Ni wakati wako wa kumiliki

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Yohana 15:5 “ Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.”
Ukikaa katika mzabibu mwema ambaye ni Baba wa mbinguni Yeye atakupa kumiliki lakini ukikaa nje yake yaani katika mzabibu mwitu utazaa matunda ya dunia hii ambayo ni ya uharibibifu na kamwe hautaweza kumiliki milki zako alizokukusudia Baba yako wa Mbinguni.
Biblia inasema “maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote”, ukiona kuwa hauwezi kufanya chochote jua kuwa huenda umeokoka lakini haupo ndani ya wokovu.
Siku zote mtoto anapokaa tumboni mwa mama yake wakati wa yeye kutoka unapofika anatoka hata kama mama hataki; hivi ndivyo itakavyokuwa kwako; huu ni wakati wako wa kumiliki, hata kama wamekufunga kwa kiasi gani ili usiweze kumiliki wakati wako wa kutoka umefika. Kuna watu wamefungiwa mahali kwa miaka mingi lakini safari hii wanaenda kukuachia nawe lazima utoke ili uweze kumiliki.
Mwanangu unakwenda kutoka katika nyumba ya kupanga, hali ya kudandia bajaji kila siku inaenda kuisha kwako. Mungu anaenda kukupa usafiri wako, hali ya kusubiri kusaidiwa kila siku ndipo uishi unaenda kutoka hapo kwa sababu wakati wako wa kutoka na kumiliki umefika. Mungu akakupe nguvu ya kutoka ili upate kumiliki milki zako.

Add Comment