Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI MEI 19 2024

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI MEI 19 2024

SOMO: MAZINGIRA YANAYOHUSU KUMILIKI KWETU NA TARATIBU ZAKE.
Katika ukamilifu wa safari ya ukombozi unakamilishwa na kumiliki, safari yenyewe ya kumiliki ilipoanza mwanadamu alipoteza kuelewa asili ya kumiliki kwake.
Wana wa Israel walipokuwa Misri ulifika wakati walijikuta katika utumwa lakini hawakuingia pale kama watumwa bali Yakobo na wanae waliingia wakiwa huru kabisa. Kuna mambo mawili yalifanyika wakati huo; Wana wa Israeli walijikuta watumwa na milki yao ilichukuliwa.
Wewe mwana wa Mungu Saa ambayo utagundua kuwa wewe upo utumwani jua kuwa hata milki yako imekwisha kuchukuliwa, safari ya wana wa Israel ilikuwa ni kivuli cha sisi leo hii kuweza kufikia umiliki wetu.
Kwanza walianza na kilio cha kutaka ukombozi, lakini Mungu alipoanza mchakato wa kuwatoa utumwani alikuja na mkakati pia wa kuwarejesha kwenye umiliki wao japo hicho kilikuwa sio kilio chao.
Mtu yeyote aliye katika eneo la kukandamizwa kilio chake ni kutoka na kuwa huru lakini mpango wa Mungu ni mkubwa kuliko huo kwa maana mpango wa Mungu ni kukufikisha katika umiliki wako
Waefeso 1:13-14 “Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.”
Hapa tunaona mchakato mzima wa safari ya wokovu ukiratibiwa na kusimamiwa na Roho ambaye ndiye anabeba asili ya ukamilifu wa ukombozi wa mwanadamu. Sababu ya kuleta habari hizi njema, kutoka kwenye mateso yaani kupokea wokovu, kuileta Imani na kuithibitisha kwa Roho wa ahadi sababu kuu ni “ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.” Hili ni jambo kubwa sana ambalo unapaswa kujua wewe kama mwana wa Mungu.
Sababu au kusudi kubwa la wewe kukombolewa ni ili uweze kufikia milki yako, kwa sababu kile ibilisi alichochukua kwenye maisha yako hakikuwa cha kwake. Mungu Anapokuletea ukombozi ni ili wewe ufikie umiliki wako, kwa maana Ufalme wa Mungu unaporejeshwa, unarejeshwa na milki yake.
Yesu alipokuja alikuja na yote mawili ili kutukomboa na kuturejeshea milki yetu na huu ndio wito wa Efatha, ukombozi na uponyaji.
Ukombozi utanatolewa kwenye mateso na uponyaji maana yake unarejeshwa kwenye hali yako ya asili, asili yetu ni nini? Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”
Wakati Mungu anapanga kuwatoa wana wa Israel, alipanga mapigo 12 kwa Farao, alipanga wana wa Israel kutoka na zawadi na kila alichokitaka Mungu, wakati anapanga haya wana wa Israel hawakujua chochote kile, baada ya kukamilisha mpango wake ndipo akaweka shauku kwa wana wa Israel ya kutaka kutoka utumwani. Unapohisi kuwa unahitaji ukombozi jua kuwa hiyo ni Neema imekujilia na Mungu amekwisha kuanza ukombozi wako.
Kwa nini Mungu alisababisha wana wa Israel wakutane na hatari zote walizokutana nazo njiani? Ni ili kuwaandaa kwa ajili ya milki yao. Kwa sababu kupata milki ni rahisi lakini kuitunza ni ngumu kama haujaandaliwa, na ndio maana unaweza kuona watu wengi waliookoka Mungu akawabariki pasipo kuandaliwa wanaacha wokovu kwa sababu ya kutokuwa na maandalizi ya kutunza hizo baraka.
Umiliki wowote unaanuani, Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;” Baraka zetu zina anuani, zinapatikana ndani ya Kristo Yesu hivyo unapokuwa ndani yake una uhakika wa milki hiyo.
Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.” Popote palipo na milki ya Bwana anakuondolea huzuni na machungu hivyo unafurahia yale uliyopewa
© KATIBU MKUU WA KANISA LA EFATHA – PROF. EMMANUEL CHAO