Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mungu anaweza kubadilisha maisha yako.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 20/10/2023.
Yeremia 32:27 “Mimi ndimi BWANA, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza?”
Mungu tunayemtumikia ni Mungu aliye Mkuu sana, Muumba wa Mbingu na Nchi, YEYE aliumba na itabaki kuwa hivyo hakuna awezaye kubadilisha alichokifanya. YEYE ndiye chanzo cha kila kitu huku duniani na ndiye chanzo cha maisha yako, ndiye anayejua siku zako na maisha yako, hakuna kinachojificha mbele zake.
Mungu ninayemzungumzia ni yule aliyemtumia Eliya kufanya miujiza mingi na hata kushusha moto, alisababisha Daudi kumuua Goliati kwa jiwe dogo tu. Alisababisha Samsoni kuua maelfu ya askari na ndiye aliyemfufua Lazaro kutoka katika wafu, huyu ni Mungu aliyefanya Mariamu akapata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Yeye anaweza kukubadilisha na kukufanya vile anavyotaka uwe, YEYE ndiye aliyemfanya Sara apate mtoto katika uzee wake, ndiye Mungu aliyemfufua Yesu kutoka katika wafu na kumuweka mahali pa juu kule Mbinguni.
Mungu huyu huyu ndiye aliyekuumba wewe na anataka kubadilisha maisha yako yawe bora kwa ajili ya Utukufu wake. Mungu ana uwezo wa kukubadilisha na akikubadilisha sasa ni mpaka milele, ndiye Mungu aliyenichagua ili niwe Mtumishi wake. Hutakuwa kama ulivyokuwa tena, yule aliyenibadilisha Mimi na kunifanya kuwa Mtumishi wake atakubadilisha na Wewe katika JINA la YESU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*