Linda sana moyo wako

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”
Mafanikio hayatokani na fedha unazozalisha, wala vitu ulivyonavyo bali yanatokana na wewe ulivyo ndani yako, kama wewe ni mtu wa kushindwa ndani basi utashindwa na nje, lakini kama wewe ni mshindi ndani basi utashinda na nje. Mara zote ibilisi anapenda kukudhoofisha ndani ili uwe mpotezaji nje. Kama kuna kitu unapaswa kukilinda sana ni moyo wako, linda moyo wako maana humo ndimo zilipo Nguvu za mafanikio, Nguvu za ushindi wako zipo hapo.
Ndani ya moyo wako ndipo nguvu zako zilipo, ukipoteza nguvu zako za ndani basi hata nje wewe ni mpotezaji, usiruhusu hilo litokee kwako. Mungu anakupenda zaidi ya unavyofikiri na kamwe usiruhusu nguvu za yule adui zikudanganye kuwa Mungu hakupendi.

Add Comment