Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Utendaji wa Neema ya Mungu

Watch Now

Download

Utendaji wa Neema ya Mungu

KIONGOZI WA KIROHO WA KANISA LA EFATHA – MTUME NOEL KAPINGA
Je! Unaishi kwa Neema ya Mungu au kwa nguvu zako mwenyewe?
• Neema ya Mungu ni nini? Ni sehemu muhimu ya tabia ya Mungu, kama unataka kuona tabia ya Mungu utaiona kwa haraka kupitia Neema. Palipo na Neema pana tabia ya Mungu.
• Neema ya Mungu ni kibali toka Mungu kwa mtu ambaye hakustahili, sio kwa nguvu zako bali ni kwa kibali cha Mungu umesamehewa na kuinuliwa.
• Neema ya Mungu ni nguvu au msaada toka juu. Neema ya Mungu ni msaada wake kwako, unaishi sio kwa nguvu zako bali ni kwa msaada wake. Hauwezi kupigana na mtu ambaye ana kibali cha Mungu.
Unapokutana na changamoto omba Neema ya Mungu na Neema ya Mungu inapokujia utapata msaada toka juu, usitegemee ufahamu wako mwenyewe bali tegemea Neema ya Mungu.
Usipoteze muda kumpa changamoto mtu yeyote anayetembea na Neema ya Mungu kwa maana kamwe hautafanikiwa na ibilisi ataishia kukucheka.
AINA ZA NEEMA:
1. Neema ya Wokovu, Neema hii unaipokea pale unapopokea Injili na ukamwamini Yesu Kristo, hii ndiyo inaitwa Neema ya Wokovu. Kama haujaokoka Neema hii ikakukute kwa Jina la Yesu.
Waefeso 2:8 “ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;” Tumeokolewa kwa Neema na sio kwa nguvu zetu, ni kwa Neema ya Mungu sisi sote tumeokolewa.
2. Neema ya Utakaso; Neema hii inakupa wewe kufanana na Kristo.
Yohana 17:17 “ Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Ukiona umenajisika kimbilia katika Neno la Mungu kwa maana Neno la Mungu ni kweli hivyo litakutakasa. Kama mtu amelaani maisha yako soma Neno la Mungu, kama mtu amenena kinyume na Baraka zako soma Neno la Mungu litakutakasa. Soma Neno la Mungu na litatakasa akili yako, nafsi yako na roho yako.
OMBI:
Bwana Yesu kwa Neno lako takasa nafsi yangu, roho yangu na akili yangu.
Kama unataka Neema ifurike ndani yako ni lazima ujue maana ya Neema na aina za Neema, ukijua hayo kamwe hautarushwa rushwa huku na kule katika Wokovu wako, wala hautakuwa mwiba kwa mtu yeyote katika utumishi wako. Kama unajua namna ya kuheshimu Neema utapandishwa cheo kila mahali na utakuwa Mtu Mkuu.
3. Neema ya Kutumika;
Aina hii ya Neema inatupa kumtumikia Mungu na inatupa kibali cha kuwatumikia wengine. Unaweza ukawa na Neema ya Mungu ya kuhubiri, ukawa muhudumu, mwimbaji, mtoaji n.k, kwa Neema hii ambayo Mungu amekupa ya kutumikia wengine ndipo wewe unabarikiwa. Unatumika mbele za Mungu kwa sababu Mungu amekupa Nguvu ya Neema ya kutumika na siyo kwa nguvu zako hivyo unapokuwa katika utumishi wowote usijiinue bali mshukuru Mungu na usione wengine hawafai.
Palipo na Neema ya kutumika hapo ndipo unapoona upekee wa mtu, ukitaka kuwa mtu wa tofauti omba Neema hii ya kutumika kwa maana Neema hii itakufanya uwe tofauti na wengine kwa maana hiyo kila mtu atatamani akukaribie kwa maana unavutia. Ukiwa na Neema ya kutumika utavutia wengi wapate kumjua Mungu wako.
Wakati mwingine katika kumtumikia Mungu kuna vikwazo, kuchoka na kurudishwa nyuma lakini kwa kupitia Neema ya Mungu utashinda.
OMBI:
Muombe Mungu akusaidie uweze kumtumikia ili uweze kupokea thawabu kutoka kwake.
KANUNI ZA KUISHI KATIKA NEEMA YA MUNGU.
1. Ondoa udhuru; Kama unataka kuona Neema ya Mungu ikifanya kazi ndani yako na kuongezeka ondoa udhuru. Udhuru ni adui mkubwa sana wa kuzuia Neema kuongezeka kwako kwa sababu udhuru unatokana na ibilisi; na ukiwa na udhuru unaonyesha kwamba wewe ni mtu wa nia mbili. Hakikisha unapambana na udhuru katika kutumika kwako. Yeyote ambaye ana Neema ya kutumika hana udhuru kabisa.
Yeremia 1:4-7 “Neno la BWANA lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.”
Yeremia alianza kutoa udhuru mbele za Mungu, akimwambia Mungu kuwa yeye ni mtoto, lakini Bwana akamwambia lazima ufanye.
2. Elewa kuna uwepo wa Neema ya kutosha, ukikutana na changamoto iambie akili yako ya kuwa unayo Neema ya kutosha na hakuna kitakachokuharibu.
3. Usiitumie Neema ya Mungu aliyokupa katika mtazamo hasi juu ya wengine,
4. Jinyenyekeshe, hakikisha unakuwa mnyenyekevu, unyenyekevu unaleta kuinuliwa na msaada kutoka juu, wale wote ambao ni wanyenyekevu ukijaribu kupigana nao kamwe hautashinda kwa maana Mungu anawapigania. Adui anakushinda kwa sababu hauishi katika unyenyekevu, kuwa mnyenyekevu haina maana ya kuwa unapaswa kukubaliana na kila kitu, la! Bali wakati mwingine ni lazima uchakate mambo kabla ya kusema ndio. Kuwa mnyenyekevu haina maana ya kutembea kinyonge, la! Bali ni kumjua Mungu wako, kulijua Neno lake na kulifanyia kazi sawa sawa. Huwezi kutenganisha unyenyekevu na Neno la Mungu bali ukilijua Neno la Mungu litakupa kwenda sawa sawa na mapenzi ya Mungu.
UKIRI:
Ninayo Neema ya kutosha inayonizunguka, hakuna cha kunizuia wala cha kunitisha; hakuna kurudishwa nyuma wala kufilisika kwa maana ninayo Neema ya kutosha inayonizunguka.
Mimi Nina kibali mbele za Mungu hakuna cha kunizuia.
TANGAZO:
Umepokea maneno mengi ya kukatisha tamaa lakini sasa nakutangazia pokea Neema ya kutosha, utavuka hapo ulipokwama nawe utakuwa salama.