Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mahubiri Jumapili 17/12/2023

Watch Now

Download

Mahubiri Jumapili 17/12/2023

Je, wewe una msifu Bwana? Je, unazo sifa za Bwana? Kuna wengine wana sifu sifa za Bwana, lakini kuna wengine wanazo sifa za Bwana, mwana wa Mungu sio tu unatakiwa kusifu bali unatakiwa kuwa na sifa za Bwana, ukiwa na sifa za Bwana kweli itakuwa ndani yako.
Kwa nini watu wanateseka na wamezaliwa mara ya pili? Ni kwa sababu wanapenda uongo kuliko kuipenda kweli. Uongo utakusababisha uteseke, lakini kweli itakukomboa. Kweli inakufanya uwe salama ndio maana Biblia inasema kweli itakuweka huru. Kweli ni njia ya wokovu na njia hiyo ndiyo inakupeleka kuwa salama.
Tunaipataje kweli? Ziko dini nyingi hapa duniani, lakini dini pekee inayofanya watu waielewe kweli ni dini inayozungumzia wokovu. Ni wokovu pekee unaokupa kweli na kukufanya kuitwa mwana wa Mungu, hakuna anayeweza kusema mimi ni mtoto (mwana) wa mtu fulani mpaka baba aseme kuwa mimi ni baba yako. Mtoto hakuwepo bali aliyekuwepo ni Baba na Mama, walipitia tukio fulani na kupitia hilo tukio mwana au binti akazaliwa.
Kama unataka kukaa mbali na uharibifu penda kweli, lakini kama unataka uharibifu ukae na wewe penda uongo.
Kuna muda unashindwa kuendelea kwa sababu unajilinganisha na shangazi yako aliyeshindwa badala ya kujilinganisha na yule aliyeshinda. Wewe ni mwana wa Mungu hivyo maisha yako hayafanani na shangazi yako bali yanafanana na Mungu aliyeumba Mbingu na nchi.
Kama tunaishi hapa duniani, tunatakiwa kujua nchi hii tunayoishi iliumbwa na Mungu aliye Baba yetu. Unapaswa kujua mimi ni wa duniani kwa sababu nipo duniani lakini wenyeji wangu ni mbinguni.
Mwanzo 1:2 “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”
Anaposema mbingu na nchi huu ni uumbaji, Mbingu ilikuwa na kila kilichokuwa kinahitajika, lakini dunia ilikuwa utupu na ukiwa mpaka pale Mungu alipoumba.
Mwanzo 1:3 “Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.”
Mungu alifanya mambo matano:
1. Aliumba
2. Akaona
3. Akaigundua
4. Aliamua
5. Alitendea kazi kwa furaha
Kwa hiyo kazi tunayoifanya lazima itupe furaha. Mungu aliumba dunia kwa furaha na ndio maana aliuona ule utupu uliokuwa duniani na ule ukiwa, Mungu akagundua kuna vurugu kwa sababu ya giza, kwa hiyo Mungu akafanya maamuzi na akasema na iwe nuru. Kwa nini nuru? Nuru inasaidia kuweka wazi mambo, na kuweza kupambanua vitu. Pasipo Nuru hauwezi kutembea katika kweli.
Nuru inakupa kupambanua hii ni nyeupe na hili ni giza. Je, unaweza kujua nani ni nani ndani ya giza? Ndani ya giza utasikia tu kelele kwa sababu humuoni yeyote, kwa hiyo giza ni vurugu. Hivyo Mungu akaamua kutuliza vurugu kwa kuingiza (nuru) akasema “na iwe nuru” na nuru ikawa.
Mungu akasema nuru ilikuwa njema maana yake Mungu alikuwa na furaha ni kwamba giza halikuwa jema.
Wakati Mungu anatenganisha vitu wakati wa uumbaji aligundua giza na nuru maana yake aligundua mbaya na njema; kwa hiyo giza ni baya, na nuru ni njema, kwa hiyo kile kibaya ni cha uovu, na cha nuru ni kitakatifu. Uovu unaleta uharibifu, kitakatifu kinaleta amani. Uharibu unaleta chuki, amani inaleta ukarimu na vingine vingi.
Mungu alisababisha tukio na baada ya hilo tukio aligundua vitu vingi. Kutokana na giza, akafanya jambo la kusababisha giza liondoke kwa sababu giza sio jema. Haya yote ni matukio na Mungu ndiye aliyesababisha haya matukio yawe. Giza halikutokea tu lenyewe, bali Mungu ndiye aliyeumba giza. Nuru ilikuwa ni tukio maana Mungu ndiye aliyeweka nuru. Kwa hiyo kilichochema na kilicho kibaya ni matukio na Mungu ndiye aliyefanya haya matukio yote mawili. Mema na mabaya ni matukio, uovu na utakatifu ni matukio.
Mwanzo 1:26-27 “Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.” Anga ni mali ya nuru. Anga lilikuwa hivyo kwa ajili ya nuru. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.
Mungu aliyafanya haya kwa ajili ya nuru na sio kwa ajili ya giza. Kwa hiyo usiruhusu ibilisi akalitumie anga lako. Mungu hakuliumba anga kwa ajili ya ibilisi bali kwaajili yako.
Mwanzo 1:9-11 “Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.” Uoto na miti inayozunguka nchi ni kwa ajili ya nuru na sio kwa ajili ya giza.
Mwanzo 1:14 “Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;” Nyota, Mwezi na Jua vipo pale kusababisha majira yako, siku na mwaka wako.
Kila siku jua linapochomoza kuna jambo jipya kwenye maisha yako, kama jua limechomoza na ukaamka na maisha yako yakawa kama jana, basi kuna tatizo na uharibifu upo juu yako. Kila siku, jua likichomoza lipo pale kukusababisha unga’e maana yake kila siku, kila mwaka lazima kuwe na kitu kikuu na kipya katika maisha yako na kiwe na mguso kwenye maisha yako na maisha ya watu wengine wanaokuzunguka, lakini ukiona mwaka unaisha na maisha yako yako vile vile, hakuna kusonga mbele jua kuna tatizo.
Mwanzo 1:17 “Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi”
Mwanzo 1:20 “Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.”
Hapa ina maana kila kilichopo kwenye maji ni mali ya nuru. Mpaka sasa giza halina kitu yaani halimiliki chochote. Kwa hiyo usimkuze ibilisi akaonekana ni mkubwa sana kuliko Nuru.
Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mungu alitaka wewe uwe nakala (copy) yake, ufanane naye, maisha yako yawe kama Yeye, kama Yeye alivyo muumbaji na wewe uumbe mambo mapya na ufanye mambo makubwa katika maisha yako kwa sababu wewe ni nakala (copy) yake.
Nilipomuoa mke wangu, nilitaka kutoa nakala zangu, na kama hii ni kweli maana yake chochote kinachotoka kwa mke wangu (watoto) ni changu, yani kinafanana na mimi. Na kama ni nakala zangu, lazima zitende kama mimi ninavyotenda, chochote nilichonacho ni cha kwao. Kama mimi ni muhubiri, wanangu lazima wapende ninachokifanya na wasikie furaha lakini kama ninachokifanya hawakipendi, maana yake sitembei katika nakala ya Mungu.
MAOMBI:
1. Baba nipo tayari kuchukua nafasi yangu kwa sababu mimi nimzalishaji na mimi ni wa Mungu na uzalishaji umo ndani yangu, na sasa ninazalisha, kile kilicho ndani yangu na kukitoa nje, hivyo lazima kila talanta iliyowekwa na Mungu ndani yangu lazima itoke, akili yangu lazima itoke ikazae matunda, mbegu ndani yangu lazima itoke, na kuzaa sana, sitakufa maskini kwa sababu mimi ni mzalishaji, mbegu iliyopo ndani yangu ambayo Mungu aliiumba ndani yangu lazima itoke na izae matunda.
2. Amrisha tunda lilipo ndani yako litoke, ile mbegu ya Mungu ambayo Mungu aliiumba ndani yako lazima itoke, acha ikachipue na kuleta matunda.
TANGAZO:
Baba mimi nina matunda kwa sababu uliniumba katika nuru na sio katika giza na wala sio chini ya uharibifu, bali katika amani, sio katika chuki, bali katika ukarimu. Eh Baba, napokea amani yangu sasa, ili niweze kuzaa matunda. Amen