Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ibada ya jumapili Desemba 3 – 2023

Watch Now

Download

Ibada ya jumapili Desemba 3 – 2023

Mungu akikujalia kusikia kutoka ndani yako kwenda ibadani, kama unatamani kusogea uweponi mwa Bwana maana yake ni kuwa neema ya uzima wa milele unayo.
Daudi alisema katika Zaburi 27:4 “Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.”
Hili ndilo lilikuwa ni tamanio la Daudi kwa Mungu wake, tamanio lake halikuwa fedha, chakula, uzima, wala kuinuliwa, lakini ombi lake kwa Mungu lilikuwa apate kukaa nyumbani mwa Bwana. Kwa nini nyumbani mwa Bwana? Kwa sababu hii; Zaburi:27:11 “ Ee Bwana, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;”
Ukikaa nyumbani mwa Bwana Yeye atakufundisha na kukuongoza katika njia ya salama, na mkononi mwake utakuwa salama.
Unaweza ukawa ni muhudhuriaji mzuri wa kanisani lakini sio mwenyeji, Daudi alitamani awe mwenyeji wa nyumbani mwa Mungu na sio mpitaji wala mgeni. Kanisani kuna watu wa aina mbili wahudhuriaji na wafanya ibada, je! Wewe ni muhudhuriaji au ni mtu wa ibada? Unaweza kujibaini wewe mwenyewe.
Utajuaje kuwa wewe ni mtu wa ibada?
1. Utaijua njia ya uzima, ukiijua njia ya uzima maana yake uzima wa milele ni wa kwako, na kwa maana hiyo hata ukifanya kosa Roho Mtakatifu atakwambia hii siyo sawa ili upate kujirekebisha ili usipotee, ukifanya sawa sawa anakwambia ongeza mwendo.
Hii siyo kwa sababu wewe ni muhudhuriaji mzuri wa kanisani, la! Bali ni kwa sababu wewe ni mtu wa ibada. Kwa nini Sauli alikufa mapema? Kwa sababu Bwana hakusema naye, si kwa ndoto wala maono wala kwa kupitia Manabii. Ukiishi huku duniani na unasema umeokoka lakini Bwana hasemi na wewe kwa namna yoyote ile kwamba hapa umekosea au hapa uko sawa, jua kuwa wewe ni muhudhuriaji tu wa kanisani na sio mtu wa ibada.
2 Mambo ya Nyakati 7:1-3 “Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba. Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana…”
Mungu hakushuka kwa sababu ya yale maombi ya Sulemani, la! Watu wengi wanafikiri ni kwa sababu ya maombi, kwa sababu hawakujua nini kimotokea. Maombi yalikuwa ni kukabidhi kile ambacho walikuwa wamefanya (ujenzi wa hekalu) kwa Mungu hivyo Mungu hakupokea maombi bali alipokea kile walichokuwa wamekifanya, kwa sababu hiyo Mungu alishuka na utukufu wake. Ni kipi kinamfurahisha au kumchokoza Mungu? Mungu mara zote hutazama watu wa ibada, ibada ni nini? Ni kutoa, kile unachokitoa ndicho kinachobeba ibada yako, je! Wewe unafanya nini? Sio kipi unachokiomba, kwa sababu Mungu ni mtendaji na sio mwana maombi.
Mungu alimuumba mtu awe mtendaji na sio mwana maombi, Mungu aliwapa majukumu, hakusema ninakuumba wewe mwanadamu ili uniombe mimi, la! Bali alimuumba mtu na kusema “ na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu” sisi ni mfano wa Mungu, Mungu ni nani? Yeye ni muumbaji, mtawala na mtendaji. Mungu anataka kuona vitendo na sio maombi yako. Mungu alikuumba ili ufanye kitu. Kwa nini kuna umaskini mwingi huku duniani? Kwa sababu wanadamu walio wengi ni wavivu hawataki kufanya chochote bali wanataka miujiza tu itokee, jambo lolote haliwezi kutokea kwako kama haujalifanyia kazi.
Hesabu 14:10 “Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.”
Ukiwa tayari kuufia Ufalme wa Mungu, kulipa gharama na kutoa maisha yako kwa ajili ya Mungu, watu watainuka, adui atakuja mbele yako ili kukuzuia, vikwazo vitajitokeza kukushambulia lakini mbingu haitakaa kimya bali itashuka na utukufu wake. Kwa nini utukufu ulishuka? Ulishuka ili kuwatakasa walioisema kweli na kuwalinda.
Utukufu wa Mungu ni ulinzi, palipo na utukufu kuna ulinzi na kudumu, maongezeko na kuzidi. Ndani ya utukufu kuna vingi unavyovihitaji katika maisha yako kutoka kwa Mungu.
Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”
Ukifanya mambo kwa ajili ya Mungu utukufu wa Mungu utakuwa juu yako hautakufa kabla ya wakati wako, sio kwa magonjwa wala ajali kwa sababu utukufu wa Mungu uko juu yako. Utukufu ni maongezeko yako na ni kila kitu unachokihitaji.
Unapoishi huku duniani na umeokoka acha kuomba maombi ya kijinga, Mungu nipe chakula, acha ujinga muombe Mungu akupe kujua ufanye nini kwa ajili yake akikuelekeza cha kufanya na ukisha kifanya ndipo uweza wa Mungu utakufuata na siku baada ya siku afya yako inarejeshwa, ndoa yako inahuishwa na familia yako inawekewa msingi imara. Acha kuomba maombi ya Mungu niponye, mwambie Mungu “najua nilikuwa mbali na wewe na sijafanya kitu kwa ajili yako niambie nifanye nini ili nikufurahishe” hakika roho wa Mungu hatakaa kimya bali atakuja na utukufu wake.