Baraka kutoka kwa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Baraka kutoka kwa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Sasa ninaachilia baraka ambazo Mungu amenipa ili niweze kutembea nazo, zije juu yako kwa jina la Yesu Kristo. Neema ambayo Baba yangu wa Mbinguni amenipa, sasa nakuachia. Nakubariki ili asiwepo yeyote atakayesimama dhidi yako kwa jina la Yesu. Yeyote au chochote kitakachoinuka dhidi yako, Mungu atainuka dhidi yao. Kila kitu kitakachoinuka kukushambulia, Mungu atainuka kukishambulia. Mlango wowote uliokuwa umefungwa, sasa naufungua kwa jina la Yesu. Kila ukuta uliokuwa umejengwa mbele yako, nauangusha kwa jina la Yesu. Mamlaka yoyote inayokukandamiza na kukutendea vibaya, naiinamisha mbele yako kwa jina la Yesu.

Ikiwa ni ugonjwa au laana zilizowekwa na mwanadamu au shetani, sasa naziangamiza kwa jina la Yesu. Pokea baraka zako; barikiwa na baraka za kitume na kinabii. Baraka kwa wingi zitaambatana nawe popote uendapo. Upokee kila kitu ulichotamani. Neema ikutangulie popote uendapo.

Mahitaji yoyote yanayohitajika kwa ajili ya biashara yako uyapokee sawasawa na hitaji lako, kibali changu na kikutangulie. Kampuni yoyote unayotamani kumiliki, na chochote unachohitaji ili kampuni hiyo istawi, sasa nakuruhusu iwe yako. Kila kitu unachotamani kufanya ili moyo wako ufurahi, na kiwe chako kwa jina la Yesu.

Biashara kubwa zitakujia; kampuni kubwa zitakujia. Kila aina ya neema unayoitafuta imeamriwa kuja kwako. Kuanzia sasa, hutakataliwa popote. Nenda ukafurahi na ufurahie kwa jina la Yesu.

Hutateseka tena na mateso yaliyokusumbua jana, wala hali iliyokukandamiza, kwa kuwa Bwana anakwenda kukuokoa kutoka kwenye dhiki zako.

Add Comment