Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Namna ya kutunza na kulinda baraka zako

Watch Now

Download

Namna ya kutunza na kulinda baraka zako

Kwa nini tunalinda Baraka zetu? Kwa sababu tunajua kuwa kuna adui, Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”Tunapaswa kulinda Baraka zetu kwa sababu kuna mwizi, muuaji na muharibifu wa hizo Baraka.
Namna ya kushinda hao maadui ni kuomba msaada kutoka juu, sawa na Zaburi 91:1-4 “ Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.”
Zaburi hii inatuambia namna ya kukaa katika uvuli wa Mungu ili adui asiweze kuchukua Baraka zetu.
1. Unapaswa kukaa uweponi mwa Bwana, kwa nini? Kwa sababu katika uwepo wa Bwana kuna mahali pa kujificha panaitwa mahali pa siri. Unalindwa ili nini kisikupate? Mwizi, muuaji na muharibu asikupate.
• Mahali pa siri ni mahali pa kujificha unajilinda wewe mwenyewe na Baraka zako.
2. Katika uwepo wa Bwana utapata hazina zilizo fichika, kwa ajili yako, na hizo hazina zitafunuliwa kwa wana wa Mungu.
1 Wakorintho 2:9 “ lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.”
Mambo hayo yamefichwa na ili uweze kuyapata lazima uende mahali pa siri pake YEYE aliye juu (Mungu) unapokubali kuingia mahali pa siri hazina hizi zinafunuliwa kwako na zinakuwa za kwako.
3. Uweponi mwa Bwana kuna uvuli unaokufunika, Mungu anatulinda kwa mbawa zake kama kuku anavyolinda vifaranga vyake. Ukiona kuna vitu hauvielewi kimbilia katika uvuli wa Bwana hapo utakuwa salama. Tamani kuwa katika uwepo wa Bwana usiku na mchana ili uwe salama.
4. Lazima udumu katika uvuli wa Bwana, kuwa na sehemu moja ya kuabudu ambapo Mungu akitaka kukubariki anajua atakupata wapi ili uweze kuziona Baraka zake kwako, lakini ukizunguka kanisa baada ya kanisa unakosa baraka zako.
Luka 8:40-55 “ Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote. Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;………..”
Watu hawa walipokuwa katika mkutano huu walikuwa na shauku ya kupokea kutoka kwa Yesu, lakini mtu mmoja aliyeitwa Yairo alikuwa na ajenda maalum katika moyo wake ya kutaka binti yake aweze kuponywa. Jina la mtu huyu lilitajwa kwa nini? Kwa sababu yeye alikuwa ni mtu wa kanisani; je! Wewe unayesema kuwa umeokoka jina lako linajulikana mahali unaposali? Na ili lijulikane lazima uwe na kitu unachokifanya ndani ya nyumba ya Bwana. Kile unachokifanya kwa ajili ya Bwana ndicho kitaorodhesha jina lako mbele za Bwana wa mabwana. Wakati mwingine unaweza ukapitia changamoto lakini kupitia kile unachokifanya unapata usaidizi.
Kupitia kile unachokifanya ndani ya nyumba ya Bwana ndicho kitakutambulisha kwa Mungu na kitaweka alama katika ulimwengu wa roho.
Mara zote unapokuwa katika uwepo wa Bwana kiri kile unachotaka kuona sawa sawa na kile unachokitaka na ndicho kitakachokuwa kwako.
Mara zote mwamini Mungu aliye juu na umtumaini YEYE kwa maana Yeye yupo na ana nguvu zaidi ya mamlaka zote na Neno lake ni la mwisho na hakika litatimia kwako kwa maana hakuna anayeweza kulifuta Neno lake.
Mungu akisema umebarikiwa Neno lake ni la mwisho na lina mamlaka juu ya mamlaka zote; na hakuna aliye juu yake wala anayeweza kukata rufaa kwake. Akisema umeponywa basi ni kweli umeponywa na hakuna anayeweza kubadilisha hilo, hivyo ukija kwake mwamini yeye na ukimwamini hautahangaika huku na kule kutafuta manabii bali wewe unakuwa nabii mpya wa maisha yako.
Jifunze kujitabiria mwenyewe katika maisha yako na itakuwa, hata kama unaona kuwa wewe ni maskini sema “mimi ni tajiri nimebarikiwa” hakuna atakayeweza kufuta ukiri wako bali utatimia kwako. Simama Imara tabiria maisha yako mwenyewe, acha kutafuta watu ambao wao wenyewe hawajamaliza kutabiria maisha yao ili wakutabirie, simama na ujitabirie wewe mwenyewe na hayo unayojitabiria yatatimia kwako.