Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 03/03/2024

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 03/03/2024

SOMO: UTII

Daniel 10:7-8 “Nami, Danielii, nikaona maono haya peke yangu; maana wale watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona maono haya; lakini tetemeko kuu liliwashika, hata wakakimbia ili kujificha. Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu.”
Huyu alikuwa ni Malaika anakuja kusema na Daniel na watu waliokuwa karibu na Daniel wakakimbia na kujificha kwa sababu ya uwepo wa yule Malaika. Wakati mwingine ni kwa sababu ya pendo la Mungu, tunakuja Kanisani tunaabudu na kusema hayo tunayoyasema na kufanya hayo tufanyayo kwa sababu Mungu ni Pendo, lakini anaposimama kama Mungu Muumbaji, kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana na enzi yake yote usifikiri ni rahisi kwako kukaribia Uwepo wake au kumsogelea, lakini unapaswa kutambua hili ya kuwa Mungu anakupenda na ndio maana anakuja kwetu kama Pendo.
Daniel akasema “nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu;” Nguvu zinatoka wapi? Kwa Mungu, unatembea, unaona, unasikia, unakula na kufanya mengine yote kwa sababu Mungu amekupa nguvu ya kufanya hayo yote; wala usiseme unajua ninaamka asubuhi sana nina Nguvu sana, mpendwa mshukuru Mungu.
Daniel 7:10-11 “Na tazama, mkono ukanigusa, ukaniweka juu ya magoti yangu, na vitanga vya mikono yangu. Akaniambia, Ee Danielii, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.”
Hauendi Kanisani kwa sababu unajua kuabudu sana, la! Bali ni kwa sababu ya Pendo la Mungu limekujia.
Usifanye jambo kwa Mungu kwasababu wengi wanafanya, bali fanya kwasababu wewe umeelewa unachofanya. Unaporuhusu UTII uwe sehemu ya maisha yako, utapata USAIDIZI kutoka JUU.
Ni kupitia UTII pekee unapewa kuinuliwa na kuwa na jina kuliko ndugu zako na wanaokuzunguka.
Huhitaji kufunga na kuomba ili Mungu aseme na wewe, bali unatakiwa uelewe na ukielewa Yeye atasema na wewe. Unapokuwa tayari kumsikia Mungu Yeye anakuja na kusema na wewe. Unaweza kufunga na kuomba lakini Mungu asiseme na wewe, ukahisi Mungu hakusikii.
Unapaswa kutambua kuwa kufunga na kuomba ni maandalizi ya wewe kusema na Yeye, wengi wanafikiri wakifunga na kuomba ndio wakati wa kusema na Mungu, la! Bali unapaswa kutambua kuwa huo ni wakati wako wa kujiandaa ili uwe tayari kusema na Yeye. Daniel alifunga na kuomba siku kwa siku baada ya kumaliza maombi yake ndipo Mungu akamjibu, akasikia maombi yake, wakati gani? Alipokuwa tayari ndipo Malaika akasema Daniel 10:12 “ Ndipo akaniambia, Usiogope, Danielii; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.” Hii inamaana kuwa ukiwa tayari kusikia ndipo Mungu anamtuma mjumbe wake kwako ili kusema na wewe. Kwa nini? Kwa sababu unakuwa upo tayari kusikia.
Watu wengi wanafunga na kuomba kwa sababu ni wagonjwa, hivyo wanataka Mungu awaponye na sio wanafanya kwa sababu wanataka kumsikia Mungu bali wanafunga kwa sababu wanataka usaidizi wake. Wengi wetu tunapofunga na kuomba ni kwa sababu tunataka kupeleka maombi mbele za Mungu, hii ni sawa, lakini swali ni kuwa, je! Yesu alipokuwa anafunga na kuomba kwa siku 40 alikuwa anaomba nini? Hakuomba chochote bali alikuwa anajiandaa kwa ajili ya kazi kubwa mbele yake. Kwa sasa unahitaji kujiandaa ili kumsikia Bwana wako. Kwa nini ibilisi alikuja kwa Yesu baada ya kumaliza kufunga? Hapa ndipo wengi tunafeli, kwa nini ibilisi anakuja mwisho? Ni ili kukurudisha mwanzo.
Mwana wa Mungu ukifanikiwa kufunga na kuomba na ukamaliza hakikisha unaishi kama vile ulivyokuwa unafunga.
Lengo la kufunga ni ili kuuadabisha mwili ili tuweze kuongea na Mungu, kama umefunga ni ili mwili usiwe na nafasi kubwa kwako upate muda wa kuongea na Mungu. Baadhi ya watu wakimaliza kufunga ndipo sasa wanafungulia kila kitu, unakuta wanaanza kusengenya hii inamaana kuwa hawampi Mungu nafasi ya kuongea nao.
Siku ukifunga na siku unamaliza ukaendelea kuyafungia yale uliyokuwa umeyafunga ndipo sasa Mungu ataanza kutembea na wewe.
Mwana wa Mungu ukitaka kuchanua usisubiri Utukufu wako Mbinguni bali Utukufu wako unaanzia hapa duniani.
Huu ni Mwaka wetu wa KUMILIKI, hauwezi Kumiliki kisicho cha kwako, bali Utamiliki kile kilicho cha kwako, hivyo kama hauna ambacho Unamiliki, Je! Utamiliki nini? Tangu mwanzo Mungu alimpa Mtu MAMLAKA YA KUMILIKI, alimpa Anga ili ajaze na fahari yake. Anga na Bahari vyote vilikabidhiwa kwa Mwanadamu ili kuonyesha UMILIKI wake.
Nini kilitokea hata mwanadamu hamiliki? Kwa sababu ya ukosefu wa Utii ambao uliruhusu dhambi kuingia. Vurugu zote unazoziona huku duniani ni kwa sababu ya dhambi, magonjwa, mauaji, njaa, kupambana kumetokana na kutokutii. Kungángána katika ndoa ni zao la kutokutii ambako kunazaa dhambi na hiyo dhambi inaleta vurugu zote hizi.
Mwanzo 3: 23-24 “Kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.” Bwana alimfukuza Adamu mahali pa utele, utele chanzo chake ni Mungu na uhitaji chanzo chake ni dhambi.
Mungu hashindwi KUTUPONYA au KUBADILISHA Maisha yetu, kinachotutesa tunafikiri sisi tunaweza wenyewe, hakuna ugonjwa mkubwa wa kumshinda Yesu ila fahamu kuwa kuna mahali tu haujakubali kuwa Mtii.
Maisha unayoishi hayajamshinda Yesu kuyabadilisha lakini wewe unaishi hivyo kwa sababu haujaamua kuwa Mtii. Maana Yesu alichukua madhaifu yetu ili Sisi tuwe WAZIMA. Inapofika wakati wa Kutii uwe tayari hata ikiwezekana kumwaga damu na Yesu atakuwa pamoja na wewe.
Unapotii MAMLAKA iliyokuzidi ndivyo unaweza kutiisha mazingira yanayokuzunguka. Siku ukiamua Kutii utatiisha pesa, utatiisha magonjwa na kila unachotaka kikutii na hakuna kitu kitakachokuwa kinyume chako na kukushinda.