Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 28/04/2014

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 28/04/2014

SOMU: UMILIKI
Umiliki ndio msingi wa kile ambacho Mungu amekusudia kwa ajili ya mwanadamu, kwa sababu ya umiliki Mungu aliamua kumuumba mwanadamu, Mungu anamilki na kwa sababu ya hili aliamua kumuumba mwanadamu ili akamiliki milki yake. Mtu mwenye milki nyingi mara zote hugawanya milki yake kwa watu wake.
Mungu anazo milki na aliamua kumuumba mwanadamu ili akamiliki, vivyo hivyo hapa duniani wanadamu ambao wana milki nyingi wanampa mtu amiliki pale na kule na ndio sababu nyakati za zamani, wafalme na wakuu walikuwa wanamiliki vitu vingi na maeneo mengi hivyo wakaoa wake wengi ili waweze kumiliki kile walichonacho. Hivyo Mungu anazo milki na alimuumba mwanadamu ili aweze kumiliki kile ambacho Mungu anamiliki.
Kwa sababu ya hizo milki wewe upo sasa. Wewe upo kwa sababu Mungu anataka umiliki kile anachomiliki Yeye, wewe uko hai kwa sababu Mungu anacho kitu kwa ajili yako ili uweze kukimiliki. Sasa ni wakati wako wa kumiliki na ndio maana upo hai, wafu hawawezi kumiliki, sasa usimuwaze baba yako wala mababu zako ambao walisha kufa, bali huu ni wakati wako wa kupata ufahamu ya kuwa Mungu anazo milki na Mungu anataka wewe ukamiliki. Hauwezi kuipata hiyo milki pasipo kili yako kupata ufahamu.
Hakuna anayeweza kuoa au kuolewa pasipo kuelewa ni kwa nini anaolewa au anaoa, kama sivyo basi hiyo ndoa haitadumu, ndio maana kuna talaka, talaka ipo kwa sababu ya ukosefu wa ufahamu. Kwa nini? Kwa sababu kama kukiwa na tofauti ya kuelewa kile mwenzako anasema lazima mtaishia kugombana.
Ndoa ni kushirikishana upendo na sio makasiriko. Usiongee lugha katili kwa mke wako au kwa mume wako kwa maana huo sio upendo na sio ndoa kwa sababu ndoa ni mahusiano na upendo na sio ugomvi.
Mwanamke muonyeshe mume wako ya kuwa hajakosea kukuchagua, lakini usipofanya hivyo hicho ndicho kinamuumiza mume wako na hicho ndicho kinasababisha wanaume wengi wanakufa mapema. Ni kama vile Mungu alivyomchagua Sauli kuwa Mfalme na baadae Sauli akaonyesha kuwa Mungu alikosea na ndipo Mungu akasema najuta kumchagua Sauli. Wewe mwanamke usisubiri mumeo ajute kukuchagua, mfanye mumeo ajisikie furaha kuwa alifanya uchaguzi mzuri na akijisikia hivyo ndipo ataanza kustawi na matokeo yake familia yenu itastawi.
Mungu aliposema na tufanye mtu alimuumba mwanaume peke yake ndipo kaona kuwa huyo mwanaume hajisikii vizuri na afanye kazi yake vizuri ndipo Mungu akamuumba mwanamke ili aje amfanye mume wake ajisikie vizuri hivyo mwanamke ukifanya vizuri kwa mume wako hakika mtastawi lakini kama sivyo mume wako ataishia kuwa na madeni na magonjwa ya kila aina.
Mfanye Mungu akufurahie ili aweze kukupatia Baraka zake, sisi tuliookoka wote ni ma bibi harusi wa Bwana Yesu, hivyo usimfanye Bwana harusi akukasirikie. Siku zote tamani kumfanya Yesu akufurahie ili aweze kukufurahisha na wewe.
Mungu anazo milki na hizo milki anataka wewe ukazimiliki.
Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Hapa inamaana kuwa Mungu alimuumba mtu kama nakala yake (copy) hivyo lazima upate ufahamu katika hili kwa maana pasipo hili kamwe hautaweza kufanana na Mungu.
Chochote alichonacho Mungu ni cha kwako kwa maana Mungu alimuumba mtu kwa kusudi lake ili afurahie yale aliyoyaumba.
Yoshua 1:7 “Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”
Ili uwe vile ambavyo Mungu anataka uwe unapaswa kuwa hodari na ushujaa mwingi, hii inamaana kuwa ili uweze kuwa vile ambavyo Mungu anataka kuna vikwazo vingi sana ambavyo vinaweza kukusababisha uishie njiani kwa sababu yupo adui hapa duniani ambaye atakuzuia wewe usimiliki.
Kwa nini Mungu aliamua kumuumba mwanadamu? Mungu anazo milki lakini alijua kuwa yupo mvamizi ambaye anataka kunyakuwa na kuiba kile kilicho cha Mungu. Mungu alitaka mwanadamu awepo hapo ili aweze kumiliki hicho ili yule mvamizi asiweze kuchukua. Kwa sababu yule mvamizi atatafuta kuiba na kuvamia, ndipo Mungu anakwambia wewe uwe hodari kwa sababu mvamizi atakuja na ataanza kukutishia akikwambia hauwezi kumiliki, hichi sio cha kwako, hauwezi kuwa bora lakini ukiwa na uhodari na ushujaa utasimama Imara na utaweza kumiliki kilicho cha kwako.
Yoshua 1:8 “Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.”
Hapa kuna mambo mawili, uwe hodari na ushujaa mwingi lakini pia, hakikisha unatafakari neno la Mungu. Jifunze kusema kile ambacho Mungu amekisema kuhusu wewe na sio kile ambacho watu wamesema au kile unachokiona. Kwa sababu ibilisi anaweza kukuletea vitu ili akuchanganye na matokeo yake uweze kusema kile ambacho umekiona na sio kile ambacho Mungu amekisema.
Mwanamke unapoolewa na ukaona mama mkwe amesimama juu yako jua kuwa huyo mume wako anahitaji msaada wa kutoka hapo ili aweze kwenda mbele ndio maana Mungu amekupeleka hapo.
Mungu alikujua akakupeleka kwa mume aliyekupa, anajua mume wako kule aliko anashindwa kwenda anapotakiwa kwenda, hivyo Mungu akakupeleka wewe binti kwa huyo mume ili uweze kumfanya yeye aweze kwenda mbele, sasa ukifika huko usimuangalie mkwe wako wala mawifi zako wanasema nini bali wewe unapaswa kusimama katika nafasi yako ili kumfanya huyo mume wako aweze kwenda anakotakiwa kwenda.
Mungu anasema uwe hodari na mwenye moyo wa ushujaa, Kwa maana usipokuwa hodari na mwenye moyo wa ushujaa utashindwa kufikia mapenzi ya Mungu na ulichokusudiwa na Mungu kwa sababu ya yale yanayoendelea, acha matukio yaendelee kutokea lakini wewe shikilia tukio lako.
MAOMBI:
1. Ruhusu damu ya Yesu kuvunja vunja mawazo yako na kuruhusu mawazo ya Mungu kwako.
2. Ita damu ya Yesu ikavunje na kuondoa kile kinacholeta uadui kati yako na Mungu.