Naitwa Patrick namshukuru Mungu kwa kuwaokoa wazazi wangu ambao walikuwa wanaamini sana nguvu za giza.
Pia namshukuru sana Mungu kwa neno la Mtumishi wake Thabo Masenya, katika kusanyiko kuu la mwaka 2021 alisema ifike wakati sisi wana Efatha tuzalishe bidhaa zetu wenyewe, kuanzia hapo nilichukua hatua na kuanza kilimo cha matikiti na sasa nazalisha matikiti mengi na kupitia matikiti hayo nimeweza kuchangia fedha kwa ajili ya kusafirisha watu kadhaa kuja katika kusanyiko hili ili wakutane na Mungu na waweze kupokea uponyaji wa yale yanayowatesa.