Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

2024 NI WAKATI WAKO WA KUFURAHI.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 8/1/2024.
Mungu anakwenda kuzaa Mambo Mapya katika maisha yako hivyo utakwenda Kung’aa. Leo ni siku mpya ya Kugeuka kwako, ni siku ya Kung’aa kwako, ni siku ambayo Mungu amekupa kutiisha adui zako.
Ibada yako ya Mwaka huu haitakuwa ya kawaida, utakwenda ibadani ukiwa umechoshwa na mambo lakini utarudi nyumbani ukiwa Huru katika hayo mambo. Utakwenda Ibadani ukiwa na Imani unataka jambo fulani litokee kwako na litatokea, hautakwenda na kulia bali kwa wewe kutokea tu Kanisani adui ambaye alikuwa anakukandamiza atakuachia pasipo wewe kumwambia akuachie, kwa sababu Nguvu ya Roho Mtakatifu itakufunika na kusababisha mambo hayo kutokea kwako na ibilisi hatakuwa na nguvu tena kwako.
Magonjwa ambayo madaktari wamekwambia kuwa unapaswa kufanyiwa upasuaji kamwe hautafanyiwa upasuaji kwa maana Mungu wako ni Tabibu Mkuu, atakufanyia upasuaji Yeye mwenyewe.
Ili hayo yote yatokee kwako wewe unapaswa kuwa Mwaminifu katika kile ambacho Mungu anachokisema, Mungu akisema fanya hiki kupitia Watumishi wake wewe fanya usisubiri mpaka Yeye ashuke na kukwambia kitu ndipo ufanye kwa maana ametuweka hapa duniani sisi Watumishi wake ili aweze kusema na wewe hivyo unapaswa kutii.
Muda wa huzuni kwako UMEKWISHA huu ni wakati wa Kufurahi mwanangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*