Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI FEBRUARI 11/2024

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI FEBRUARI 11/2024

SAFARI YA WANA WA ISRAELI.
Katika Safari ya Wana wa Israeli wakati wanatoka Misri walitoka wengi sana lakini waliofanikiwa kuingia Kaanani ni wawili tu ambaye ni Joshua na Kaleb, lakini makamanda wengine wote walifia jangwani. Hivi ndivyo ilivyo katika maisha haya ya Imani, unapoanza kuokoka kunakuwa na mchecheto mkubwa lakini baada ya misukosuko kidogo kutokea unatoka kwenye mstari, Mungu akusaidie usitoke kwenye mstari, kwa maana gharama ya kurejea tena kwenye mstari ni kubwa.
Unapaswa kutambua kuwa ukiona vituko vinakuwa vingi au magumu yanakuwa mengi jua kuwa umekaribia sana pale unapokwenda, hivyo vumilia. Unapaswa kutambua kuwa gharama ya kurudi nyuma na kwenda mbele ni ile ile, ukiendelea kuna mema ya milele lakini ukirudi nyuma kuna janga la milele hivyo maamuzi ni yako.
HUU NI MWAKA WA KUMILIKI.
Huu ni Mwaka wa Kumiliki kwa maana hiyo ni Mwaka wa kuchukua Fungu lako.
Mathayo 9:35-38 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina………”
Kufundisha ni nini na Kuhubiri ni nini? Kufundisha sio Kuhubiri;
1. Kuhubiri- Kuhubiri maana yake watu wapate taarifa kuhusu Wokovu na Msamaha wao, wapate kujua toba na watu waweze Kuzaliwa Mara ya Pili (Kuokoka), wapate kumjua Yesu Kristo na kumuhusu Roho Mtakatifu, haya ndiyo Mahubiri.
• Tunahubiri kusababisha watu waamini na Waokolewe, Maajabu na Miujiza itokee. Kuhubiri ni kama kushuhudia, tunashuhudia kile Yesu amefanya katika Maisha yetu, ina maana kuwa unaposhuhudia unahubiri habari za Yesu. Mwamini yeyote lazima ahubiri kwa maana kama hauhubiri au haushuhudii hautapata chochote katika Ufalme wa Mungu na utafika Mbinguni pasipo matunda. Usitembee huku duniani ukiwa umeokoka pasipo kuwa na Ushuhuda, hakikisha unashuhudia kwa maana kwa namna unavyoshuhudia ndivyo utawafanya wengine wapate kuja kwa Mungu (Kuokoka). Hakikisha unashuhudia popote ulipo, Kazini kwako, Shuleni kwako na popote utakapokuwa, wewe ni Mwamini hakikisha unashuhudia.
2. Kufundisha: Kufundisha ni kwa ajili ya wale ambao tayari wameokoka, unawapa Ufahamu ni namna gani wataenenda katika Nguvu, namna ya kumshinda ibilisi na wapate kujua namna ya kusababisha Imani yao ipate kudhihirika. Hakuna atakaye kuamini au atakayejua kuwa unaye Mungu kama hujadhihirisha Imani yako. Ibilisi na wachawi hawatakuogopa, miujiza haitatokea, maisha yako hayawezi kubadilika ni mpaka ufanyie Kazi kile unachokijua, hivyo fundisho ni kwa ajili yako wewe kama Mwamini. Hakikisha unaposema umeokoka kuna jambo linatokea kwako kwa maana Wokovu ni badiliko la kweli na sio maneno.
Katika dunia hii hauwezi Kuvuna pasipo Kupanda, ni lazima upande ndipo uvune lakini hapa Yesu hakuwa anazingatia kupanda bali Mavuno; ndipo akasema;
Mathayo 9:37-38 “Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”
Hii ina maana kuwa wapandaji ni wengi lakini Wavunaji ni wachache; hauwezi kuvuna kama haujapanda; Vivyo hivyo hauwezi kumiliki ulichokipanda bali kile ulichokivuna. Mungu akasema “humpa mbegu mpanzi lakini humpa mkate mwenye njaa” Je! Mbegu ni yako? Hapana bali anayekupa mbegu ni Mungu, anakupa mbegu ili nini? Ili uweze Kupanda, nini kilicho chako sasa? Ni Mavuno.
Mungu akikuona una haja ya kufanya kitu ili upate Yeye analeta usaidizi wa wewe kufanya ili uweze kufaidi kile kitakachotokea. Mbegu ni nini? Haina maana ya mbegu ya mahindi bali ya chochote unachotaka kupanda yaani kupata katika Maisha yako. Ni chochote unachohitaji msaada. “Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa Mavuno, apeleke watenda kazi katika Mavuno yake.”
Hapa Yesu alizingatia mambo matatu:-
1. Mavuno ni mengi.
2. Wavunaji ni wachache.
3. Mwombeni Bwana wa Mavuno ili Wavunaji wawe wengi. Hivyo ni ombi letu sasa kuomba ili tuwe wamoja kati ya wale Wavunaji (yaani wale watakaopokea kutoka Mungu).
UNAVUNAJE?
Mathayo 13:1-9 “……… Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda. Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila; nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga; nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini. Mwenye masikio na asikie.” Kuna mbegu nyingine japokuwa zilipandwa lakini mpanzi hakuvuna.
Kuna makundi ya maeneo manne ya mbegu zilizopandwa, Je! Wewe unataka kuwa wapi?
1. Mbegu nyingine zilianguka karibu na njia na ndege wakaja wakala, Je wewe ni mara ngapi mbegu zako zilichukuliwa? Ulianzisha jambo lakini ibilisi akaja akachukua na kula.
2. Nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina; na jua lilipozuka ziliungua.
3. Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga.
4. Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini Je unataka kuvuna kwa kiasi gani? Mwaka huu zingatia sana mavuno na sio kupanda. Matarajio yatakupa kujua ni aina gani ya mbegu unayotaka kupanda kulingana na kile unachoelewa.
Ukitaka uvune mazao ya kukupeleka mbali angalia ni zao gani unapanda, ukipanda mchicha kila baada ya miezi kadhaa unapanda tena lakini ukipanda mchungwa au muembe mpaka vitukuu Vitavuna.
Angalia unataka Kuvuna nini na sio unapanda nini. Mawazo yako yasiwe kwenye unacholima au kupanda bali yawe katika kile unachokwenda Kuvuna.
Luka 10:2 “Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.” Uzingativu wa Yesu ulikuwa katika Mavuno, uzingativu wako unapaswa kuwa katika Mavuno; kwa nini? Kwa sababu ukiwa katika Mavuno utayafikia kwa sababu usiku na mchana utazingatia kulinda yale Mavuno yako. Lakini kama uzingativu wako ni kwenye kupanda basi utaishia kupanda kando kando ya njia, kwenye miamba au njiani na kamwe hautavuna.
Lakini kama uzingativu wako upo katika Mavuno kamwe hautapanda kwenye ardhi ambayo itameza mbegu yako bali utazingatia mahali palipo na udongo mzuri. Ni wapi penye udongo mzuri? Ni pale Uwepo wa Mungu ulipo.
Mara zote utazingatia haya:
1. Mahali penye uwepo wa MUNGU.
2. Kuwasikiliza Watumishi wa Mungu wenye uwepo wa Mungu katika maisha yao ambao wamefanikiwa ki maisha na wanatembea na Utukufu wa Mungu.
3. Wewe mwenyewe, Je upo chini ya Utukufu wa Mungu? Unatembea kwenye Uwepo wa Mungu? Je! Tabia yako inampendeza Mungu, mavuno yatakuja kulingana na jinsi ulivyo kwa sababu wewe mwenyewe ni mbegu ya Mungu. Mathayo 13:9 “ Mwenye masikio na asikie.”
Anaitwa Prisca John, anamshukuru Mungu kwa kuwaokoa Watoto wake katika nguvu za giza; Watoto wake walikuwa wakitumikishwa kichawi kwa muda wa miaka 6 bila yeye kujua. Siku moja usiku alipokuwa amelala na Watoto wake wakati mume wake amesafiri alishangaa alipoamka akawa hawaoni kitandani ndipo alipoamka na kuanza kuwatafuta. Katika harakati za kuwatafuta ndipo akamkuta Mtoto mmoja sebuleni na mwingine kwenye kibaraza cha nje ya nyumba ndani ya beseni la maji machafu.
Priska anasema alishangaa sana maana lile halikuwa ni tukio la kawaida. Ndipo akaamua kumtafuta mume wake na kumwambia kilichotokea; lakini pia alikumbuka kuna Jirani yake ni Mwana Efatha alimshuhudia habari za Yesu lakini hakumsikiliza hapo mwanzo ndipo akamfuata, Priska akaamua kuja Kanisani na alipofika Watoto wake wote walifunguliwa, na ndipo wakaongea yote yaliyokuwa yanawatokea. Baada ya maombi Priska akaamua Kuokoka.
Lakini pia Priska anasema anamshukuru sana Mungu kwa kumsomeshea Watoto wake, kwani alitamani sana Watoto wake wasome shule nzuri alipomwambia mume wake akamwambia hatutaweza kuwasomesha Watoto wetu huko kwa maana hatuna fedha za kutosha, wakati huo yeye alikuwa anafanya kazi za ndani na kulipwa mshahara wa laki 2 tu 200,000/= kwa mwezi; akaamua Kwenda kutafuta shule na akapata shule nzuri ya English medium ambayo ada yake ni shilingi milioni moja, ndipo alikwenda kwa boss wake na kumuomba amkopeshe kiasi cha shilingi milioni moja ili aweze kumpeleka mtoto wake shule, boss wake akamwambia utawezaje wakati mshahara wake ni mdogo akamwambia utakata mshahara wote mpaka nitakapomaliza deni langu.
Baada ya Priska kufanikiwa kumpeleka mtoto wake shule na alipofika darasa la nne ndipo akaja boss wake wa zamani ambaye aliwahi kumfanyia kazi na hakumlipa pesa hivyo alikuja kwa lengo la kumlipa, baada ya kusikia kuwa Priska anasomesha ndipo akamwambia atamsomeshea mtoto wake mpaka atakapomaliza darasa la saba lakini cha ajabu baada ya mtoto wake kumaliza darasa la saba na kufaulu vizuri yule boss akamlipia ada ya miaka yote minne sekondari na mtoto wake mdogo pia analipiwa ada.
Priska anamshukuru sana MUNGU kwa Matendo yake MAKUU katika Maisha yake na kwa Familia yake pia.