tunaomba uondoe kizuizi chochote kinachowafanya watu wako wasifanye kazi yako. Kwa jina la Yesu, waweze kujituma kwa bidii katika nafasi zao. Ameni.”