Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ibada maalumu mkesha wa kuvuka 2023/2024

Watch Now

Download

Ibada maalumu mkesha wa kuvuka 2023/2024

Zaburi 121:1-8 “Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.”
Huu ni urejesho wa maisha yetu, namna Mungu anavyotenda kazi itategemea ni kwa jinsi gani unawasiliana naye, unahusiana vipi na Yeye na unamjuaje, je unamjua tu kama muumbaji au unamjua kama ni mlinzi wa maisha yako?
Mara zote mimi nimetambua kuwa siwezi lolote pasipo Yeye, kwa maana Yeye ndiye aliyenifanya mimi kupanda milima na kufika salama. Yeye ndiye aliyekukomboa kutoka katika uovu, Yeye ndiye aliyeharibu nguvu za giza katika maisha yako, Yeye ndiye aliyekutoa mavumbini na kusababisha leo hii unang’aa sio kwa nguvu zako, upo hai leo sio kwamba wewe ni mjanja mno bali ni kwa rehema za Mungu tu katika maisha yako.
Yeye ndiye uvuli wetu, mtetezi wetu, Yeye ndiye mkuu wetu, ndiye asili ya utumishi wetu, kazi hii pasipo Yeye sisi hatuwezi lolote. Kuanzia leo salimisha maisha yako kwake na mruhusu Mungu akutoe hapo ulipokaa kwa muda mrefu hapo ambapo umekwamia na kutafuta tafuta, muite Yeye kama Petro alipokuwa anazama, alimuita Yesu na kusema “Yesu niokoe nisizame”. Ukimuita Yeye katika maisha yako kamwe hautaangamia bali atakuokoa na wewe utakuwa salama.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MWAKA HUU 2024
Kuanzia leo Mungu hatakunyima vitamanikavyo, utakula kile moyo wako unachotamani, hii inamaana kuwa hautakula kwa sababu ndio kilichopo, la! Bali utakula kile moyo wako unachotaka.
Kuanzia leo ugonjwa wowote unaotokana na chakula, maji au matunda hautakuwa juu yako maana Bwana atakubariki. Unachokula na unachokunywa hakitasababisha magonjwa wala maumivu kwako. Mungu ataponya chakula unachokula na maji unayokunywa kwa Jina la Bwana.
Maadamu umekubali kuijenga nyumba ya Bwana Mungu atakutafutia nyumba nzuri maana umemfanyia Bwana makao mazuri aweze kuheshimiwa katika dunia hii, hivyo Mungu anakwenda kulitukuza jina lako nawe utakuwa na makazi mazuri.
Kuanzia leo kwako ni makao salama, adui hataruhusiwa kuingia ndani ya nyumba yako, mchawi hata kuloga wewe wala kazi ya mikono yako ibilisi hataigusa.
Shika haya ninenayo leo katika siku hii ya kwanza ya mwaka huu maana ndiyo yatakuwa yako katika mwaka huu 2024.
Mungu anakwenda kuzaa mambo mapya katika maisha yako hivyo utakwenda kung’aa. Leo ni siku mpya ya kugeuka kwako, ni siku ya kung’aa kwako, ni siku ambayo Mungu amekupa kutiisha adui zako.
Ibada yako ya mwaka huu haitakuwa ya kawaida, utakuja ibadani ukiwa umechoshwa na mambo lakini utarudi nyumbani ukiwa huru katika hayo mambo. Utakuja ibadani ukiwa na Imani unataka jambo fulani litokee kwako na litatokea, hautakuja na kulia bali kwa wewe kutokea tu kanisani adui ambaye alikuwa anakukandamiza atakuachia pasipo wewe kumwambia akuachie kwa sababu nguvu ya Roho Mtakatifu ambayo itafunika mahali hapa itasababisha mambo hayo kutokea kwako na ibilisi hatakuwa na nguvu tena kwako.
Magonjwa ambayo madaktari wamekwambia kuwa unapaswa kufanyiwa upasuaji kamwe hautafanyiwa upasuaji kwa maana Bwana wangu ni tabibu mkuu atakufanyia upasuaji Yeye mwenyewe. Ili hayo yote yatokee kwako wewe unapaswa kuwa mwaminifu katika kile ambacho Mungu anachokisema, Mungu akisema fanya hiki kupitia watumishi wake wewe fanya usisubiri mpaka Yeye ashuke na kukwambia kitu ndipo ufanye kwa maana ametuweka hapa duniani sisi Watumishi wake ili aweze kusema na wewe hivyo unapaswa kutii.
Muda wa huzuni kwako UMEKWISHA.
Mwaka 2024 ni Mwaka wa KUMILIKI VYA KWAKO
Kumbu kumbu la Torati 1:21 “Tazama, Bwana, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike.”
Kila kilicho chema ni sehemu ya fungu lako kwa sababu Kristo alikifia kwa hiyo ni cha kwako.
Yakobo 1:17 “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.”
Mungu hawezi kukataa wewe kuwa na kila kilicho chema, Mungu yupo kukuhakikishia kwamba utakuwa nacho. Mungu tayari amefanya maamuzi kwako kwamba ukapate kila kilicho chema.
Chochote kilicho chema unaweza kukitaja maana umepewa, chochote kilicho chema ambacho kimeinuliwa kinatoka juu (Mbinguni), unastahili kukipokea, chochote ambacho kipo chini ambacho hakijakidhi viwango na hakina thamani ni kitu cha duniani lakini chochote kilicho kizuri na kina thamani maana yake kinatoka juu ni pamoja na wewe kwa maana wewe ni wa thamani. Chanzo chako ni juu. Chochote chenye thamani kinatoka juu. Kila zawadi njema na zawadi kamili inatoka juu
Siku ya kwanza Mungu alipokwenda kwa Waebrania na alipotaka kuwatoa alitaka kuwaonesha ni jinsi gani alivyo mzuri, aliwaandalia chakula wakala; hivyo waliona ni jinsi gani Mungu alivyo mzuri. Tumeanza mwaka huu kwa tafrija ili muone ni jinsi gani Mungu ni mzuri, Yeye ametupa chakula ili kutuamuru sisi twende tukamiliki milki yetu.
Mwanangu huu ni wakati wako wa Kumiliki milki Yako.
Mungu ametupa chakula ili tuweze kutembea na tuweze kumiliki milki yetu. Chochote kilicho chema na kizuri kinatoka juu ingawa bado haujakishika lakini ni cha kwako, kama nyumba ni nzuri basi ni yako, kama shamba ni zuri basi ni lako, kama mume au mke ni mzuri basi ni wa kwako, kama watoto ni wazuri basi ni wa kwako, kama nguo ni nzuri basi ni za kwako, kama gari, fedha ni nzuri basi ni za kwako. Chochote kilicho kizuri ni stahiki yako.
Weka hili katika akili yako; Chochote kilicho kizuri ni chako kwa sababu Bwana wako Yesu alikilipia ili wewe uwe nacho.
Kuanzia leo kama mtu akikujia na kukuambia njoo ununue hii nyumba usimwambie sina hela bali mwambie sio sasa, maana ukisema sina hela itakuwa kama ulivyosema.
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”
Wewe haujalaaniwa bali umebarikiwa ndani ya Kristo Yesu, Yeye alifanya mambo hayo kwa ajili yako. Chochote Yesu alichokifanya ni chako. Baraka yako imehakikishwa na kutiwa muhuri, zimekabidhiwa kwako, ni zako na huu utakuwa ni wakati wako wa kwenda kuchukua kilicho chako.
Mwaka huu UTAMILIKI chochote Moyo wako unachotamani na kitakuwa cha kwako. Tamka kile unachotaka kumiliki mbele za Bwana.
Anayelaaniwa, aliyekandamizwa au mgonjwa hawezi kumiliki bali yeye aliyeponywa, aliye mshindi na aliyebarikiwa ndiye anayeweza kumiliki. Hakuna mwenye mateso ataondoka nayo mahali hapa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareth.
Hata kama walikufungia ukiwa nyumbani, walichukua jina lako au chochote walichofanya na kukufunga kifungo cha kipepo au cha kichawi leo, moto wa Roho Mtakatifu ukakiteketeze hicho kifungo na minyororo ivunjike kwa jina la Yesu.
Msiba wa JANA hauwezi kuwa msiba wa leo. Mateso, maumivu, ugonjwa, talaka na magomvi ya JANA hayawezi kuwa ya leo; NENDA KASHANGILIE USHINDI WAKO.