Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA JUMAPILI TAREHE 21/07/2024

Watch Now

Download

IBADA JUMAPILI TAREHE 21/07/2024

SOMO: KUPOKEA AHADI

1. Hatua ya kwanza kwa Ibrahimu ilikuwa ni kupokea mwana, Ibrahimu alifanya nini wakati alipokuwa anasubiri Baraka kutoka kwa Mungu? Tunaona ukarimu na moyo wa upendo aliyokuwa nao ambao ulipelekea kupokea majibu ya kile alichokitamani. Mwanzo 18:1-10 “…….. Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.”

Kuna uhusiano mkubwa kati ya Baraka unazotakiwa kumiliki na moyo wa upendo na ukarimu.

Kuna watu wanafunga hatima zao siyo kwa sababu hawaombi, la! Wanaomba, siyo kwa sababu hawafungi, la! Wanafunga lakini tatizo ni kujua muda wa kujiliwa kwao. Anaweza akaja mtu yeyote ukampuuza lakini huyo ndiye amebeba hatima yako; Biblia inasema “usiache kutenda vyema” kwa maana unaweza ukamkaribisha malaika pasipo wewe mwenyewe kujua. Inawezekana kuna watu na wewe usijue wamebeba nini kwa ajili yako, kuwa mkarimu kwa kila mmoja.

Wakati wa Mungu kukupeleka ulipokusudiwa kuna watu ambao wapo kwa ajili ya kubeba mzigo wako na kukupeleka kule ambapo Mungu amekukusudia; mwana wa Mungu kuwa mkarimu kwa kila mmoja maana haujui nani amebeba nini kwa ajili yako.

Unaweza kumdharau mtu kwa namna moja au nyingine lakini unaweza kukuta uharibifu ambao utatokea hapo kupitia huyo ni mkubwa.

Wakati wa kuiendea miliki yako ni wakati wa kuangalia sana tabia yako kwa maana wakati wa kujiliwa kwako unaweza usijue kama tabia yako ni mbaya.

HATUA MUHIMU SANA YA KUPOKEA URITHI WAKO;

Warumi 5:1-2 “Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.”

Maana ya kuhesabiwa haki ni nini? Ni kuondolewa kila aina ya shaka au baya, kuna watu wameokoka lakini hatua ya kujiona ndani kwamba amehesabiwa haki haipo, kwa sababu hatua ya kuipokea haki ni tofauti na kuisikia. Mungu anaangalia kama umeipokea hiyo haki. Tunaposema mwenye haki inamaana kuwa umekwisha kuipokea haki yaani imetangazwa kwako.

Kwa kupitia pendo Mungu alimtoa mwanaye ili kulipa gharama zetu, Mungu alimtwisha Yesu ghadhabu zetu zote, lengo la Mungu kufanya hivyo ni ili sisi tuhesabiwe haki. Tangazo hili lililotangazwa katika ulimwengu wa roho ni lazima lidhihirishwe kwa huyu ambaye ametangaziwa yaani mimi na wewe.

Mungu alitengeneza kitu kinaitwa Neema, neema siyo upendeleo wa Mungu tu bali ni uwezesho wa Mungu kukuwezesha wewe kufanya kile usichoweza kukifanya. Kwa kupitia neema, Mungu alitufanya sisi kuweza kuwa wenye haki.

Mungu aliitangaza Imani ifanye kazi pamoja na Neema, tunaupokea wokovu kwa neema kwa njia ya Imani, ukiitoa Imani Neema haina kazi, Neema ya Mungu haina kipimo lakini kulingana na Imani yako kwa Mungu basi utapokea Neema yake kwa kiasi hicho hicho.

IMANI KUTUPELEKA KUIPOKEA HAKI YETU

Warumi 5:2-3 “ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;”

Imani inaanza kwa kujidhihirisha kwa namna ambavyo hatupendi sana, inaweza kujidhihirisha kwa njia ya dhiki, wana wa Israel waliahidiwa kuingia katika nchi ya ahadi lakini baada ya kuvushwa katika bahari ya Sham kitu cha kwanza walichokutana nacho ni changamoto, ukiona changamoto zinakuja jua kuwa hapo ndipo imani yako inapamba moto.

Changamoto zinapojidhihirisha kwako zinaifunua Imani yako kwa maana Biblia inasema “ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi;” Ukiwa na Imani itakujengea uvumilivu ambao utakupa kupokea kile ambacho ulikuwa unakitazamia.

Zaburi 105:19 “Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya Bwana ilimjaribu.” Ukiona majaribu yanaongezeka kwako jua kuwa ni wakati wa kujiliwa na Mungu, kabla ya utumishi wa Yesu alipelekwa nyikani ili kujaribiwa, Wakati wana wa Israel wanaikaribia milki yao walijaribiwa jangwani na asilimia kubwa na wana wa Israel waliishia jangwani. Wakati wa ahadi ya Mungu kukujia neno linaweza kukujaribu.

Inapokuja saa ya kuinuliwa kwako na Mungu usiangalie mwanadamu anasema nini, bali wewe simama na Mungu wako na Mungu atakuonekania.

MAOMBI:

1. Muombe Bwana Yesu akuwezeshe kutimiliza safari yako ya Imani.

2. Kataa kila kizuizi mbele yako kiwe kinatokana na wewe mwenyewe, mazingira au familia uliyotoka kinachosababisha wewe ushindwe kutimiza ratiba yako ya ukamilifu.