Naitwa Leopadia George, namshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya, nilifanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi, baada ya siku chache mshono ulifumuka na kumwaga usaha mwingi sana na ndipo nilipopoteza fahamu. Nikiwa hospitali magonjwa mengine yakaibuka, mapafu yakajaa maji, figo zikagoma, kuanzia pale nilipoteza fahamu nikakaa ICU kwa muda wa miezi minne.
Namshukuru Mungu kwa ajili ya wachungaji wa Efatha kwani hawakuchoka kuniombea, madaktari walisema hawawezi wamefika mwisho ndipo Baba yangu Josephat Elias Mwingira akatuma ujumbe wenye maneno ya ushindi akasema maneno hayo niyatamke kwa kinywa changu, nilikuwa siwezi hata kuongea, lakini alipoingia mchungaji aliniita nikaweza kuitika akanipa maneno nitamke nikatamka, baada ya hapo nikapokea uponyaji wangu.
Baada ya kuponywa tulimshukuru Mungu kwa kuimba na kucheza pale wodini. Hakika Mungu wa Efatha ni Mungu anayefungua watu.