Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ibada ya jumapili tarehe 10/12/2013

Watch Now

Download

Ibada ya jumapili tarehe 10/12/2013

Mungu ni mwema na ni mzuri kwako siku zote, chochote unachopitia unaenda KUSHINDA, pale tumaini lako linapokuwa kwa Bwana, pale moyo wako unapofurahishwa na Mfalme wa wafalme, pale kazi yako inapomsifu Mfalme wa utukufu, pale uzuri wako unapogusa moyo wa Mungu, yule simba angurumaye katika maisha yako hatakumeza kamwe.
Haijalishi maadui wanakuja kwako kwa wingi kiasi gani, haijalishi wako wangapi wana nguvu kiasi gani, haijalishi wana hasira na wewe kiasi gani lakini Neema ya Mungu, Utulivu na Nguvu zake zitakufunika na utakuwa salama. Moto unapowaka ili kukuunguza, upepo unapovuma ili kukupuliza, mafuriko yatakapokuja ili kukusomba, usijali; Bwana Yeye atakuinua juu ya yote, haijalishi wamekuficha chini ya mwamba kiasi gani, wewe liitie Jina la Bwana Yeye atakuja na kukutoa hapo kwa sababu Yeye ni mwema atakutafuta popote ulipo na atakutoa hapo kwa maana anakuamini, anakupenda na anakujali atakuchukua kutoka hapo. Bwana anakupenda na anakujali.
Huu ni mwezi wa mwisho, tunaumaliza mwaka 2023; sijui ni kwa namna gani unakwenda kuumaliza mwaka huu, lakini nakuombea uweze kumaliza salama. Pengine hauko vizuri katika ndoa yako, uchumi wako, mahali pako pa kazi biashara yako lakini leo nakutangazia chochote ambacho hakiko sawa Bwana akakupe kumaliza mwaka huu kwa ushindi.
Mara zote Mungu yupo kwa ajili ya ubaadae wako, muda uliobakia kwa mwaka huu ni wa muhimu sana kuliko uliopita, kwa nini? Kwa sababu ubaadae ni wa Mungu lakini yaliyopita ni ya ibilisi na ndio maana ibilisi hawezi kujua nini kinafuata kwako bali anajua nini kilitokea kwako, hivyo ubaadae wako ni wa muhimu sana kuliko wakati uliopita.
Katika ulimwengu huu kuna mtu mmoja ambaye nampenda sana ni yule aliyeangikwa msalabani pamoja na Yesu, katika wakati wa mwisho alifanya jambo zuri kisha akaondoka. Mtu huyu alikuwa mwizi na muuaji akahukumiwa kifo pamoja na Yesu lakini katika wakati wa mwisho wa kufa alifanya maamuzi ya kubadilika na hilo badiliko likamfanya yeye awe mshindi na akamaliza mwisho wake kwa utukufu. Watu wengi wanaanza jambo katika ushindi na utukufu lakini wanamaliza katika aibu na kushindwa. Wanaanza kwa mng’ao lakini wanamaliza kwa kufifia, wanaanza kwa kuruka ruka lakini wanamaliza wakiwa wamelala chini, hii isiwe kwako. Watu wengine wanaanza kwa ufahari na mashangilio makuu wanapo oa au kuolewa lakini wanamalizia katika talaka; hii isiwe kwako. Watu wengi wanatembea katika maisha ya ushindi lakini wanaishia kama walioshindwa.
Katika wale watatu ambao waliangikwa msalabani mmoja akamaliza safari yake ya maisha kwa maumivu ya milele lakini mwingine alimaliza kwa utukufu milele, hii inakuwaje? Vile unavyovisikia na kuvitafakari ndivyo vitakupa wewe kumaliza katika maumivu au utakatifu milele. Vile unavyowasilisha ujumbe wako au unavyonena Neno la Mungu ndivyo itakupa wewe kuwa mshindi au wakushindwa; katika wale watatu walioangikwa msalabani mmoja alisema fanya kama unavyofanyaga tutoke hapa lakini mmoja alisema Bwana unikumbuke, hakusema uniponye bali aliomba kukumbukwa wakati wa utukufu na ndivyo ilivyokuwa.
Unapokaribia kufika pale ambapo Mungu amekuandalia kwa ajili ya urithi wako, mahali ambapo amekuahidi, unapokuwa tayari kutimiliza kile ambacho Mungu amekuahidia kuwa makini sana kwa maana jambo fulani linaweza kutokea ili kukurudisha nyuma. Unapokaribia kuinuka katika ukuu wako wakati wote na mara zote jambo fulani lazima litokee ili kukurudisha nyuma.
Wakati ambapo unakuwa tayari kufurahi, kusherekea au kuona ghafla hakuna linalokuja wala kinachoonekana kwako, unaona kama uko jangwani. Ulikuwa punde tu uweze kutukuzwa lakini ghafla tu jambo linatokea furaha yako inaondoka, inaonekana kama kila kitu kimezimishwa, hakuna jambo lolote zuri linakuja kwako, usijali unapoona wakati huo anza kucheza, kufurahia kwa maana ukuta ulioko katikati yako na utukufu wako unaokuzuia unakaribia kuanguka na punde utashinda.
Kitu chochote cha thamani kimefichwa mahali fulani, na ndio maana unaona kuna kitu kimekuja mbele yako kukuzuia, unapoona hivyo inamaana kuwa vitu vyako vya thamani vipo karibu kuja katika maisha yako. Lakini wengi wanapoona hivyo wanaanza kulaani, kunung’unika na kulalamika, wananza kuudhika na kuwa na hasira, na wengine wanakata tamaa kabisa. Unapoona chochote unachokihitaji hakiji, furaha imeondoka, uzuri umeondoka au kipato kimeondoka usijali sasa fahamu katika akili yako kuwa unaingia katika vitu vya thamani. Kama ni fedha ilikuwepo lakini sasa imetoweka, ulikuwa unafanya vzuri katika biashara lakini sasa vimetoweka, jua kuwa unaenda kupokea vitu vikubwa kuliko vya mwanzo.
UKIRI:
Bwana sasa ninaanza kuelewa, ninapitia haya kwa sababu jambo fulani la thamani kwa ajili yangu lipo karibu yangu nipe kulifikia.
Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.
Isaya 54:17 “ Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana.”
UKIRI:
Kuanzia leo hakuna silaha itakayofanyika kinyume changu ambayo itaweza kufanikiwa juu yangu. Kuanzia leo hakuna silaha itakayokuja kinyume changu ikaniangamiza bali nitazitumia hizo silaha kumshinda ibilisi na kamwe hazitatumika kinyume changu bali mimi nitazitumia kinyume cha uyo adui.
“Na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa” kuanzia leo kila ulimi ambao umenilaani naugeuza unibariki, kila ndimi zinazoinuka kinyume changu zitanibariki na sio kunilaani kwa sababu huu ni urithi wangu kubarikiwa na sio kulaaniwa, hivyo nyinyi ndimi mnaoinuka kinyume changu kaa kimya mpaka pale utakapojifunza kunibariki.
MAOMBI:
1. Batilisha kila maneno yaliyotamkwa kinyume chako yakawa laana kwako badilisha hiyo laana kuwa baraka.
2. Kila ulimi ulionena kinyume changu katika mawazo, mahali pa wazi au pa siri mahali pa kuabudia popote pale leo nabatilisha hayo maneno, kuanzia leo hawatanena kinyume changu tena bali watanibariki.
3. Mimi nimebarikiwa hivyo hakuna laana itakayoinuka kinyume changu na ikitokea imeinuka naibatilisha ikawe baraka kwangu.
4. Baba nachukua nafasi yangu, ninampiga ibilisi, namfukuza aende nje ya maisha yangu, ndoa yangu, uchumi wangu, afya yangu, urithi wangu, mwili wangu na kila uchawi katika mwili wangu au laana au kazi za wachawi kwenye mwili wangu, kila umiliki wa kipepo katika maisha yangu ninaupiga uende nje ya mwili wangu, hili ni hekalu la Roho Mtakatifu, na kamwe hautaingia tena kwa Jina la Yesu, mimi ni mbarikiwa wa Bwana.