Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA JUMAPILI TAREHE 04/08/2024

Watch Now

Download

IBADA JUMAPILI TAREHE 04/08/2024

TAFAKALI SANA HAYA MWAKA HUU WA KUMILIKI

Huu ni mwaka wetu wa kumiliki, tunapozungumzia kumiliki ina maana kuwa eneo lako, nafasi yako, maana yake wewe ni nani, hivyo kumiliki kupo ili kukuonesha wewe ni nani.
Unapoelewa milki unayomiliki, hicho ndicho kitakupa utambulisho wako. Leo hii tunaona wezi wakiitwa wajanja, kwa nini? Kwa sababu hawana umiliki.
Mmiliki hawezi kuiba bali yeye anawakamata wezi kwa maana yeye ni mmiliki, yeyote unayemuona anaiba jua kuwa yeye si mmiliki, leo hii unaweza kuona hata viongozi wetu wakiiba, sielewi; je! Wanajitambua wao ni kina nani? Ni kwa sababu hawaelewi maana ya umiliki na ndiyo maana wanafanya hivyo.
Mwaka huu ni mwaka wetu wa kumiliki mali, mmiliki hawezi kuiba, mmiliki anachukua kile ambacho ni chake, na ndiyo maana tunatakiwa kurejesha vyote vilivyo vya kwetu, kama haujui ya kuwa wewe ni mmiliki utakufa hapa ulimwenguni ukiwa maskini na haujamiliki chochote.
Tumepewa mwaka huu kuwa mwaka wetu wa kumiliki, Maana yake ni kuwa kila mmoja wetu arudi katika ufahamu wake ili awe mmiliki.
ELEWA VIZURI KUHUSU KILE UNACHOTAKA KUMILIKI
Unawezaje kuwa mmiliki kama haujui kile unachotakiwa kumiliki? Lazima uelewe unamiliki nini ili uweze kumiliki.
1 Yohana 4:17 “ Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.” Sisi tupo katika utimilifu kupitia pendo, kwa nini kupitia Pendo? Kwa sababu tumeumbwa katika pendo na siyo chuki, Mungu alitupenda.
• Biblia inasema; “ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu;” Hii inamaana kuwa siku moja mahali fulani kutakuwa na hukumu, lakini hata sasa, jaribu la hukumu bado linaendelea, na ndiyo maana unaweza kuona kuna magonjwa, kushindwa, kutengana, talaka na kila aina ya maumivu, hii ni jaribio la hukumu ili kukufanya wewe uweze kugeuka na uweze kukwepa hukumu ya milele, hivyo inategemea wewe, je unaelewa nini kuhusu majaribu?
• Biblia inasema “kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.” Siyo mbinguni, bali ulimwenguni na siyo kesho bali ni sasa, kwamba unakubali au unakataa ila huu ndiyo ukweli. Namna unavyopokea ndivyo utakavyokuwa na utakavyokwepa hukumu ya milele. Unatakiwa uelewe leo ili uweze kukwepa leo hukumu ya milele kabla haijaja.
© Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha Mwenge.
 
KAMA KRISTO ALIVYO NDIVYO TULIVYO HAPA DUNIANI.
1 Yohana 4:17 “ Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.”
Mungu akasema “kama yeye alivyo ndivyo na sisi tulivyo ulimwenguni humu” wakati upi utakuwa kama Yeye? Ni sasa, ukielewa jambo hili anaongelea kwa habari ya sura yake (kwa maana yeye alituumba kwa sura na mfano wake), hapa ndipo sura ya Mungu ilipo kama alivyo ndivyo tulivyo, ukimuona Mungu namna alivyo basi ndivyo tulivyo sisi.
Ukiweza kumuelezea Mungu ndivyo unaweza kuielezea sura yake, kwa nini Mungu alisema hivyo? Kwa sababu alitaka mtu afanane naye, Mungu akasema “na tumfanye mtu kwa sura na mfano wetu” hii inamaana kuwa Mungu alitaka mtu afanane naye. Mungu alitaka sisi wanadamu tuwe kama Yeye hapa duniani.
Unapotembea huku duniani hauwezi kuona ukuu katika maisha yako mpaka uelewe kile Mungu anataka uelewe, Mungu alitaka mimi na wewe tuwe kama Yeye huku duniani.
Sijaelewa kwa nini watu wanasema kuwa wao ni mali ya Mungu lakini wanamilikiwa na mapepo, je unajitambua kweli wewe? Ni sawa na mke wa mtu halafu analala na mwanaume mwingine, je! Huyu mtu anajitambua kweli. Mwana wa Mungu jitambue, Mungu alitaka sisi tuwe hapa duniani kwa niaba yake, alitaka tuwe mabalozi, wapatanishi, amiri jeshi tukiamuru vitu vitokee na kusababisha vitu vitembee.
Leo hii unaweza kumuona mtu ameokoka lakini anaanza kulia na kusema “nahitaji msaada, naomba mnisaidie mimi kwa sababu sijaolewa ndiyo maana nashindwa hili au lile” je unajitambua kweli wewe? Kwa sababu haujaolewa ndiyo hauwezi kufanya mambo makubwa, huwezi kujenga nyumba na kununua gari? Sio kweli, Mungu alikuumba wewe uwe mmiliki hata kama hujaolewa.
Mungu alitaka sisi tuwe wamiliki tukimiliki hapa ulimwenguni na siyo ibilisi.
Mungu anataka sisi tuwe watendaji kwa maana sisi ni wamiliki wa ulimwengu wote na alitukabidhi sisi na si ibilisi, Mungu alitaka tuwe watendaji, watu wengi leo hii ni omba omba wakiomba huku na kule na wakisema “unajua mimi sina kitu,” lazima uwe mtendaji, fanya jambo kwa ajili ya Mungu na kwa ajili yako mwenyewe na siyo unazurura zurura tu, Mungu ametuumba tuwe sura yake ili tutawale hapa ulimwenguni. Ametuumba ili tuwe wanawe na tumiliki, jitambue na chukua nafasi yako ili uweze kumiliki.
MUNGU ANACHOTAKA TUFANYE
Mungu alitupa sura yake, kwa nini? Ili tuwe kama yeye yaani wawakilishi wake hapa ulimwenguni.
Alitaka tuwajibike kwa kila tendo linalotokea hapa chini ya jua, hatuhitaji kumlaumu ibilisi au wanaotenda maovu bali tunatakiwa tujilaumu sisi kwanza kwa maana Mungu alitupa huu umiliki hivyo tunapaswa kumiliki na siyo kumuachia ibilisi. Chochote kilichoumbwa na Mungu tunatakiwa tukimiliki. Tunatakiwa tuwajibike kwa habari ya uumbaji wa Mungu, Mungu hatawauliza wasiyo haki bali atakuuliza wewe mwenye haki, mwabuduo.
Sura ya Mungu nini? Ndiyo hatuwezi kumuona wala kumgusa lakini tunaweza kumfahamu na kujua sura yake kupitia kile alichosema, Mungu alisema nini?
• Mungu ni muumbaji, Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Kama Mungu aliumba mbingu na nchi yeye ni muumbaji, aliumba nini? Mbingu na nchi.
• Mungu ni mmiliki ana miliki nini? Mbingu na nchi. Mithali 8:22-30 “Bwana alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale. Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji. Kabla milima haijawekwa imara, Kabla ya vilima nalizaliwa. Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde Wala chanzo cha mavumbi ya dunia, Yohana 1:1-3 na Yohana 15:5.
Hapa ulimwenguni tunaona uharibifu kila mahali kwa maana watu hawana ufahamu juu ya Mungu, chochote unachokifanya lazima kiongozane na Roho wa Mungu na Roho wa uumbaji. Unapopika, unapokula na chochote ufanyacho lazima uelewe kuwa hakiwezi kukamilika pasipo Roho ya ukamilifu, ili uweze kufanya kitu na kikawa na muendelezo lazima uwe na Roho ya uumbaji pasipo na Roho ya uumbaji kamwe hauwezi kuona muendelezo.
Tunafanya mambo kwa njia salama zaidi kwa sababau ya Roho ya uumbaji, na tunafanya vitu kwa viwango ni kwa sababu ya Roho ya uumbaji, hauwezi kufanya vitu kwa kiwango kama hauna Roho ya uumbaji.
Tunafanya vitu vinavyodumu kwa sababu ya Roho ya uumbaji, unapoanzisha duka na kama unataka hilo duka lako likuwe na kukaa miaka kwa miaka unapaswa kuwa na Roho ya uumbaji ukiumba duka lako kila siku. Roho ya uumbaji ipo ili kukusaidia kufanya vitu vya kudumu na vyenye kustahimili.