KUHUSU EFATHA?

Marko 7:34 akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka.

Kanisa la Efatha, ambalo hapo awali lilijulikana kama Huduma ya Efatha, likiwa na msingi wa kitume na kinabii, lilianzishwa mwaka 1996 na kusajiliwa rasmi kama huduma hapa Tanzania mwaka 1997. Mnamo mwaka 2021, lilipata usajili rasmi kama kanisa.

Mafundisho yanayotolewa wakati wa ibada za Efatha ni ya kitume na kinabii, yakifuatana na udhihirisho wa nguvu za Mungu katika kuokoa, kukomboa, kuponya, na kuweka huru wale waliotwaliwa na nguvu za giza

Kanisa la waabuduo

Kanisa la Efatha lilianzishwa na Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, ambaye ni Mtume Mkuu wa kanisa hili.

Mafundisho yanayotolewa wakati wa ibada ni ya kitume na kinabii, yakifuatana na udhihirisho wa nguvu za Mungu katika kuokoa, kukomboa, kuponya, na kuweka huru wale waliotwaliwa na nguvu za giza. Mwanzoni, kanisa hii halikuwa na maeneo yake ya ibada, bali ilitegemea kukodi au kuazima kumbi kutoka kwa wale waliounga mkono kanisa hii. Muundo wa ibada ulianza katika kituo kilichopo Mji wa Moshi, na baadaye huduma hii ilienea katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na: Arusha (Mererani, Mji wa Arusha, King’ori), Morogoro (Mji wa Morogoro, Kilombero), Iringa (Mji wa Iringa, Ilula), Mkoa wa Pwani (Kibaha), Dar es Salaam (Sinza Mori), Kilimanjaro (Machame, Sanya Juu), Mbeya (Mji wa Mbeya), Kenya (Nairobi – Dandora), Mwanza (Mji wa Mwanza)

Hadi kufikia mwaka 2021, kanisa  lilikuwa imeshaanzisha vituo vya ibada 670 ndani na nje ya nchi, ambapo asilimia 90% ya vituo hivyo vilikuwa na majengo ya kudumu ya ibada, na asilimia 30% ya vituo hivyo vilikuwa na makazi ya wachungaji. Mafanikio haya yalitokana na kutambua nyakati na majira ya kuchukua hatua, pamoja na utayari wa Kiongozi Mkuu na wale walio chini ya uongozi wake.

Uponyaji na Ukombozi kwa Damu ya Yesu.