Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI 05/05/2014

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI 05/05/2014

SOMO: MAISHA MATAKATIFU 

Huu ni mwaka wetu wa kumiliki na Mungu ametupa mwaka huu kwa sababu anatuwazia mazuri na anatupenda sisi tulio watoto wake. Mzazi yeyote anamawazo mazuri kwa ajili ya watoto wake, mzazi yeyote hapendi watoto wake wataabike na siku zote anatamani mtoto wake awe bora kuliko yeye, huyu ni mzazi wa dunia hii. Sisi tuliookoka Baba yetu ni wa Mbinguni na ametangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wetu wa kumiliki; Mungu aliposema kuwa huu ni mwaka wetu wa kumiliki alimaanisha anakwenda kutumilikisha vyote alivyonavyo kwa maana Yeye hafurahii uchovu wetu, au kuteseka kwetu.

Baba yetu wa Mbinguni Yeye ni Mtakatifu lakini, tusipokuwa watakatifu kama Yeye hatutaweza kumuona, hivyo kama tunataka kumuona lazima tuishi maisha Matakatifu.

Zaburi 24:3-6 “ Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.” 

Ni nani anayeweza kupanda katika mlima mtakatifu wa Bwana?

• Mtu ambaye mikono yake ni misafi mbayo haijamwaga damu, huyu ndiye anayepaswa kumkaribia Bwana, Je! Wewe mikono yako ni safi?

• Mtu mwenye moyo safi; Biblia inasema “moyo unaugonjwa wa kufisha, je! Ninani anaweza kuujua? Lakini Biblia inasema wale wenye moyo safi ndio wanaweza kumuona Bwana.

• Mtu asiye na hila; “Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila” mtu mwenye hila ni mtu hatari sana kwa maana anaweza kukuchekea lakini moyoni mwake anatamani uangamie. Je! Wewe una hila? Mbona mwenzako akipata hufurahii? Mbona ukiona mwenzako kapanda cheo moyo unakuuma? Mbona ukiona mwenzako biashara yake inachanua hupendi? Ukiona ndoa ya mwenzako inafuraha na amani unaanza kuifuatilia na kuanza kusema unajua huyu angekuwa mume wangu ningefanya hiki na kile, acha kupoteza muda kwa kufuatilia wenzako tafuta wa kwako na wewe tukuone utafanya nini. Ni rahisi sana kukosoa wachezaji ukiwa nje ya uwanja ingia uwanjani tukuone, tuache ushabiki kwenye maisha ya wengine, ukiona mwenzako anachemka na wewe unaelewa msaidie na umshauri kwa upendo lakini usitamani kuona akiharibikiwa hii ndiyo inaitwa hila.

Kama una hila utasikia tu kwa watu kwamba kunakumiliki kwa maana hautaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu, Biblia inasema “Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.”

Maisha matakatifu ni ya aina gani? Je! ni nani anayepaswa kuyaishi? Je! Yanafaida gani kwa anayeyaishi na yanahasara gani kwa kutokuyaishi?

Maisha Matakatifu ni maisha ya usafi wa moyo na mwenendo na usafi wa matendo pia, mtu ambaye anasema kuwa yeye ameokoka ni lazima mwenendo wake uoneshe kwamba ni mtakatifu, njia zako lazima ziwe ni njia za utakatifu.

Zaburi 16:3 “Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.” Kuishi maisha Matakatifu duniani siyo kwamba haiwezekani; inawezekana, kuna watu wanafika mahali wanahalalisha dhambi zao kwa kusema huu ni wokovu wa kisasa, mwana wa Mungu unapaswa kujua kuwa hakuna wokovu wa zamani wala wa kisasa, wokovu ni wokovu tu.

Wewe unayesema kuwa umeokoka unapaswa kuwa Mtakatifu mpaka Yesu atakaporudi. Ukiambiwa kuzini ni dhambi itabaki hivyo, Biblia inasema Mungu anachukia talaka basi itabaki kuwa hivyo, kusengenya ni dhambi itabaki kuwa hivyo, n.k, Usitafute maneno ya kujifariji dhambi ni dhambi, ukisema umeokoka basi hakikisha unakuwa mtakatifu mpaka Yesu atakaporudi.

Zaburi 24:5 “Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake”

Je! Unataka kuziona Baraka za Mungu ? Lazima uwe safi na ndipo utamiliki na kumuona Mungu katika maisha yako, Mungu anatamani akufurahie lakini anautaratibu wake ili uweze kumfurahia, kwa maana ukipokea kwa urahisi hautaona uthamani wa kile alichokupa na ndiyo maana Mungu anataka uheshimu kile alichokupa kwa kukilipia gharama.

Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” Lazima ujiwazie vizuri kwa maana wazo lako wewe ndilo litakalomfanya Mungu afanye kitu kwako, kwa maana utapokea sawa sawa na kile unachowaza, sasa kama ukiwaza mabaya basi hayomabaya ndiyo yatakuwa yakwako. Mungu hawezi kukupa kitu nje ya mawazo yako.

Mungu hawezi kufanya kitu nje ya kile unachowaza na kama kile unachokiwaza ni kitu chema basi Yeye atakupa.

Mara nyingi ibilisi anakuchokoza ili unene vibaya ili hayo yaweze kutimia kwako, mwana wa Mungu ni lazima uwe makini sana na kile unachonena na kuwaza kwa maana ndicho ambacho Mungu atafanya kwako, hata kama unaona ni kigumu sana kwako kwa Mungu hakuna lililo gumu, wewe sema na waza sawasawa na unavyotaka na Mungu atatimiza. Acha kuangalia mazingira.

Kwa nini haupokei mazuri? Ni kwa sababu unaangalia mazingira, unaangalia kule ulikotoka na ukajilinganisha, wewe uliyeokoka ni mwana wa Mungu hivyo ni lazima uwaze sawa sawa na Baba yako wa Mbinguni anavyokuwazia.

Mwana wa Mungu jifunze kuwaza sawa sawa na Mungu anavyokuwazia, waza mambo makubwa, andika ndoto yako juu ya kile unachotaka kitokee nacho kitatimia kwako.

©️ Mtume Mama Eliakunda Mwingira- Kanisa la Efatha