Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mahubiri Jumapili 08 Januari 2024

Watch Now

Download

Mahubiri Jumapili 08 Januari 2024

Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.”
Wakati wetu wa kumiliki umefika na tangazo kwamba mwaka 2024 ni wakati wetu wa kumiliki limekwisha kutoka.
Biblia inasema “katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu;” mlima Sayuni ni mahali patakatifu, ni mahali ambapo wana wa Israel walimjengea Bwana Hekalu, Mlima Sayuni unawakilisha utakatifu, na mlima Sayuni ni wewe na umeanza kuwepo mahali pa takatifu hivyo utakwenda kumiliki vile ambavyo unapaswa kumiliki. Ili uweze kumiliki ni lazima uende katika nyumba ya Bwana mahali patakatifu.
Mwaka huu natamani mimi na wewe tuelewe kwamba tukiwa mlima Sayuni adui hataweza kutuibia, kutupokonya wala kutuchokoza bali tutamiliki milki yetu ambacho Bwana ametupa.
UKIRI:
Bwana mwaka huu ninamiliki milki zangu zote, hata zile nilizopoteza kwa adui ninakwenda kuzikomboa zote; napokea ahadi zangu zote kwa Jina la Yesu.
Katika mwaka wetu huu wa kumiliki tujifunze kupitia safari za wana wa Israel; safari hiyo itatupa kujifunza kupitia wao pale waliposhindwa ili tupaepuke na yale waliyoshinda ili tuweze kujua namna ya kushinda kwa sababu umiliki ulikuwa ni semhemu ya safari yao.
Biblia inasema katika; Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.” Hii inamaana kuwa iwapo utakaa mlima Sayuni (kwenye uwepo wa Bwana) adui hawezi kukunyang’anya umiliki wako bali utakuwa ni wako na utakuwa nao milele na milele.
Usisahau kuwa tumetangaziwa kumiliki lakini pia unapaswa kujua kuwa katika tangazo hili adui naye amesikia mbiu hii ya umiliki, hawezi kufurahi kuona wewe ukimiliki. Sawa sawa na wewe ulivyojiandaa kumiliki na yeye anajiandaa namna ya kukunyang’anya umiliki wako. Lakini ili uweze kumiliki milki yako na adui asipate nafasi ni lazima urudi katika mstari, ili safari yako ya umiliki iendelee mbele.
Ili usipoteze umiliki wako lazima ung’ang’ane na utakatifu ili uweze kumiliki milki yako. Rudi kwenye mstari, amua kukaa mlima Sayuni (mahali patakatifu) na ukikaa hapo utamiliki, na sio kumiliki tu utazidisha na kuzalisha. Mara nyingi watu wakishapata fedha wanakuwa bize na kujifanya hawana muda wa kwenda kanisani tena, mpendwa rudisha gari barabarani.
Yakobo 4:27 “wala msimpe Ibilisi nafasi.” Usimpe ibilisi nafasi ya kukunyang’anya vya kwako, kwa maana nyingine amua kuishi maisha matakatifu kwa maana ukiishi katika utakatifu hata kama adui atakutegea mitego ya aina gani Roho Mtakatifu atakuambia na atakupa namna ya wewe kutegua hiyo mitego nawe utakuwa salama.
Ili uweze kuzungumza na Roho Mtakatifu lazima uwe Mtakatifu. Lazima ukae Mlima Sayuni (mahali pa ibada, mahali patakatifu) rudi katika Utakatifu wako ili uweze kumiliki milki yako aliyokuandalia Baba yako wa mbinguni.
Mpendwa milki yako ipo tayari unasubiriwa wewe ukae katika nafasi yako ili uweze kuchukua umiliki wako. Kwa maana Biblia inasema katika; Mithali 13:22 “Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.” Kaa katika nafasi yako ili uweze kumiliki milki yako.
Ni kweli tunashangilia umiliki lakini unapaswa kujua kuwa katika kila ahadi ya Mungu kuna kanuni yake ili wewe uweze kuipokea hiyo ahadi yako.
Katika wakati wetu huu wa kumiliki chochote unachokipata lazima uulize kwanza ni nini mapenzi ya Mungu katika hicho ulichokipokea.
Mithali 6:9 “ Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.” Uvivu utakufanya upoteze vyote unavyopaswa kumiliki. Lazima tuondokane na uvivu ili umiliki wetu uwe wa kudumu.
Vitu vitatu vitakavyochochea umiliki wetu mwaka 2024:
• Maombi
• Shukrani
• Utoaji
Mara nyingi watu wakipata husahau haya na matokeo yake wanampa ibilisi nafasi katika maisha yao na ndipo wanapoteza kila walichonacho. Lakini ukizingatia mambo hayo matatu yatakulinda usipoteze umiliki wako.