Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Watch Now

Download

MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
Kuna mambo unayofanya na matokeo yake unamsababisha Mungu aseme na kufanya jambo kwako. Isaya 65:24 “Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Hii ina maana gani? Mungu hajibu kwa sababu umesema, Bali ni kwa sababu umefanya jambo ndipo unamsababisha Yeye aseme au atende kwako. Kumsababisha Mungu asimame kwa ajili yako lazima umchokoze kwanza, mfanye Yeye atende kwako kwa kufanya jambo katika Ufalme wake.
Mungu anasikia maombi ya wengi wakiomba lakini anawajibu wachache, kwa nini? Kwa sababu kuna mambo ambayo unapaswa kufanya.
Kama unataka kumgusa Mungu na kumfanya atende kwa ajili yako unapaswa kufanya yafuatayo:-
1. Utoaji wa kupitiliza matarajio au kilichotarajiwa.
Kwa nini malkia wa sheba utoaji wake unakumbukwa mpaka leo? Kwa sababu alitoa kuliko matarajio yaliyotarajiwa. Utoaji wa ziada ndio unaomchokonoa Mungu na humsababisha akuulize unataka nikutendee nini? Kuna mambo mengine unaweza kuomba sana lakini Mungu hatajitokeza mpaka utoe zaidi ndipo utamsababisha ajitokeze kwako na kukuuliza unataka nikutendee nini?
• 2 Nyakati 1:7-13 “Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi……….”
Suleiman alitoa zaidi na hata akaugusa moyo wa Mungu ndipo Mungu akauliza unataka nikufanyie nini? Usimtolee Mungu kwa sababu unacho cha kutoa bali toa zaidi ili kuugusa moyo wa Mungu na kusababisha Mungu atende kwa ajili yako.
2. Unapoijenga nyumba ya Bwana Mungu wako utukufu unakuwa ni wa kwako. 2 Mambo ya Nyakati 7:1-3 “ Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukaijaza nyumba. Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa BWANA, kwa kuwa utukufu wa BWANA umeijaza nyumba ya BWANA………..”
Unapoacha kila kitu ili kuijenga Nyumba ya Bwana Yeye atakutakasa wewe na kila kitu kinachokushika na kukusumbua na kukutoa katika kuwa mateka na hata kukufanya uwe Utukufu kwake. Ukitaka kuuona Utukufu wa Mungu kwako hakikisha unaijenga Nyumba ya Mungu. Utukufu wa Mungu ni ulinzi wako. Ukielewa hili hakuna anayeweza kukuangamiza kwa maana Utukufu wa Mungu unakuwa upo juu yako ili kukulinda.