Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Hakuna jambo gumu kwa Mungu.

Watch Now

Download

Hakuna jambo gumu kwa Mungu.

Hakuna kitu kilicho kigumu kwa Mungu, hata kama akili yako haiwezi kukubali lakini kwa Mungu inawezekana kwa maana kwa Mungu hakuna kisichowezekana, Mungu anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi, ukienda na akili hii mbele za Mungu inamaana kuwa umefungua mambo makubwa katika maisha yako.
Wewe amini kile Mungu anasema kwako namna atakavyotimiza sio kazi yako bali kazi yako wewe ni kuamini tu na Mungu atafanya.
Amini sasa na Mungu atafanya kwako.
Kama unamwamini Mungu kwa habari ya kipato, miujiza, uponyaji n.k wewe amini tu namna atakavyotimiza kwako sio kazi yako kazi yako ni uamini kuwa atafanya.
Esta 4:13-15 “ Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo? Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,”
Esta alikuwa ni mke wa mfalme (Malkia) alikuwa ana kila kitu alichokihitaji katika maisha yake lakini baada ya Mungu kusema naye juu ya Wayahudi hakuwa na amani mpaka Wayahudi wakawa salama. Inaweza kuwa Mungu amefungua mlango kwa ajili yako ili kuingia katika nyumba ya mtu mmoja ambaye hamjui wala kumuheshimu Mungu, au unafanya kazi katika kampuni ambayo mtu huyo hamjui Mungu au unaishi katikati ya watu ambao hawamjui Mungu, hiyo ni sababu au njia ya wewe kumuwakilisha Mungu hapo.
Lakini walokole wengi wamechagua kuridhika na kutokufanya chochote kile katika maisha hayo, Mungu amekuweka hapo ili umuwakilishe na kuwabadilisha hao watu, usiikumbatie amani yako pekeyako bali tamani watu wengine wapate kumjua Mungu kwa maana Mungu amekuchagua uwe hapo kwa kusudi maalumu nawe yakupasa kulitimiza hilo kusudi.
Mungu anasema usiitafute amani yako binafsi na ukaacha kinachowatokea wengine, kataa kushikilia amani yako pekeyako au amani ya familia yako tu, kijiji chako, majirani zako, kataa kuwa na amani juu ya magonjwa ya watu wengine, usiruhusu maisha yako yakakufanya uache kile ambacho wengine wanapitia bali simama mpaka umuone Mungu akifanya jambo katika maisha ya watu wengine.
Wakristo wengi changamoto yao ni kuwa wakiokoka na wakaipokea amani wanafurahia hiyo amani yao pekeyao hawajali maisha ya watu wengine, Mungu amekuponya, amekubariki, amekupa familia nzuri ili uweze kumuwakilisha Yeye na kuwafanya wengine wapate kumjua Yeye. Esta alikuwa na kila kitu lakini Mungu akasema naye kwa kupitia kinywa cha Mordekai ili aweze kuwasaidia wengine na akafanya kama alivyoagizwa.
Kila mmoja wetu mbele za Mungu anambadala wake, hicho ambacho Mungu amekupa kukifanya na ukakataa kukifanya wakati unaweza kukifanya Mungu atatafuta mtu mwingine afanye badala yako. Wakati wa Sauli Mungu alikuwa tayari na Daudi baada ya Sauli kwenda tofauti Daudi akashika madaraka badala ya Sauli, na Mungu akikubadilisha kwa sababu haujafanya wajibu au majukumu yako aliyokupa kuyafanya, sio wewe tu bali hata familia yako itateseka kwa ajili yako.
Usiache kufanya kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako, usiikumbatie amani yako peke yako na familia yako, usikiache kile ambacho unapaswa kukifanya, pigana mpaka kile ambacho Mungu ameweka ndani yako kitimie.
Kuna watu Mungu ameweka mzigo katika mioyo yao ya kumtumikia Mungu lakini wanakataa kufanya wakisema kuwa watu wengine watafanya, Mungu anaposema na wewe aliona unaweza kufanya na sio mtu mwingine na ndio maana akakupa wewe ufanye, wengine wanaingia hata kwenye maombi ili kumfanya Mungu abadilishe wito wao na kumtaka mtu mwingine afanye badala yako, Mungu alipokupa kufanya hakutaka umpe mtu mwingine bali ufanye wewe.
Usiwe na amani kabisa wakati unaona mambo hayako sawa, usiwe na amani mahali unapoishi wakati unaona wanaokuzunguka hawamjui Mungu, usiikumbatie amani yako kwa maana kama ukifanya hivyo Mungu atainua mtu mwingine asimame badala yako; kwa maana Mungu anapokuonyesha kitu cha kufanya tambua kuwa huo ni wakati wako wa kuinuka na kutimiza kile ambacho Mungu anataka ufanye. Acha kuwa na maisha ya amani mpaka kile ambacho Mungu amekuonyesha kitimie.