Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

NENO IBADA YA JUMAPILI 28/01/2024

Watch Now

Download

NENO IBADA YA JUMAPILI 28/01/2024

Huu ni mwaka wetu wa kumiliki hivyo hakikisha unamiliki kitu. Umiliki ndani ya Kristo Yesu kamwe hauhusiani na nguvu yako wala mapato yako bali unahusiana na mahusiano yako na Yesu. Kupitia mahusiano yako na Yesu, utaanzisha biashara pasipo mtaji, utaenda chuo kikuu ilihali wazazi wako hawawezi kumudu ada; utajenga nyumba ilihali haunafedha; kwa sababu Mungu ni Baba yako na Kristo Yesu ni chanzo cha fedha yako, ni chanzo cha ada yako, mtaji wako na fedha za kujenga nyumba.
Hakikisha mwaka huu unaweka mahusiano mazuri na Yesu, kaa mbali na dhambi kataa dunia na mambo yake husiana na Kristo na utembee pamoja na Yeye; mfanye Yeye afurahi, namna unavyoongea, unavyotembea na kutenda hakikisha unafanya kama Yesu kwa sababu Yesu anaishi ndani yako. Mahusiano yako na Kristo yakikaa vizuri kamwe hautakufa maskini.
Waefeso 1:3-7 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo……..” vitu vyote tunavyotaka vinaanza rohoni, hivyo unapoanza kitu rohoni inamaana kuwa hicho kitu tayari kimeshaletwa kwako.
Siku utakapoanza kuvitafakari maana yake umesha kabidhiwa tayari, kwa nini umeokoka lakini ibilisi anaweza kukuchawia? Kwa sababu hauna mikono safi na moyo mweupe. Anza kuishi maisha ya kujidhabihu maisha ya mikono safi na moyo mweupe ili chochote utakachoomba kwa Mungu aweze kukupata.
Zaburi 24:1 “ Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.” Huku duniani utasikia kiwanja hiki ni cha flani na hiki ni cha flani nani anayewapa? Biblia inasema mmiliki ndiye anayewapa (Mungu). Kama unataka kumiliki kile ambacho Mungu alichonacho yapasa uelewe mambo machache.
Zaburi 24:3 “Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.” Aina ya mtu huyu anaweza kumuendea Mungu na kuomba kitu na akapewa, usifikiri ni kwa sababu haufanyi kazi kwa bidii ndio maana haupokei au wewe ni maskini, la! Bali unapaswa kutambua kuwa hauna sifa za kutosha na ndio maana haupokei kutoka kwake. Uumbaji wote una haki ya kumwendea Mungu na kupokea kitu kutoka kwake, hao ambao ni waaminio wana haki ya kumwendea Yeye na kupata kitu lakini wanapaswa kwenda wakiwa na mikono safi na moyo mweupe. Hao ndio tunawaita waabuduo.
Waefeso 2:19-20 ” Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Watu hawa ndio warithi wa nyumbani mwake Mungu.” Siku nilipogundua kuwa Mungu ana kilichobora kwa ajili yangu nilihakikisha ninastahili pamoja na watakatifu wake ili niweze kurithi. Sio kila anayekwenda chuo kikuu anamaliza akiwa na cheti, vivyo hivyo hata katika Ufalme wa Mungu unapaswa kuhakikisha unastahili kupokea kutoka kwake.
Ili kufurahia maisha bora huku duniani ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili yako inakupasa uwe na tabia ambayo itampendeza Mungu, tabia ambayo itasababisha Mungu akutangaze kuwa huyu ni mwanangu mpendwa mpeni chochote anachokitaka kwa sababu ninapendezwa naye, lakini usipoichonga tabia yako ikampendeza Mungu, utaabudu na utakuja kanisani kila siku, kweli utafika mbinguni lakini kamwe hautayafurahia maisha hapa duniani utaishia kuwa kama mpitaji tu ilihali ulikuwa ni mwenyeji sawa sawa na watakatifu wa Mungu.
Huu ni wakati wako wa kuchukua kilicho cha kwako hivyo jiandae kuwa na tabia njema ili uweze kupokea kutoka kwake. Zaburi 24:4 “ Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila.”
MAOMBI
1. Baba yangu wa mbinguni nataka niwe kwa ajili yako peke yako, namna ninavyozungumza ninavyotenda, nataka niwe kwa ajili yako. Yesu tumia kinywa changu, miguu yangu, mikono yangu na kila kitu changu ili ninapostawi sitasema ni kwa nguvu zangu bali nitasema Mungu amenibariki.
2. Mungu nataka nifanane na wewe, na chochote kinachonizuia kufanana na wewe acha kiondoke. Roho wa Bwana akakubadilishie namna ya kuongea kwako, usiongee tena kama shetani anavyotaka uongee bali ongea kama vile Mungu anavyotaka tamka mema kwa ajili yako, Roho wa Mungu akubadilishie namna ya kutembea usiende kama ulimwengu unavyotaka, watu, ibilisi wala kama ulivyokuwa unaenda huko nyuma, ruhusu Roho wa Mungu abadilishe mwenendo wako. Lolote ulitendalo fanya kwa moyo mweupe ili ibilisi asizuie, anza kukisema ili kipate kutimia.