Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 09/06/2024

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 09/06/2024

MWAKA WA KUMILIKI.
TABIA NDIYO ULINZI WAKO.
Tabia yako ndiyo ulinzi wako, mtu asiye na ulinzi ni kama ngome ambayo imeharibika, na chochote kinaweza kuingia, hivyo yeyote ambaye hajajifunza kuwa na adabu chochote kinaweza kumtokea.
Mwanzo 1:26-27 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
Wote wawili yaani mwanamke na mwanaume waliumbwa katika umoja, wote wana Sura ya Mungu. Sura ya Mungu ilikuwa ni kipaumbele cha kwanza wakati Mungu alipomuumba mwanadamu; na sio sura ya nyani wala mnyama yeyote bali ni Sura ya Mungu.
Unaweza ukawa na shida nyingi, unaweza ukawa na ugonjwa ambao wanakwambia kuwa hauwezi kupona, lakini sikiliza Neno la Mungu linasema nini kuhusiana na kile unachokipitia, Biblia inasema “hulituma Neno lake na kuwaponya”, kama analituma Neno lake na kuruhusu uponyaji kwetu, hivyo kula Neno lake ili upate kuwa hai.
Kula Neno haina maana ya kuwa ni kuja Kanisani kila siku, la! Kanisani ni mahali pa kujifunza Neno na kutambua kuwa hilo Neno linasemaje na ukishalielewa unalishika na kulikiri katika maisha yako nalo litakuwa lako.
Ukilisikia Neno na likaingia ndani yako basi ni lako ukilisimamia litakuwa la kwako.
Tamka Neno maana Mungu anasema huliangalia Neno la mtumishi wake ili apate kulitimiza.
Ukiri wako ndio unaoruhusu Malaika wafuatilie kile unachokitamani na kutimiza kwako, usisikilize ulimwengu unasemaje, bali sikia Neno la Mungu linasema nini na ukishalisikia hilo Neno basi ni la kwako ukalikiri na kushukuru maana litakuwa la kwako. Ukisikia ulichokisikia basi umepata ulichokisikia.
Mungu aliamuru Sura iwe na umiliki, hakuamrisha mtu awe na umiliki, bali Sura yake Mungu ndani ya mtu ndiyo iwe na umiliki, ukiipoteza Sura ya Mungu utabaki na Mfano tu, hivyo utatembea huku duniani ukiwa na Mfano tu lakini haujaibeba Sura ya Mungu. Kwa nini Mungu alimpa mwanadamu Sura yake? Ili awe na umiliki huku duniani. Watu wengi wamebaki na Mfano wa Mungu na siyo Sura ya Mungu na ndiyo maana hawawezi kumiliki.
Ukikosa Sura ya Mungu ina maana kuwa haupati vitu vya Mbinguni bali vya duniani; Vitu vya Mbinguni ni vipi? Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”, hauzalishi chochote kwa maana wewe siyo Sura ya Mungu.
Katika dunia nii asilimia 3% wamebeba Sura ya Mungu (hawa ndiyo wazalishaji), asilimia 10 wamebaki na Mfano wa Mungu na asilimia 87 wamepoteza kila kitu (walaji) na ndio maana unaweza kuona wanahangaika huku na kule kuomba kazi.
Sura ilikuwepo kabla ya kumiliki, Sura ya Mungu kwa mwanadamu ndiyo kipaumbele cha kwanza cha Mungu kwa mwanadamu ili aweze kumiliki.
Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”
Kile unachokizalisha ndipo umiliki wako uliko, Je! Wewe unazalisha nini? Sura pekee ndiyo inaweza kuzalisha, pasipo Sura hauwezi kuzalisha na ndiyo maana unaona katika dunia hii kuna walaji wengi, na wazalishaji ni wachache, Je! Wewe ni nani? Unazalisha nini? Pasipo Sura hauwezi kuzalisha, acha turejee kwenye uumbaji.