Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mambo ya msingi na yakuzingatia kwa watu waliookoka

Watch Now

Download

Mambo ya msingi na yakuzingatia kwa watu waliookoka

MTUME BETSON KIKOTI – KANISA LA EFATHA MWENGE.
1 Wathesalonike 5:11-15 “Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.………”
Biblia inasema “Farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake,” faraja haiwezi kutoka kwa mtu ambaye hana pendo. Kwa kawaida kanisa halina lugha nyingine isipokuwa kufarijiana sisi kwa sisi tulio watakatifu tuendao mbinguni, kwa sababu kanisa la Yesu Kristo lina njia ya kutembea haliendi tu hivi hivi na hiyo njia ni Yesu Kristo.
Kuna aina tatu za familia:
1. Familia ya kuzaliwa; hapa ndipo kila mmoja wetu ametokea, tumetoka katika mazingira na familia tofauti tofauti, kupitia familia zetu tumejifunza mambo mengi sana ya mila na desturi ambayo yametupa hofu za kila aina; familia zimetushika kwa mambo mengi sana ambayo kila mtu anatembea nayo na mtu huyo anaweza kuona kuwa ni kawaida, lakini kupitia hayo yanatesa maisha yao.
2. Familia ya kidini; hii inatokana na watu kuabudu kila kinachoonekana, wengine wanaabudu maji, ng’ombe na kila kitu ambacho wanahisi wao ni Mungu kwao.
3. Familia ya waliookoka; Hii familia inaongozwa na mtu mmoja na mwenye maelekezo yote naye ni Yesu Kristo. Huyu anajumlisha watu wote kutoka katika hizo familia ambao watamkimbilia yeye naye atawafanya kuwa kitu kimoja na kumwabudu Mungu aliyeumba Mbingu na nchi (Mungu wa mbinguni).
Sisi kama wana wa Mungu tulioamua kumkimbilia Yesu (kuokoka) tunapaswa kufarijiana sisi kwa sisi na Yesu anapoona tunakumbatiana na kufarijiana ndipo Yeye mateso kwake yanapungua kwa maana Biblia inasema “tukifanya tofauti tunamsulubisha Yesu mara ya pili”
Familia ya waliookoka wanatakiwa kuwa na tabia ya upendo na sio kuchukiana sisi kwa sisi.
Hauwezi kuishi huku duniani bila changamoto, changamoto ikija kwako inakusaidia wewe kusonga mbele, na sio kukufanya ushindwe kuendelea na wokovu wako.
1 Wathethalonike 5:12-13 “ Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi. ”
1 Timotheo 5:17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.” Hapa hana maana ya wazee ki umri, la! Bali wale ambao wapo mbele yetu kama viongozi wanaotufundisha na kutuhubiria Neno la Mungu.
Wewe kama mshirika ukiona mtumishi anayekuongoza anafanya tofauti una wajibu wa kumuombea na sio kumhukumu, kwa wewe kufanya hivyo Mbingu inafurahi na kukujibu haja ya moyo wako na ndipo unaanza kuona Mungu akimbadilisha huyo kiongozi wako hatua kwa hatua.
Mambo ya msingi na yakuzingatia kwa watu waliookoka.
1. Tunapaswa kuwaonya watu ambao hawajakaa katika utaratibu
2. Kuwatia moyo walio dhaifu, tunapaswa kuwatia moyo ili waweze kuwa majasiri na ili waweze kuwa imara kwa utukufu wa Mungu.
3. Tuwatie nguvu wanyonge, wanyonge ni wale wasiojiamini wenye kukataliwa, wenye kudhulumiwa na wahitaji.
4. Kuvumiliana na watu wote, wewe uliyeokoka uwe mponyaji kwa watu wenye tabia ambayo haimpendezi Mungu.
5. Tusilipe mabaya kwa mabaya, Warumi 12:19-21 “Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.”