Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Namna ya kutunza na kulinda baraka zako.

Watch Now

Download

Namna ya kutunza na kulinda baraka zako.

Ili uweze kutunza baraka za Ibrahimu katika maisha yako hekima inahitajika, Biblia inasema hekima ni ulinzi, hekima itakupa kukomboa wakati kwa maana utajua nini cha kufanya na wakati gani wa kufanya na hicho unachofanya kitafanikiwa.
Waefeso 5:15-16 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” Ili uweze kupokea Baraka za Bwana katika maisha yako unapaswa kuitafuta hekima, kwa maana wakati mwingine ili uweze kuzipokea hizo baraka utapaswa kufanya kwa haraka, ukiwa na hekima itakupa kufanya hayo. Biblia inasema “ukipungukiwa na hekima uombe” ukipungukiwa na hekima omba na ukishaomba tembea kama mtu mwenye hekima. Hekima ni kitu cha muhimu sana katika maisha yako.
Baada ya Sulemani kuomba hekima kwa Mungu akapewa lakini baada ya Mungu kumpa hekima ndipo akajua kuwa Sulemani anaweza kumiliki na kutawala vitu vingine vyote, ndipo Mungu akampa mali zote za ulimwengu huu. Ukitaka kupokea baraka za Mungu omba hekima ya Bwana ikujilie, kwa maana hekima ikikujilia utapokea vyote unavyovihitaji.
UKIRI:
Eeh! Mungu naomba unijalie kuwa na hekima, nijue namna ya kuenenda, kutenda na kuukomboa wakati kwa maana kuna mema umeniandalia mbele yangu kwa ajili ya ubaadae wangu, maisha yangu na utumishi wangu, eeh! Bwana nipe hekima yako ili nipate kuufurahia wokovu wangu siku zote za maisha yangu.
Ili uweze kutunza baraka za Ibrahimu katika maisha yako unahitaji kukaa hemani mwa Bwana katika uwepo wake.
Daudi akasema katika: Zaburi 27:4 “Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.”
Hili ndilo tamanio la moyo wa Daudi, je! Wewe kiu yako ni ipi unapokuwa hemani mwa Bwana? Maana yamkini kuna changamoto nyingi sana unapitia katika maisha yako, familia yako, ndoa yako, n.k, je ukiwa mbele za Bwana unatazama yale yanayokusumbua au unafungua ukurasa mpya wa kutazama uzuri wa Mungu? Hakikisha ukiwa mbele za Bwana unautazama uzuri wa Mungu na kuukiri. Lile Neno ulilolipata kwa kufundishwa au kusoma Neno hakikisha unalikiri mpaka litimie na liwe la kwako.
Je! Wewe unakwenda ibadani kufanya nini? Kukutana na marafiki zako? Kukutana na watu au kuna kitu unakitarajia kutoka kwa Bwana? Mfalme Daudi akasema “Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.” Je wewe unatafuta nini ukiwa mbele za Bwana.
Luka 2:43-46 “Na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.”
Wazazi wa Yesu walipomtafuta Yesu walimkuta hekaluni, kwa nini? Kwa sababu alikuwa anasikia raha kukaa hekaluni mwa Bwana. Je! Wewe wakikutafuta watakukuta wapi? Je watoto wako wakipotea unawapata wapi? Jumapili ikifika, je! Unapenda kuwa wapi wewe? Pale unapopenda kuwa ndipo patakuonyesha una vinasaba (DNA) ya wapi kama ni ya Mungu au kwa ibilisi.
Je unataka mambo yatokee kwako? Weka nidhamu ya ibada yako na Mungu.
Kitu chochote ukikifanya nje ya uwepo wa Bwana ni bure lakini ukiwa uweponi mwa Bwana kuna nguvu ya Mungu ya kukushindia.
ITIFAKI YA KUINGIA UWEPONI MWA MUNGU
Yeyote anayetamani kuingia uweponi mwa Mungu anaweza kuingia kama akifuata itifaki zifuatazo-:
1. Lazima uwe umeyatoa maisha yako kwa Yesu (umeokoka) ukiokoka hakikisha unaisha maisha ya Imani katika Kristo Yesu kwa maana umefanyika kuwa Mwana wa Mungu. Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.”
2. Tunaingia uweponi mwa Bwana kwa njia ya sifa na kushukuru, Zaburi 100:1-5 “ …….Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.” Nini kinatokea unapoingia mbele za Bwana kwa kusifu? Adui zako wanazungukwa na kukamatwa, na wewe unavikwa nguvu.
• Uweponi mwa Mungu nguvu ya dhambi inavuliwa madaraka.
3. Unapokuwa uweponi mwa Bwana tafakari uzuri wa Bwana, acha kutafakari matatizo yako, ukiona jambo haulielewi katika maisha yako ingia uweponi mwa Bwana, imba, sifu na shukuru; sifa zako zitafungua kila kifungo kwako. Paulo na Sila walipofungiwa gerezali waliamua kumsifu Bwana na kwa kupitia sifa zao milango yote ya gereza ilifunguka na vifungo vyote walivyofungwa viliachia. Kwa kupitia sifa zako milango ya baraka itafunguliwa kwako na kila kifungo kilichofunga maisha yako kitaachia na wewe utakuwa huru.