Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Nguvu ya Neema

Watch Now

Download

Nguvu ya Neema

SEMINA YA UREJESHO IRINGA

TAREHE: 01-12-2023

KUHANI: JAMES NYANSIKWA

 

Neema inarejesha imani iliyopigika inarejesha tumanini lililopotea inarudisha nuru katika giza.

Yohani 1:16 “Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.”

Kinachowafanya walokole wengi wasisonge mbele ni shetani aliyewakalia mbaka kichwani, neema imebeba utimilifu utimilifu ni kitu ambacho hakipungukiwi chochote. Neema imebeba pendo imebeba utimilifu imebeba urejesho yaani neema ina kila kitu. Na neema imeandaliwa kwaajili ya sisi sote.

Efeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu”

Kunawatu mbalimbali duniani hii ni kwasababu wengine wameikataa neema. Neema inakupa kutumiwa na Mungu, Mungu akikutumia inasababisha ipate utimilifu na kutumiwa na Mungu kunasababisha shetani asikutumie maana huwezi kutumika na watu wawili kwa wakati mmoja. Tunachoitaji ni neema ya Mungu ukishaipata ile neema unakua msaada kwa watu wengine kama upochini ya mtumishi wa Mungu mwenye neema unahaki sawa nayeye kuipata ile neema na hiyo ndiyo neemaa juu ya neema.

Kutoka33:12 “Musa akamwambia Bwana, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu.”

Kutumiwa na Mungu kunahitaji neema, haijalishi katika magumu tunayopitia tunahitaji neema ya Mungu iliitotoe tulipo.

Kutoka 3:7-10 “Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.”

Baaada ya vilio vya wana wa Israel Mungu alimpa neema Mussa ili awatoe wanawaisrael kutoka utumwani hivyo Mussa alitumia neema aliyopewa na Mungu kuwatoa watu wa Mungu utumwani.

Kutoka 4:22 “Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu”

 

Matokeo yoyote ya mtu yanategemeana ndani, kwamba unaelewa nini kuhusu neema iliyompeleka Yesu msalabani.

1wakorintho 1:4-5 “Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote”

Ukipewa neema unapewa na utimilifu wake. Neema haijapungukiwa chochote, na chochote utakachopoteza neema inarudisha, ukimkili Yesu kua Bwana na mokozi wa maisha yako unapokea neema na damu yako inakua damu ya Yesu maana unaile neema yake.

Mtu anaeikosa hiyo neema anapungukiwa maarifa na mtu aliyepungukiwa maarifa hajatajirika na anakua mjinga hatakama ni msomi, ukibeba neno la Mungu unakua hujapungukiwa kitu chochote maana ni uweza ubebao vyote. Ukibeba neno la Mungu umebeba uweza wa Mungu na ukibeba uweza wa Mungu umebeba kila kitu na unakua na ile neema ya Mungu ukielewa ile nguvu ya neema na kwamba Yesu alikufa kwaajili yako na alikuja kwaajili yako na kesi zako zote, maana unapokua na nguvu ya neema hutakiwi kufanya fitina iliuwe katika viwango vya juu kwasababu unakua na ile neema ya Mungu na ile nguvu ya neema ya Mungu inakupa uwezo wa kufikia ile sehemu unayoitaka.

Kipindi cha Sauli Mungu alimtumia Samweli kumpaka mafuta na kumuandaa kwaajili ya kuokoa watu wake kwenye mikono ya adui kwasababu alishindwa kuitumia ile neema ya Mungu alitamani kumuua Daudi, Mungu alimteketeza yeye na kizazi chake ndipo Mungu akamtumia Samweli kumpaka mafuta Daudi kua mfalme na kwasababu ya ile neema ya Mungu juu ya Daudi alifanya mambo makubwa kuliko Sauli na alishinda kila vita iliyoinuka juu yake, Daudi kila alichopata alimpa Mungu kwanza ikasababisha kizazi chake kukaa madarakani mda mrefu mbaka wajukuu zake.

Luka 1:30-32 “Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.”

Kumbukumbu ya torati 8:18 “Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.”

Nguvu ya neema inafanya kazi kwenye kila kitu

1Wakorntho 15:9-10 “Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.”

Ukiwa na neema ya Mungu unanfanya kazi zile alizokua anafanya Yesu maana neema inakupa nafasi ya kufanya kazi kubwa.

1yohana 3:8 “atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.”

Ufunuo wa yohana 12:7-9 “likuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”

 

Luka 19:10 “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

Lazima tumjue huyo anayekuja kuokoa na kutafuta kilichopotea.

Mathayo 1:21 “Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.”

Ukikataa wokovu inamaana umemkataa Yesu na ukimkubali Yesu na ukakataa wokovu inamaana umemkataa Yesu pia na kukataa wokovu ni kutafuta njia ya kuelekea jehanamu.

Ndani ya neema kunawokovu na ndani ya wokovu kunarehema huruma na msamaha inamaana ukiwa ndani ya wokovu utapata rehema na ukikataa wokovu inamaana ukitaka msamaha bila wokovu inamaana unatengeneza njia yakuelekea kuzimu.

Ni kitu gani kilimfanya yesu aje na kuokoa?

Yohana 1:14 “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”

Alikua na neema iliyomuwezesha kuja kuokoa na kutafuta kilichopotea kuja kuleta wokovu utakao tupa rehema.

Efeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;”

Yeye amejaa neeema na kweli vinavyorudisha na kurejesha heshima yetu pia neema hiyo na kweli hiyo inatupa rehema. Ukiwa na wokovu nguvu za giza hazikupati kwamaana unakua na neema yake.

Wakolosai 1:13 “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake”

Zaburi 103:2-3 “Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote”