Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 21/04/2014

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 21/04/2014

HAKI TULIZONAZO KATIKA BWANA
Wefeso 1:3 ” Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”
Tumebarikiwa baraka zote tunazozihitaji huku chini ya jua, hakuna hata moja ambayo tumenyimwa.
UKIRI:
Mimi nina baraka zote, hakuna hata moja niliyonyimwa, kama kuna jambo linaloitwa baraka mimi ninazo zote; kama kuna kitu kinahitaji baraka, mimi ninazo zote; kama kuna mtu anazo baraka basi mimi ninazo zote.
Neno linasema baraka hizi zipo katika ulimwengu wa roho na sio mwilini, Mungu aliye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na aliye Baba yetu ametubariki kwa baraka zote za rohoni na sio za mwilini. “aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”
Vyote unavyoviona huku chini ya jua asili yake ni rohoni, kama haujavipata rohoni basi jua kuwa wewe ni mwizi kama ibilisi, ibilisi anaitwa mwizi kwa maana yeye anaiba.
Baraka ambazo mimi na wewe tumepewa ni za rohoni na ni za ulimwengu wa roho ili uweze kuzipata inakupasa uwe rohoni ili uweze kuzifikia hizo baraka zako. Kuwa rohoni ndiyo siri ya kwanza ya kuingia na kuchukua vilivyo vya kwako.
Mungu amekubariki kwa baraka zote lakini kwa nini hauzipati hizo baraka?
Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.”
Mungu anasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;” Wanao angamia sio watu wa dunia hii, la bali ni watu wa Mungu, je wewe ni wa Mungu? Kama jibu ni ndio na haujazipata baraka ni kwa sababu unaangamia kwa kukosa maarifa. Nini kinacho kuangamiza? Ujinga (kukosa maarifa), anayekuangamiza sio ibilisi kwa maana wewe ni wa Mungu tayari. Walokole wengi wanahangaika na ibilisi, wewe uliyeokoka unapaswa kutambua kuwa ibilisi hana kitu na wewe tena, kinachokutesa ni kutokuwa na maarifa (ujinga).
Mithali 9:6 “ Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.”
Maana yake ni kwamba mjinga haishi, kwa nini? Kwa sababu mara zote unakuta ana presha, kisukari, hana fedha yaani ni maskini, ana mapepo n.k, kwa nini kwa sababu hajapata maarifa ya kujitambua yeye ni nani kwa Baba yake wa mbinguni kwa maana hiyo ni mjinga (hana ufahamu). Lakini Biblia inasema ukikubali na kutii utakula mema ya nchi, Isaya 1:19 “Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;”
Ujinga ni kiwango cha juu cha kutokumjua Mungu, kwa maana neno linasema “kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa” inamaana kuwa ukimjua Bwana ndipo unapata maarifa na ujinga unaondoka kwako.
Yesu akasema Mathayo 6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Ukiupata huo Ufalme wa Mungu hakuna kitakachokusumbua; siyo chakula, mavazi, malazi na kila unachokihitaji kitakuwa cha kwako.
Yale niliyoadhimia moyoni baada ya kuokoka:
1. Kujitambua;
Baada ya kuokoka nilitaka kujitambua mimi ni nani kwa Baba yangu wa mbinguni; Wewe uliyeokoka kitu cha kwanza unachopaswa kukifahamu ni kujitambua wewe ni nani, wewe ni mwana wa Mungu kwa maana Neno linasema “bali wote waliompokea aliwapa uwezo wakuwa watoto wa Mungu” kuanzia hapo anza kuishi kama mtoto wa Mungu.
2. Nilijifunza kufanya kile ambacho Mungu anataka na sio kile nataka.
3. Nilijifunza kumtumikia Mungu kwa sababu ndiyo tabia ya rohoni, usitake kutumikiwa kama haujatumikia wengine, usijitangaze na kusema unajua mimi ni mtumishi, la! Acha kile unachokifanya kikutambulishe. Unakuta wewe ni mtumishi lakini ukisukumwa sukumwa unakasirika, mtumishi lazima achoke kuliko bwana wake, sasa usipotaka kuchoka inamaana kuwa haujakubali kutumika.
Kwa nini watumishi wengi wanakwama? Ni kwa sababu hawako tayari kushuka, maana neno linasema ajishushaye atakwezwa, wewe kubali kujishusha ili Yeye akukweze.
4. Nilitamani kulijua neno lake; manaa Biblia inasema katika Yohana 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Nilipookoka niling’ang’ana kuijua kweli ya Mungu ambayo ni Neno lake. Acha Imani yako isiwe katika misimamo yako bali ijengwe katika Neno la Mungu.
Usifunge na kuomba ili mke au mume wako awe kama wewe, huo ni ujinga na maombi ya aina hiyo utafunga mpaka utoke vidonda vya tumbo na Mungu hatasikia.
Unachotakiwa kuomba ni kumwambia Mungu akupe wewe kujua namna ya kuishi na mke au mume wako. Lakini ukitaka awe vile unavyotaka mtaishia kugombana kila kukicha.
Hivyo ndivyo ilivyo hata katika maisha yetu ya kiroho tumuombe Mungu atupe kuishi na watu wengine hivyo walivyo, tutoke kwenye ujinga kwa maana Mungu hawezi kukubariki wakati wewe ni mjinga.
TANGAZA:
Mimi sio wa mwilini bali ni wa Rohoni na Baraka zangu ni za Rohoni, sikiliza ibilisi, sikiliza wewe mtu wa kale, Mimi ni wa Rohoni na Baraka zangu ni za Rohoni, ndani ya Kristo Yesu.
MAOMBI:
Hosea alisema katika Hosea 4:6a “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;”
Mimi ni mwana wa Mungu na sitaangamia kwa kukosa maarifa, sifi kwa ujinga nitamjua Mungu wangu. Kuanzia sasa ujinga hauna nafasi kwangu bali nitamuelewa Bwana na kile alichonikusudia, nitatenda yale ya rohoni na nitayajua yale ya rohoni.
Neno linasema katika Wagalatia “chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna” kuanzia sasa, sitapanda ujinga kwa maana mimi sio mjinga; sitapanda ujinga nisije nikaangamia, bali nitapanda vya rohoni kwa maana mimi ni mtu wa rohoni na ninataka vyote vilivyo vya rohoni ambavyo Bwana ameniandalia.
Yako mazuri mbele yako ambayo Mungu amekuandalia, usikate tamaa na yale unayoyaona sasa ni ya muda mfupi tu, tarajia mazuri.