Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI 21/01/2024

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI 21/01/2024

MCHUNGAJI VICTOR GASPER MALAMLA KUTOKA KANISA LA EFATHA MWANZA
Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba akiwa ameshaweka kila hitaji lake tayari, ikimaanisha kuwa kila kitu ambacho mwanadamu alihitaji tayari Mungu alishakiumba, hii inamaana kuwa kabla ya mtu kuumbwa Mungu alianza kutengeneza vitu ambavyo huyo mtu alihitaji, alipoumba mti ndani ya mti aliweka kitanda, masofa, mwiko na kila kitu ambacho mwanadamu angeweza kutumia kinachotokana na mti.
Mungu alimuumba mtu ili aweze kumiliki vile alivyoviumba. Alipoumba ulimwengu tayari alikwisha kuumba ndege, magari, maghorofa na kila kitu ambacho anajua mwanadamu anaweza kukitumia, hata kabla havijagunduliwa. Ndipo Mungu akamuumba mtu ili aweze kumiliki vile ambavyo ameviumba tayari.
Mungu alimuweka mwanadamu katika bustani ya Edeni ambapo aliweka kila kitu ndani yake, lakini dhambi ilipoingia mwanadamu aliondolewa kwenye bustani ya Edeni; aliondolewa kwenye umiliki wake akaanza kula kwa jasho na kupambana; lakini atukuzwe Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alimtoa mwanaye wa pekee ili wale wamwaminio waweze kurejeshwa tena Edeni ambapo kuna kila kitu.
Ukishamwamini Bwana wa mabwana Mfalme wa wafalme aliyeshinda kifo na mauti unapewa kumiliki na kuushinda ulimwengu na kila aliyezaliwa mara ya pili (aliyeokoka) ameushinda ulimwengu na amefanyika kuwa uzao wa Yesu. 1 Yohana 5:4 “ Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.”
Ukishazaliwa mara ya pili wewe sio uzao wa baba yako au ukoo wako au kabila lako bali wewe ni wa uzao wa Yesu na kwa Yesu hakuna kushindwa ndani yake. Mtu anapozaliwa mara ya pili anaingizwa kunako nuru; Wakolosai 1:13-16 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi……….”
Baada ya dhambi ndipo mwanadamu alitolewa katika bustani ya Edeni na tulipotoka katika Bustani ya Edeni tulikuwa gizani lakini ukiupokea Wokovu unahamishwa kutoka gizani na kuingizwa katika nuru. Aliyezaliwa mara ya pili ( aliyeokoka) hapaswi kuwa maskini kwa sababu uzao wa Yesu unakaa ndani yake.
Je! Wewe umeokoka? Kama jibu ni ndio ni marufuku kuwa maskini.
Ukishazaliwa mara ya pili (ukiokoka) kukubali kuwa maskini au kuwa tajiri ni maamuzi yako, hii haiendani na elimu yako, usomi wako wala kujulikana kwako bali ni maamuzi.
Kinachosababisha watu wengi waliookoka kuwa maskini na kuwa na uhitaji wa kifedha ni ufahamu wao, matatizo yote ya kifedha yanatokana na ufahamu wako,
Je! Wewe unajionaje? Sahau namna ambavyo watu wengine wanavyokuona, je wewe uanjionaje? Kama ukijiona kuwa wewe ni kati ya maskini basi utadhihirisha umaskini wako, lakini ukijiona kuwa wewe ni kati ya waliobarikiwa kifedha basi ndivyo utakavyokuwa. Je wewe unajionaje?
Mithali 23:7 “ Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.”
Mtoto mdogo anajua kuwa baba na mama yake wanaweza vyote hajui kama kunakushindwa. Mtoto anapoona ndege inapita anaweza kumwambia baba nikiwa mkubwa utaninunulia ndege? Jibu la baba utasikia “wewe mtoto acha uchuro” lakini sio uchuro bali anaongea kile anachokiamini. Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ndani yake hakuweka umaskini, hata kama kwenu kuna laana, uchawi au kutambika, Mungu alishakubariki wewe, lakini kinachofanya hiyo laana au uchawi uonekane unafanya kazi ni akili yako. Hivyo ulivyo ni matunda ya kile ulichopewa.
Laana inapowekwa iwe ni kwenye familia au ukoo inawekewa utaratibu wa kudhihirika, elimu haiwezi kukutoa kwenye hayo, unaweza kusoma sana lakini kama elimu yako haijachanganyikana na nguvu ya Mungu utakufa ukiwa maskini. Tumelelewa na wazazi ambao akili zao zilishabadilishwa na ufalme unaowamiliki yaani ufalme wa giza, wewe ulipozaliwa ukiwaza jambo kubwa na ukamuhadithia baba yako utasikia anakwambia “mwanangu hayo mambo sisi hatuyawezi, sisi hatujawahi kujenga maghorofa jenga tu hata nyumba ya mgongo wa tembo maana kuna wengine hata hiyo hawana” Ile akili ambayo tumelishwa ndio leo inasumbua kanisa. Ili utembee katika uchumi wa Ufalme wa Mungu lazima akili yako ibadilishwe, vinginevyo utafunga na kuomba sana na hautakaa ufike popote.
Akili ni funguo ya kiroho inaweza kukuingiza mahali popote ulipopaona au unapopataka. Mfano: kama akili yako haioni kitu kilichobora kamwe hautaweza kukipata, kwa maana mwili hauwezi kupata kitu ambacho akili yako haioni.
Chochote unachotaka kumiliki lazima kwanza akili yako ione, ona ile picha tazama ile picha na uitafakari ikishakaa ndani yako mwili unafata wenyewe.
Ukombozi wa akili, ni muhimu sana ndani ya kanisa ili kutembea katika uchumi wa kiungu.
Ili udhihirisho wa kumiliki uchumi wa kifalme utembee na wewe lazima uzingatie haya:
Nguvu ya upendo: hakikisha akili yako haiwazi mabaya, kushindwa wala usimchukie mtu yoyote. Kitu kinachotesa watu wengi na kuwafanya washindwe kufikia ukuu wao ni chuki, ukimuona mwenzako amefanikiwa wewe unapaswa kufurahi na sio kumchukia. Kumchukia mtu aliyefanikiwa kuliko wewe unajizuia kufika kule alipofika yeye. Ukifurahi na anayefurahi na wewe neema ile ile ya yule aliyefurahi unaipata, hauwezi kufanikiwa kwa kumshusha aliye juu bali utafanikiwa na kustawi kwa kumfurahia aliye juu ili na wewe uvutwe juu.
• Hauwezi kufanikiwa kwa hila bali mara zote upendo ni nguvu ya utajiri itakayokufikisha kwenye mafanikio.
Mabadiliko ya akili yako ni ya muhimu sana, acha kuwaza mabaya ya aina yoyote, iwe ni ya kweli au siyo ya kweli, chochote hasi (negative) unachokiwaza kinaua nguvu ya udhihirisho wa jambo ambalo Mungu anataka kufanya kwako hivyo acha mara moja.
Kumiliki ni vita, baada ya Musa kufa Mungu alimwambia Yoshua, mbele yako kuna wafalme watano ukawapie ili upate kumiliki.
TANGAZO:
Mfalme yeyote anayezuia umiliki wako leo anaanguka kwa Jina la Yesu; atake au asitake, iwe ni kazini kwako, kwenye elimu yako, ndoa yako, biashara zako anaanguka kwa Jina la Yesu; lazima aanguke ili umiliki, jiandae kumiliki.
Kila kiambaza au kizuizi kilichozuia kazi, biashara au ndoa yako kwa muda mrefu, natangaza hicho kizuizi au kiambaza leo kimevunjika kwa Jina la Yesu. Kama kuna ukuta ulikuwa unakuzuia usiende mbele huo ukuta leo umeanguka kwa Jina la Yesu, chochote kilichokuwa kinazuia mtembeo wako wa kumiliki leo kimeondolewa kwako kwa Jina la Yesu. Nguvu yoyote iliyokuwa imezuia mtembeo wa kifedha kwako, kwenye ndoa, biashara, kazini kwenye kampuni yako hicho kizuizi kimeondolewa kwa Jina la Yesu.
UKIRI:
Kuanzia sasa nachukua milki yangu, kila milki yangu iliyo haki yangu saa hii kwa mamlaka ya Jina la Yesu naichukua, nachukua kazi yangu, ndoa yangu, afya yangu, uchumi wangu vyote nachukua kwa Jina la Yesu.