Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mungu ni pendo

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 18/10/2023.
1 Yohana 4:10-11 “Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba Yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.”
Kama vile Mungu alivyotupenda kwa dhati nasi tupendane ili mapenzi ya Mungu yatimie hapa Duniani na Mbinguni. Hili ndilo Pendo Kuu kupita pendo lolote lile. Pendo hili la Mungu likijaa ndani yetu basi litavuta watu kwa Mungu, kwa sababu Pendo lina mvuto.
Mwanangu pata ufahamu kuwa Mungu anakupenda sana, usiruhusu mazingira, hali unayopitia au kinywa kikulaani kuwa hupendwi, la! Unapendwa sana na Mungu, kwa sababu YEYE ni Pendo.
Pendo la Mungu limetufanya tutambulike kama Wana wa Mungu, kwa kuwa Mungu alimtoa Mwanaye wa Pekee YESU KRISTO ili alipe madeni yetu na kutuweka mbali na dhambi kupitia Msalaba; wewe uliyeokoka umefanyika kuwa Mwana wa Mungu jivunie katika hilo. Usilalamike kuwa haupendwi maana namna ujionavyo nafsini mwako ndivyo ulivyo, hivyo tambua kuwa unapendwa.
Katika yote jifunze kutembea katika Pendo maana Mungu ni Pendo YEYE ndiye heshima yetu, hivyo enenda katika Pendo. Kila siku kinywa chako kiwe na ukiri kuwa unapendwa na Mungu kwa sababu Mungu ni Pendo na anakupenda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*