Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI TEREHE 12/05/2024

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI TEREHE 12/05/2024

SOMO: UHURU WA UTUKUFU
Warumi 8:21 “Kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.”
Biblia inasema viumbe navyo vinahitaji kuwekwa huru, kama unafuga kuku pia naye anahitaji uhuru, kama viumbe vinahitaji uhuru vipi kuhusu mwanadamu? Kwa nini vinahitaji uhuru? Biblia inasema “hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.” Watoto wa Mungu wanapaswa kuwa huru katika utukufu wa Mungu.
Kama kuna uhuru wa utukufu maana yake pia kuna uhuru usio na utukufu. Mungu akikupa uhuru maana yake amekupa uhuru wenye utukufu ukiutumia vibaya huo uhuru uliopewa maana yake huo uhuru uliopewa unakosa utukufu wa Mungu.
Kuna watu wamepokea uhuru wa utukufu wa Mungu, walikuwa na vifungo vya magonjwa na Mungu akawapa uhuru wenye utukufu, uhuru wenye utukufu ni uhuru wenye ulinzi wa Mungu. Mungu ametupa uhuru wa kuamua kuja kanisani au la lakini kuna wengine wamepewa uhuru huu na kuutumia vibaya, ukifika mahali ukaanza kusema mimi siendi kanisani jua kuwa uhuru wako hauna utukufu wa Mungu kwa maana uhuru wenye utukufu wa Mungu unahitaji ibada.
UNAUPATAJE UHURU WENYE UTUKUFU WA MUNGU?
Yohana 8:36 “ Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”
Je unao uhuru kweli kweli? Mungu alitubariki tukazalishe na kuongezeka hii inamaana kuwa watu hawana uhuru wa kweli kweli, na uhuru wa kweli kweli unaanzia kwenye akili, akili yako ikiwa huru kweli kweli tutaona maisha yako yakibadilika. Uhuru huu ambao anatupa Yesu sio uhuru wa kuwa mbali na magonjwa tu, bali ni uhuru wa mitazamo yetu pia, namna tunavyoamua mambo na kuenenda. Uhuru wa kweli upo kwenye akili na moyo wa mtu. Mtu ambaye moyo wake na akili yake iko huru hata vitu vyake utaviona vikichanua.
Unapataje uhuru wenye utukufu? Kwa kusikiliza injili yenye utukufu wa Mungu, kwa maana siyo kila injili ya kusikiliza, ukisikiliza injili yenye utukufu itabadilisha akili yako; mtu ambaye anasikiliza injili ya utukufu hata maombi yake yanakuwa ya utukufu.
Injili yenye utukufu inakuletea uhuru wenye utukufu kwa maana ukiisikiliza na kufanyia kazi italeta utukufu katika maisha yako, utukufu maana yake heshima, nguvu na uwepo wa Mungu. Ukiwa msikilizaji mzuri wa injili ya utukufu lazima ikubadilishe.
2 Wakorintho 4:4 “Ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Ukisikiliza injili yenye utukufu wa Mungu unapata upenyo katika maisha yako.
Ukiipata injili yenye utukufu unakuwa huru kweli kweli.
Warumi 6:16 “Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki.”
Hapa tunaona kuna aina mbili za utumishi.
1. Utumishi wa dhambi ambao mwisho wake ni mauti, utaujuaje upo katika huu utumishi? Kila unachokifanya kinakufa, utaanzisha biashara haiendi mbele utakuwa na mahusiano yatakufa tu, kwa nini? Kwa sababu upo katika utumishi wa dhambi ambao mwisho wake ni kuua vitu.
2. Utumishi wa utii ambao mwisho wake ni haki; ukiwa na utuishi huu maana yake chochote utakachokifanya kitaleta haki katika maisha yako.
Je! Wewe upo kundi gani?
Ukitaka kupokea haki yako chochote ambacho unataka kukipata, angalia aina ya utumishi wako, je! Ni utumishi wa utii ili upate haki? Au ni utumishi ambao hautii maelekezo ili upate mauti? Ukiwa na aina hii ya utumishi wa kuasi hakuna kitakachotokea kwako mpaka pale ambapo utaamua kutii ili upate haki.
Ufanyaje ili uweze kufanya utumishi wako uweze kudumu?
Yesu alitukomboa lakini kwa nini vifungo na matatizo tuliyoyaacha yanaturudia tena, kwa nini uhuru wa utukufu wetu hatuufurahii na umeondoka? Ufanyaje ili utukufu wa Mungu uweze kudumu?
1. Tambua ya kale yamepita, katika kuishi kwako ukitaka uhuru huu uliopewa na Kristo uweze kudumu, tambua ya kale yamepita, usiishi na ya kale kichwani mwako kwa maana ya kale yanaweza kukunyika uhuru. 2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”
Kichwani mwako kutambue kuwa wewe ni kiumbe kipya na uishi katika uhuru wa utukufu na siyo wa wasi wasi. Usipotambua kuwa yakale yamepita ibilisi atatumia hayo ili kukutesa.
Ni kweli kabisa umezaliwa na familia uliyozaliwa lakini tambua kuwa una uhuru wenye utukufu, ni kweli kabisa kuwa sasa hauwezi kushika hata laki moja, ni kweli umezaliwa katika familia ambayo wanakufa mapema lakini tambua kuwa wewe una uhuru wenye utukufu kamwe hautakufa mapema. Wewe mweye uhuru wenye utukurfu una uhuru wa kuanzisha mradi, kuzaa, kufanya biashara, kufanya chochote unachokitaka na kikawa kwako. Njia nyepesi ya kuwa huru ni kusahau yaliyopita.
© Kiongozi wa Kiroho wa Kanisa la Efatha- Mtume Noel Kapinga