Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Nimepona miguu toka utotoni ilikuwa inavimba na kuuma sana

Naitwa Hapiness Shedrak napenda kumshukuru sana Mungu kwa kunikomboa kutoka katika kifungo cha magonjwa, tangu nilipokuwa mdogo niliugua miguu ilikuwa ikiumuka na ndani kulikuwa kama kuna usaha, nilikuwa natoka malengelenge na nikikanyaga chini ilikuwa kama nakanyaga moto, nimehangaika kila mahali mpaka kwa waganga lakini hawajawahi kunisaidia. Ndipo niliamua kuokoka, baada ya kuokoka nikawa naenda kwenye maombi, nakumbuka ilikuwa ni tarehe 27/5/2023 ilikuwa ni kipindi cha maombi ya mfungo, nilikuja hapa kanisani nilishinda siku nzima uweponi mwa Bwana, nilimwambia Mungu leo ni siku yangu ya mimi kumalizana na misiba yote inayonitesa, na hii ndio ilikuwa siku ambayo niliponywa miguu yangu kabisa. Namshukuru sana Mungu kwa maana haikuwa rahisi kwangu kutokana na maumivu niliyopitia kipindi chote hicho, lakini siku moja tu Mungu akanifungua na nikawa na furaha tena.
Pia sikuwa namjua baba yangu, mama yangu alifariki nikiwa na umri wa miaka miwili tu, nimekulia katika familia ya mama yangu, nilikuwa simjui kabisa baba yangu lakini baada ya kuokoka nilimtafuta baba yangu na nikamjua nikafanikiwa kukutana na ndugu zangu wengine, namshukuru sana Mungu kwa matendo yake aliyofanya katika maisha yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*