Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI 14/01/2024: KUVUKA MIPAKA

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI 14/01/2024: KUVUKA MIPAKA

KIONGOZI WA KIROHO KANISA LA EFATHA – MTUME NOEL KAPINGA
Mwaka huu unakwenda kubadilisha historia ya maisha yako, kila kitu kinaenda kubadilika katika maisha yako kwa sababu ni mwaka wa kumiliki kwako. Huu ni wakati wa kupokea nguvu ya kukuwezesha kuvuka mipaka ili uende kumiliki.
Ili uweze kumiliki milki yako, kama kuna mipaka imekuzuia itaondolewa na hautabaki vile vile; siku ya leo Mungu akakupe kuvuka hiyo mipaka, viza yako inagongwa muhuri leo ili uende ng’ambo ya pili ya maisha yako, iwe unataka au hautaki. Mpaka uliokuzuia ili usiende unakotakiwa kwenda ukakuachie leo kwa Jina la Yesu.
Neno limekwisha kutoka kuwa huu ni mwaka wetu wa kumiliki, Mungu akakupe nguvu ya kukuwezesha wewe kumiliki milki yako. Ukiipokea hii nguvu hakuna mpaka utakaokuzuia katika maisha yako, iwe ni wa kichawi, mapepo au mizimu utauvuka kwa Jina la Yesu.
Kutoka 34:24 “Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu ye yote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za Bwana Mungu wako mara tatu kila mwaka.”
Ili uweze kumiliki ni lazima uvuke mipaka uliyowekewa, lazima ubaini umewekewa mipaka ya aina gani ili uweze kutoka hapo ulipo.
Aina ya mipaka ambayo unatakiwa uivuke mwaka huu:
1. Mipaka ya kifikra:
• Mungu akitaka kukumilikisha kwanza anabadilisha namna ya kufikiri kwako, unavyochukulia mambo na kutafakari kwako ili uweze kumiliki. Watu wengi wameshindwa kumiliki kwa sababu ya namna wanavyowaza.
• Mpaka huu ndio ibilisi anautumia sana ili kuwafanya watu washindwe kuwaza sawa sawa na vile Mungu alivyowakusudia. Mtu mwenye mipaka ya kifikra ni ngumu sana kubadilika kwa sababu ngome imejengwa katika akili yake ni mpaka tu pale ambapo hiyo ngome itabomolewa ndipo anaweza kufikiri sawasawa na Mungu alivyomkusudia.
Lazima uhakikishe unashinda mipaka ya kifikra kama unataka kumiliki.
Mipaka yako ya kifikra mwisho leo, namna unavyojiwazia na kuwawazia wengine vibaya lazima kuishe leo. Mara zote umekuwa ukiwawazia watu vibaya, unahisi watu hawakupendi, umesababisha hata kuwa na tabia ya kujihami kwa sababu ya mipaka ya kifikra. Ukikosea tubu usijihami, lazima ubadilishwe fikra zako ili uwaze kama Mungu, kujihami hakusaidii lazima ubadilishe fikra zako; ukijihami unasababisha dhambi yako inakomaa na kuwa sugu, lazima utoke hapo kwa Jina la Yesu
MAOMBI:
Giza lolote kwenye fahamu zangu lazima liachie fahamu zangu, kuanzia sasa nataka nifikiri kama Mungu anavyonifikiria na niwaze kama Mungu anavyoniwazia na ngome yoyote inayonizuia kumiliki ikabomolewe kwa Jina la Yesu.
UKIRI:
Bwana Yesu tabia yoyote inayonifanya niwe sugu kifikra lazima ishindwe kwa Jina la Yesu.
Aina ya mipaka ambayo unatakiwa uivuke mwaka huu:
2. Mipaka ya ndoa na familia: ibilisi anaweza kuweka mipaka katika ndoa ili wahusika wasifurahie ndoa yao, au anaweza kuruhusu mfurahie ndoa mwanzoni katikati kuwe na vurugu ili mwisho wenu uwe mbaya.
OMBI:
Mipaka yoyote kwenye ndoa yangu naiondoa kwa Jina la Yesu, kiambaza chochote kilichojegwa katika ndoa yangu kikabomoke kwa Jina la Yesu.
3. Mipaka ya kiuchumi: Mipaka hii haiangalii unanena kwa lugha au unakarama zote za rohoni bali yenyewe inakuwepo tu, haiangalii cheo chako cha kiroho, mwaka huu ukavuke kwa Jina la Yesu.
• Mipaka hii ya kiuchumi haimruhusu mtu aone cha kufanya ili asipate kipato au wengine wameona cha kufanya lakini wanaahirisha kile kitu.
• Ukiwa na mipaka ya kiuchumi unaweza ukaanzisha mradi fulani lakini lazima huo mradi utakufa. Nenda kautamkie mradi wako uliokufa ufufuke kwa Jina la Yesu.
OMBI:
Mipaka yoyote ya kiuchumi achia akili yangu kwa mamlaka ya Jina la Yesu, huu ni mwaka wangu wa kumiliki, wewe mradi uliokufa unaenda kufufuka tena, mradi ulioishia njiani unaenda kufufuka kwa Jina la Yesu. Kumbu kumbu la torati 8:18 “Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.”
Bwana wa mabwana ile roho ya mauti inayokuja kuua kila nilichokianzisha saa hii iondoke kwenye mipaka ya biashara yangu kwa Jina la Yesu, ile nguvu ya giza iliyopo inayonifanya nishindwe kufanya vizuri katika biashara yangu ondoka kwangu kwa Jina la Yesu.
Kwa Jina la Yesu chochote nilichoanzisha hakitakufa kwa maana mimi sina roho ya mauti nitakula matunda ya kile ninachokifanya ile nguvu ya ibilisi iliyokuwa inanizuilia nisile matunda ya mikono yangu kamwe haitakuwepo tena kwangu kwa Jina la Yesu.
TANGAZO:
Hesabu 32:32 “Tutavuka, hali tumevaa silaha zetu, mbele za Bwana, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng’ambo ya pili ya Yordani.”
TUTAVUKA tukiwa tumevaa silaha ambazo ni Neno la Mungu, Maombi na Shuhuda. Tamko la kitume kuwa huu ni Mwaka wetu wa Kumiliki limekwisha kutoka, ni wakati wetu wa kumiliki; nenda ukamiliki kwa Jina la Yesu.