Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Maombi

Watch Now

Download

Maombi

MTUME SUZAN MUNGY
Yohana 17:1-10 “Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma………….”
Uzima wa milele ndio huu ya kwamba tumjue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo aliyetumwa. Mimi na wewe tuliookoka ni wa Yesu, na wote walio wa Yesu ni wa Mungu, na Yesu ametukuzwa ndani yetu.
Yohana 17:11-12 “Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.”
Haya yalikuwa ni maombi ambayo Yesu alituombea kabla hajaondoka; kwa maana hiyo ulinzi kwetu ni wa uhakika na tulisha pewa; Yesu alituombea kabla hajaondoka. Yesu anategemea sisi tuliookoka tuwe na umoja kama wao Baba, Mwana na Roho Mtakatifu walivyo, je! Sisi ndani ya Kanisa tuna umoja?
Lakini pia Yesu ameahidi kutulinda; tatizo lolote linapokujia unapaswa kurejea na kukumbuka tu ya kuwa Yesu alikuombea tayari na kwa kupitia Jina lake wewe uko salama. Unapopatwa na jambo lolote ambalo haulielewi liitie hilo Jina la Yesu kwa maana lina ulinzi nawe utakuwa salama.
Yohana 17:12 “Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.”
Yesu kwa Jina lake alitulinda, akatutunza na akahakikisha ya kuwa hakuna hata mmoja wetu kati ya wale waliomkimbilia atapotea.
Lakini pia Yesu akasema; Yohana 17:14 “Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.”
Baada ya wewe kuokoka unatakiwa kushangaa sana unapoona ulimwengu ukikupenda, bali furahi unapoona wanakuchukia, kwa maana Yesu alisema “nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia;” Wengine baada ya kuokoka wamekataliwa na wazazi wao, ndugu zao, waume zao na hata marafiki pia; unapaswa kutambua kuwa wale waliokukataa ni wa ulimwengu tu, usisikitike kwa nini wanakukataa na kukuchukia bali kumbuka ya kuwa umembeba Yesu na wale waliombeba Yesu ulimwengu lazima uwakatae. Haijalishi nani anakukataa lakini tambua kuwa Yesu yupo pamoja na wewe.
Yohana 17:15-19 “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli.”
Yesu alijiweka wakfu yeye mwenyewe ili sisi tuweze kutakaswa na hiyo kweli, na kwa Jina lake alitulinda, alitutunza na akahakikisha hatujapotea, hii ndiyo kazi ambayo Yesu ametuachia ya kwamba kwa Jina lake tukawatafute waliopotea, tuwalinde na kuwatunza na kuhakikisha wale walimpokea Yesu (waliookoka) wasipotee; je! Kwako wewe uliyeokoka ni wangapi umewapoteza? Ni wangapi uliwashuhudia lakini leo hawapo tena kanisani? Au ni wangapi umewatunza mpaka sasa wako salama ndani ya Yesu Kristo?
Unapaswa kutambua kuwa ipo siku utaulizwa kwa maana hii ndiyo kazi kubwa tuliyoitiwa humu ulimwengiuni.
Biblia inasema katika; 1 Wakorintho 3:8 “Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.” Sawa sawa na unavyotaabika ndivyo thawabu yako inavyokuwa, ili uweze kufika mahali pa wewe kupokea thawabu yako kutoka kwa Baba yako wa Mbinguni lazima ukubali kutaabika pamoja na Yesu.
Lakini unapaswa kutambua kuwa kazi unayoifanya itapimwa kwa moto, sasa itategemea na wewe uliye mjenzi umejenga kwa nyasi au dhahabu; je! Hiyo kazi yako ikipitishwa kwenye moto itadumu au itaungua? Sawa sawa na unavyojitaabisha ndivyo thawabu yako itakavyokuwa.